Sabaya aanza kujitetea Mahakamani, adai siku ya tukio alikuwa ofisini kwake Hai

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Shahidi wa 3, Lengai Ole Sabaya{35} ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro anayekabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi leo ameanza utetezi wake katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake sita na kudai kuwa januari 22 mwaka jana hakuwepo eneo la tukio alikuwa ofisini kwake Boma Ng’omba kuanzia saa 1.30 hadi saa 11 jioni na hakuwahi kutoka katika wilaya hiyo.

Sabaya alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake, Mosses Mahuna mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda na kusema kuwa kikanuni, sheria na miongozo hawezi kutoka bila kibali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Shahidi huyo ambaye alidai ni Mkazi wa Sakina Jijini Arusha alidai kuwa aliteuliwa Rais kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai julai 27 mwaka 2018 na alihudumu katika kazi hiyo kwa muda wa miezi 32 kabla ya kusimamishwa na Rais mei 13 mwaka jana alidai aliyesema kuwa alikuwa Arusha alisema Uongo.

Alidai siku ya januari 22 mwaka jana alifuatwa na dereva wake Thomas Kivuyo na gari ya serikali na alimuaga mke wake Jesca Thomas Nassari kuwa anakwenda kazini na aliingia muda was aa 1.30 na alitatua mgogoro wa wafugaji na wakulima hadi saa 11 jioni na baadae alirudi nyumbani.

Sabaya ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alidai kuwa hakutoka tena siku hiyo nyumbani kwani siku hiyo ilikuwa ijumaa yeye ni muumini wa dhehebu la Kisabato na muda huo ulikuwa tayari wa maombi kwa ajili ya siku ya ibada ya Jumamosi ya januari 23 mwaka jana.

Alipoulizwa na Wakili wake Mahuna kuwa kuna shahidi wa tatu, nne, tano wa upande wa Jamhuri katika Ushahidi wao waliieleza Mahakama kuwa januari 22 mwaka huu ulikuwa Jijini Arusha katika gereji ya Mfanyabiashara Francis Mrosso, Sabaya alidai kuwa mashahidi hao watakuwa waongo kwani siku hiyo alikuwa ofisini akiwajibika na mgogoro wa wafugaji na wakulima.

Sabaya alidai kuwa kwa mujibu wa kanuni,sheria na miongozo ya Wakuu wa Wilaya kote Nchini huwezi kutoka nje ya kituo cha kazi bila kibali kutoka kwa Katibu Msaidizi Rasilimali watu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyemtaja kwa jina la Lenatus Msanjira naye ampe taarifa Katibu Tawala wa wilaya kwa taratibu zingine za kilojistiki na sio vinginevyo.

Alidai na ndio maana Msanjira ambaye alikuwa shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri katika Ushahidi wake alidai kuwa hakuwa na taarifa yoyote ya yeye kutoka nje ya Wilaya yake kwa kuwa hakutoa kibali hicho.

Sabaya alidai utaratibu wa Mkuu wa Mkoa kutoka katika kituo chake cha kazi ni lazima apate kibali cha maandishi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa nay eye kama Mkuu wa Wilaya kipindi hicho hakufanya hivyo kwa kuwa hakutoka nje ya wilaya siku hiyo.

Alidai shahidi wa 13, Ramadhani Juma ambaye ni Mchunguzi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Arusha{TAKUKURU} na Mpelelezi Mkuu katika kesi hiyo aliposema siku ya Januari 22 mwaka jana alikuwa Jijini Arusha katika gereji ya Mfanyabiashara Mrosso akiwa na na gari ya serikali STL 5434 ni uongo.

Awai shahidi wa 2 wa upande wa Utetezi katika kesi hiyo mke wa Sabaya,Jesca Nassari{27} wakati akihojiwa na Waendesha Mashitaka Waandamizi wa Serikali, Tasilia Asenga, Ofmed Mtenga, Janeth Sekule na Neema Mbwana alidai kuwa pesa alizokuwa nazo mume wake Sabaya na kununuwa magari na mali nyingine zilitokana mauzo ya mifugo na mazao.

Alidai hata wakati anakuja na pesa nyumbani hakuweza kumuuuliza kuwa alikuwa amezipata wapi kwani kwa mila za jamii ya kifugaji ya Kimasai huwezo kuhoji chochote na hakuwa na wasiwasi juu ya hilo kwakuwa alikuwa na mifugo na mazao na biashara ilikuwa ikifanyika.

Shahidi huyo wa pili alidai kuwa alikabidhi TAKUKURU kadi ya gari aina ya VX V8 Toyota Land cruiser yenye namba za usajili T222BDW mali ya sabaya pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 10 na hakuwa na Ushahidi wowote ulionyesha kuwa alikabidhi mali na pesa hiyo.

Wakati Sabaya akianza utetezi wake leo mke wake, Jesca Thomas alifunga ushahidi wake baada ya kumaliza kuulizwa maswali ya dodoso na jopo la Mawakili watano wa Jamhuri.

Jesca ambaye ni shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 inayomkabili Sabaya na wenzake sita alianza kutoa ushahidi jana katika kesi ambayo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa upande wa washitakiwa kujitetea.

Ends...
 
Huyu jamaa anajitambua au hajitambui? Hivi ukiuza mifugo au mazao hupewi risiti? Mbona anatengeneza JINAI nyengine?
 
Uyu Sabaya katika upigaji wake lazima alipiga sehemu yamoto , huo moto ulikuwa umezungukwa na diesel na petroleum,
 
Mambo yanakua wazi with time. Mama mla kwa urefu wa kamba yake ndio kwa kuchukizwa na makomredi kaanza na sabaya aliponyakua usukani wa nchi tu.

Sasa imedhihirika mama ni antimagufulist na halali kuwaza namna ya kuwamwaga magufulists wote serikalini. Ila ni muoga nguvu kiitikadi ya magufuli ni dharuba. Siku itafika atajuta kuzaliwa kwa aibu.
 
Shahidi wa 3, Lengai Ole Sabaya{35} ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro anayekabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi leo ameanza utetezi wake katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili yeye na wenzake sita na kudai kuwa januari 22 mwaka jana hakuwepo eneo la tukio alikuwa ofisini kwake Boma Ng’omba kuanzia saa 1.30 hadi saa 11 jioni na hakuwahi kutoka katika wilaya hiyo.

Sabaya alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake, Mosses Mahuna mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Patricia Kisinda na kusema kuwa kikanuni, sheria na miongozo hawezi kutoka bila kibali kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Shahidi huyo ambaye alidai ni Mkazi wa Sakina Jijini Arusha alidai kuwa aliteuliwa Rais kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai julai 27 mwaka 2018 na alihudumu katika kazi hiyo kwa muda wa miezi 32 kabla ya kusimamishwa na Rais mei 13 mwaka jana alidai aliyesema kuwa alikuwa Arusha alisema Uongo.

Alidai siku ya januari 22 mwaka jana alifuatwa na dereva wake Thomas Kivuyo na gari ya serikali na alimuaga mke wake Jesca Thomas Nassari kuwa anakwenda kazini na aliingia muda was aa 1.30 na alitatua mgogoro wa wafugaji na wakulima hadi saa 11 jioni na baadae alirudi nyumbani.

Sabaya ambaye ni mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alidai kuwa hakutoka tena siku hiyo nyumbani kwani siku hiyo ilikuwa ijumaa yeye ni muumini wa dhehebu la Kisabato na muda huo ulikuwa tayari wa maombi kwa ajili ya siku ya ibada ya Jumamosi ya januari 23 mwaka jana.

Alipoulizwa na Wakili wake Mahuna kuwa kuna shahidi wa tatu, nne, tano wa upande wa Jamhuri katika Ushahidi wao waliieleza Mahakama kuwa januari 22 mwaka huu ulikuwa Jijini Arusha katika gereji ya Mfanyabiashara Francis Mrosso, Sabaya alidai kuwa mashahidi hao watakuwa waongo kwani siku hiyo alikuwa ofisini akiwajibika na mgogoro wa wafugaji na wakulima.

Sabaya alidai kuwa kwa mujibu wa kanuni,sheria na miongozo ya Wakuu wa Wilaya kote Nchini huwezi kutoka nje ya kituo cha kazi bila kibali kutoka kwa Katibu Msaidizi Rasilimali watu wa Mkoa wa Kilimanjaro aliyemtaja kwa jina la Lenatus Msanjira naye ampe taarifa Katibu Tawala wa wilaya kwa taratibu zingine za kilojistiki na sio vinginevyo.

Alidai na ndio maana Msanjira ambaye alikuwa shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri katika Ushahidi wake alidai kuwa hakuwa na taarifa yoyote ya yeye kutoka nje ya Wilaya yake kwa kuwa hakutoa kibali hicho.

Sabaya alidai utaratibu wa Mkuu wa Mkoa kutoka katika kituo chake cha kazi ni lazima apate kibali cha maandishi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa nay eye kama Mkuu wa Wilaya kipindi hicho hakufanya hivyo kwa kuwa hakutoka nje ya wilaya siku hiyo.

Alidai shahidi wa 13, Ramadhani Juma ambaye ni Mchunguzi katika Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Arusha{TAKUKURU} na Mpelelezi Mkuu katika kesi hiyo aliposema siku ya Januari 22 mwaka jana alikuwa Jijini Arusha katika gereji ya Mfanyabiashara Mrosso akiwa na na gari ya serikali STL 5434 ni uongo.

Awai shahidi wa 2 wa upande wa Utetezi katika kesi hiyo mke wa Sabaya,Jesca Nassari{27} wakati akihojiwa na Waendesha Mashitaka Waandamizi wa Serikali, Tasilia Asenga, Ofmed Mtenga, Janeth Sekule na Neema Mbwana alidai kuwa pesa alizokuwa nazo mume wake Sabaya na kununuwa magari na mali nyingine zilitokana mauzo ya mifugo na mazao.

Alidai hata wakati anakuja na pesa nyumbani hakuweza kumuuuliza kuwa alikuwa amezipata wapi kwani kwa mila za jamii ya kifugaji ya Kimasai huwezo kuhoji chochote na hakuwa na wasiwasi juu ya hilo kwakuwa alikuwa na mifugo na mazao na biashara ilikuwa ikifanyika.

Shahidi huyo wa pili alidai kuwa alikabidhi TAKUKURU kadi ya gari aina ya VX V8 Toyota Land cruiser yenye namba za usajili T222BDW mali ya sabaya pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 10 na hakuwa na Ushahidi wowote ulionyesha kuwa alikabidhi mali na pesa hiyo.

Wakati Sabaya akianza utetezi wake leo mke wake, Jesca Thomas alifunga ushahidi wake baada ya kumaliza kuulizwa maswali ya dodoso na jopo la Mawakili watano wa Jamhuri.

Jesca ambaye ni shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi namba 27/2021 inayomkabili Sabaya na wenzake sita alianza kutoa ushahidi jana katika kesi ambayo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa upande wa washitakiwa kujitetea.

Ends...

Sabaya ni mtu.hatari sana.,Kuna wskati alijifanya kuwa ni afisa wa usalama.wa taifa mpaks na kitambulisho.alikuwa nacho lakini kwa kuwa.alikuwa katibu wa uvccm alilindwa na kesi iliyeyuka.Lakini kwa nini.aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ?.Nani alaumiwe kwa hilo ?Je ni mwendazake au ni washauri wake kama kweli walikuwepo ?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom