Angalia CCM walichofanya; Sabodo ni mwana-CCM wa muda mrefu na ametoa michango mikubwa sana kwenye chama cha mapinduzi, vilevile ametoa visima 100 kwa Prof. Mwandosya, na kwa kuungwana wa Prof. Mwandosya amevitoa vyote na kuumpa waziri wa maji, lengo lake ni visima hivyo vihudumie taifa kwa ujumla. Angalia CHADEMA walichofanya; Masikitiko yangu yanaenda kwa CHADEMA, wamepokea visima kutoka kwa Sabodo, visima zaidi ya 200, lakini cha kushangaza, wamejenga visima hivi kwenye maeneo waliyotoka wao tu. Viongozi wa CHADEMA wamethibitisha ubinafsi wa hali ya juu sana, wajirekebishe. Huwezi kupewa msaada mkubwa hivi, halafu unaupeleka kwenye eneo ulilozaliwa, huu sio umoja tulionao watanzania. Ubinafsi wa namna hii unapelekea hali ya wananchi kuona viongozi wa CHADEMA kweli ni wahumini wa ukanda. Ndambi mbaya sana iliyokemewa na baba wa taifa.[ Na vile vile ukumbuke chadema hailokoti kodi kwa wanachi! Sidhani kama kuna baba atakayewavalisha watoto wa jirani huku watoto wake wakifa kwa njaa!