Sabodo kuchimba visima mia saba tanzania nzima

mundo

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
200
9
Mfanyabiashara mashuhuri nchini leo ametangaza rasmi kuwa atajitolea msaada kuchimba visima 600 nchi nzima, baada ya tamko hilo waziri wa maji mh mwandosya alimtembelea nyumbani kake upanga kumshukuru kwa uzalendo wake ndipo alipoongeza visima vingine 100 ambavyo vitachimbwa mkoani mbeya tu. gharama jumla itakuwa Tsh.2bn. alionekana mwenye furaha wakati akipeana mikono na waziri, kukusitiza anafanya hivyo kufuata nyayo za baba yake ambaye alikuwa rafiki wa mwalimu na akaongelea jinsi nelson mandela alivyokuja kuitembelea familia yao miaka ya tisini.


source:ITV saa 2 usiku
 
Angekuwa kijana kijana ningesema anataka kutangaza nia..Lakini kwa umri wake naamini ni msaada wa ukweli...!
Mungu ambariki sana huyu mzee, maana ameamua kuwa wa msaada kwa jamii!
 
huo msaada wa Sabado kwa Prof. Mwandyosa utaleta manung'uniko ya chini kwa chini ndani ya CCM haswa ya wale...wanaojipanga 2015!
 
vile vile ameteua kamati yake yenyewe ambayo itasimamia mchakato mzima, nadhani tutaiona soon!
nadhani anaielewa nchi vizuri kwa kuamua kufanya hivyo.
 
Angekuwa kijana kijana ningesema anataka kutangaza nia..Lakini kwa umri wake naamini ni msaada wa ukweli...!
Mungu ambariki sana huyu mzee, maana ameamua kuwa wa msaada kwa jamii!

Hata akitangaza nia kwangu mimi Mzee SABODO namuona kama Mwanamapinduzi....
 
wazee wente nia nzuri kama hawa hawafiki mbali...watazushiwa mizengwe hadi utasikia presha imempanda....mara malengo yake yanaharibiwa....Hivi tutaweza kupata akina sabodo wengine?
Mungu ampe afya na uzima mrefu.
 
wazee wenye nia nzuri kama hawa hawafiki mbali...watazushiwa mizengwe hadi utasikia presha imempanda....mara malengo yake yanaharibiwa....Hivi tutaweza kupata akina sabodo wengine?
Mungu ampe afya na uzima mrefu.
 
Tunataka wahindi wa namna hii, sio mihindi na mi lraq inayotaka kutunyonya hadi tone la mwisho
 
waziri wa maji mh mwandosya alimtembelea nyumbani kwake upanga kumshukuru kwa uzalendo wake ndipo alipoongeza visima vingine 100 ambavyo vitachimbwa mkoani mbeya tu.
source:ITV saa 2 usiku

Huyu Mzee ana utani na Mwandosya nini?
 
Umenikubusha wakati fulani mika ya 90's Nelsom Mandela alitaka kusaidia Mji wa Morogoro kwa kuwela Lami kama ishara ya kushukuru kwa wakazi wa mji huo kuishi vizuri na Raia wa south africa waliopata hifadhi Mazimbu -Morogoro kutokana na Vita vya kupigania uhuru dhidi ya makaburu.

Moja ya masharti ilikuwa ni kwamba -Contactors watatoka SA na kwamba atakachofanya yeye ni kukabidhi Mradi ukiwa umekamilika.

Viongozi wa Mkoa wa Morogoro wakati huo wakakataa na kusema wanahitaji fedha watasimamia Mradi huo wao, Mzee mandela akachomoa!!!

Angalizo: Hali hii isije Kurudiwa katika miradi mbalimbali inayotolewa na kama Msaada!
 
Tunataka wahindi wa namna hii, sio mihindi na mi lraq inayotaka kutunyonya hadi tone la mwisho

Hii kali sasa!
Hadi makanjubhai ndio wasaidie ....wazalendo wengine wa masharki mwa tz wanasaidia wapi?
Hii ni Tsunami ya akili zetu?
Yule jamaa wa Haki Elimu nae ni mwarabu?
 
Huyo ni miongoni mwa Wahindi wchache walioamua kuwa Watanzania wa kweli na wenye uchungu na hii nchi, kwa kweli wapo wachache sana Issa Shivji, Alnoor Kassam, Sabodo nk
 
Kama mtakumbuka mwaka jana mzee sobodo alitoa zaidi ya TShs 300 mill kwa ajili ya kuchimba visima vya maji safi ktk majimbo yote ya CDM nchini sijui mradi huu umeanza? Na umefikia wapi? Kama bado why? Naomba kujuzwa jamani
 
Back
Top Bottom