SabaSaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SabaSaba

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndahani, Jul 7, 2010.

 1. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Sabasaba ndio inakwenda kwenda mwishoni. Naamini kwa wale waliobahatika kutembelea mabanda ya maonyesho watakuwa wameona na kujifunza mambo mengi tofauti. Kwa mtazamo wangu, bado tuna safari ndefu ya kuimarisha viwanda vyetu vya ndani ili tuweze kuwa na uzalishaji wa kutosha. Bidhaa za ndani zilikuwa chache kuliko toka nje ambazo zililenga kupata masoko ya uhakika.
  Katika mabanda yote, banda la JKT lilinifurahisha kwa kuwa na vitu vilivyotengenezwa hapa hapa tena kwa ustadi mkubwa.
  Na lile la wakubwa zao au kaka zao, JWTZ, nalo lilikuwa zuri maana lilionyesha mambo mengi yanayofanywa na Jeshi katika kipindi cha amani.Lilinikumbusha geshi lile ambalo tulilizoe enzi tuko katika vikundi vya "komsomol" miaka michache iliyopita.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jul 7, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndahani.. miye tatizo langu ni genius gani aliyeamua kuua "Sabasaba" na kuifanya kuwa ni siku kuu ya Dar peke yake? Na ni nani aliyepata ujiniasi na kuanzisha nane nane. Kwanini Siku Kuu ya Sabasaba isiwe "MAONESHO YA KILIMO NA BIASHARA" na kuyarudisha kama yalivyokuwa zamani tu huku kila mkoa hata wilaya kuwa na viwanja vyao vya sabasaba?
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Mammbo gani JWTZ na JKT wanafanya . unaweza kuwa specif japo kidogo.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Miaka nenda rudi naona kila mara wako dar tu!
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  hiyo nane nane yenyewe huwa nashindwa kuielewa...badala ya maonyesho ya kilimo, huwa kumejaa bidhaa kibao za kichina, mitumba na mabaa ya kutosha........kweli Tanzania ni zaidi ya niijuavyo
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ni hawa makamanda wa zamani waliopata ubatizo mpya wa kileo ndio walioua sikukuu za miaka ilee. Sabasaba imekufa imekuwa ni kuuza bidhaa za nje. Mikoani ndio hivyo tena labda kilimo kwanza kama kitawakumbuka 2015.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  JKT wanavitu vingi wanatengeneza ambavyo naamini viko katika standard za uhakika kuanzia furniture, nguo, viatu na bidhaa nyingine za kilimo. At least sikuona wanatangaza bidhaa za kichina.
  JWTZ wameweka kuanzia habari ya kazi wanazofanya na kwa nimeelimika sana kwenye namna ambavyo jeshi toka miaka ya zamani lilivyo mpaka hii leo. Kuna huduma za afya, namna ya ushiriki wa jeshi la akiba, huduma za emergency kama zile za ujenzi wa reli ya kati baada ya mvua za mafuriko na kubwa kuliko yote I have seen red and black berets soldiers atleast.
  Kwakuwa walikaa kutusaidia kujua wanalofanya kuliko kutuogopesha kwamba wao ni kina nani, nilipata fursa ya kuwakumbusha umuhimu wa kumaintain historia iliyotukuka ya jeshi hilo. I hope wao hawatakubali kuwa sehemu ya uozo huu tunaouona unaendelea.
   
Loading...