Sabodo aishukia serikali!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo aishukia serikali!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Abdillahjr, Apr 30, 2012.

 1. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sabodo aishukia serikali
  Naye kada maarufu wa CCM na mfanyabiashara maarufu nchini Mustapha Sabodo, aliyealikwa katika mkutano huo, aliishukia serikali ya CCM akidai kuwa viongozi wake hawana shukrani kwa namna alivyojitolea kwa miaka 50 kuisaidia kwa kila njia. Sabodo alisema hajawahi kupewa hata ‘asante' na viongozi wa CCM, pamoja na kuipa msaada wa mabilioni ya fedha, hali ambayo imemsikitisha. "Mimi si mwanasiasa na hata wakati wa uhai wa Baba wa Taifa (Mwalimu Nyerere) nilitaka kupewa uwaziri na baadaye uenyekiti wa benki ya NBC nikakataa kwa sababu mimi ni mfanyabiashara lakini juu ya yote hawajui hata kusema asante kwa niliyowafanyia," alisema Sabodo.

  Sabodo alikiri kuwa CHADEMA imeonyesha kuwa ni chama makini, kinachopigania maslahi ya Watanzania na kuthamini mchango wa kila mtu bila ubaguzi, na kudai kuwa atawafuata marafiki zake akiwemo waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba na kuwaeleza umuhimu wa kuiangalia CHADEMA kama chama kinacholenga kuwakomboa wanyonge. Aliahidi kuzidisha misaada zaidi kwa CHADEMA, na kukumbushia ahadi yake ya kuwapatia jengo la kisasa kwa ajili ya ofisi.Alisema dhana kuwa chama hicho ni cha kidini ni propaganda za watu walioshindwa kwenda na kasi yake na kutaka kutumia nafasi ya kuwachonganisha wananchi ili wapate kuwatawala milele."Wanasema CHADEMA inabagua dini huo ni uongo na ninakuombeni muendelee kupambana CHADEMA hoyeee!" alisema Sabodo huku wajumbe wa baraza kuu wakimshangilia.

  Awali katibu mkuu wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa akiuelezea uzalendo wa Mustapha Sabodo, alisema amekuwa muwazi kwa mambo yake licha ya wafanyabiashara wengi kubaki katika mawazo mgando kuwa mtu anayetaka mambo yake yaende sawa ni lazima awe mwanachama waCCM.Alisema watu wengi wenye uwezo na hata wasomi wamekuwa wakijificha kuzungumzia siasa hususan kwa upande wa upinzani kwa hofu ya kuharibikiwa mambo yao tofauti na Sabodo ambaye ni muwazi kwa kila anachokifanya.Alisisitiza ufisadi wa Tanzania unatokana na mambo mengi kufanywa gizani kwa kuwa hadharani watu wanaogopa wataumbuliwa.

  SOURCE-CHADEMA: Wafuasi wetu 15 wameuawa
   
 2. s

  shadhuly Senior Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 141
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  kwa hiyo babu sabodo kajipambanua nia yake ni kutaka kushukuriwa na kuthaminiwa kwa mchango alioutoa.tatizo inaonekana alikuwa anatoa kwa siri angeita vyombo vya habari ili aweze kuuza zaidi
   
 3. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Wacha waendelee kujaza mikono kwa damu na kikombe chao kitakapojaa ndipo ghadhabu ya Mwenyezi MUNGU itakuwa juu yao.
   
 4. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,458
  Trophy Points: 280
  Better than most. He's done every well-wisher a mammoth of good by standing and supporting CHADEMA openly. Thank you Sabodo
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Pia amekua akitoa ushauri mzuri kwa govt ccm lakini hawaufuati!eg suala la makampuni ya madini na simu kulipa kodi
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sabodo ameshajiunga na CDM kabisaaaa
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Viongozi wa serikali ya magamba pamoja na wabunge wao utawasikia wakipaza sauti kwamba serikali yao ni sikivu lakini hata siku moja haijawhi kuwa sikivu. Nadhani ni sikivu kwa mafisadi na wahujumu rasilimali za nchi!!

  Inapopewa ushauri wa manufaa kwa wananchi wote inaziba masikio, huku viongozi wak ewakifanya mambo yao gizani.
   
 8. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Siyo dhambi!
   
 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  CCM mawazo mgando kabisa. Lazima utambue mchango wa mtu, sasa CCM hata kama walipewa michango wao wanadhani ni haki yao
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hahaaa nimeipenda hiyo Tags hapo chini
   
 11. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hii Sir Bodo janja sana.Veve kama iko akili dogo weza gundua kuwa hii ni janja ya Hindi yooote kuasapot Chadema. Hindi yote kusha jua kuwa hii M4C iko pamba moto sana dani ya nchi.
  Toa pesa mingi pitia fuko ya Sir Bodo kisha kama Chadena chukua nchi Hindi yote Chukua nchi. Mr Bodo janja sana.
   
 12. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,186
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  Naweza kusema ni Kweli kuwa hawana Shukrani Maana Mimi nimemjua baada ya Chadema Kuanza Kupewa Misaada ya Sabodo.

  Kumbe alikuwa anatoa Pia CCM... CDM wanashukrani ndo Maana Tunakujua
   
 13. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #13
  Apr 30, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sabodo na CCM nani anapaswa kumshukuru nani iwapo CCM hiyo hiyo imemfuga kumlea na kumtajirisha? Kwanini Sabodo asiwe mkweli kuwa anatafuta pa kushika iwapo mambo yataharibika? Kama anaipenda CHADEMA na kuiponda CCM kwanini haaminii CHADEMA? Huyu jamaa atawachafua CHADEMA wasipoangalia. Hawa jamaa huwa hawana adui wala rafiki wa kudumu bali maslahi. Acha wengine waseme lakini si Sabodo na wenzake ambao wanatafuta kuweka vyama vyote vinavyoonekana kuweza kuchukua dola au kubaki na dola ili baadaye waendelee kupewa dili zao. Uliza nyuma ya uchafu wa rada, ndege ya rais, Richmond, IPTL na ujambazi wote wa mabilioni kuna nani kama siyo wao.
   
 14. kalamata

  kalamata Senior Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hongera ndugu yangu umeona mbali kweli.Hawa jamaa wana akili sana.Mfano mzuri ni pale wengi wao walipoingia kwenye Michezo hususani vilabu vyetu vya mpira wa miguu, wengine kufikia hadi kua wenyeviti wa vilabu vyetu vikubwa hapa nchini,lakini baada ya kupata lile waliolitaka leo wako wapi?hata hatuwasikii tena,sasa wameshaanza kujipanga kabisa katika mambo ya siasa kwa sababu wanafahamu KWEYE UDHIA PENYEZA RUPIA.
   
 15. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kada wa CCM na ataendelea kuwa kada
   
 16. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #16
  May 2, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Ndugu unamuongelea Sabodo au Wahindi kwani wahindi wote si sawa, watu wenye asili ya Africa wote si sawa pia!. Ni ubaguzi wa kijinga kuweka watu wote kwenye chungu kimoja kwasababu ya rangi zao. Richmond inahusika vipi na Sabodo kama hii siyo race tu.
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  May 2, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ur right nakubaliana na wewe....mzee reginald mengi alishasema kua hata siku moja usimuamini mhindi coz hawa watu always wako pale kwa maslahi yao its always about them and their interests....
   
 18. i

  iMind JF-Expert Member

  #18
  May 2, 2012
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Is no longer kada wa ccm. Ni kada wa maarufu wa chadema
   
 19. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #19
  May 2, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Angalia hapa!
   

  Attached Files:

Loading...