Sababu zinazowafanya wapenzi/wenza kuchokana

Mkichokana msiachane kwa uadui maisha ni mzunguko zimwi likujualo kesho mtapeana connection za maisha kama sio nyie watoto zenu. Ukiwa boss muajiri huwezi mtosa mtoto wa ex wa ujanani aliyekutunuku
Umenena mkuu
 
Hiyo namba 2 ilishanikuta.

Binti alikua anapenda wanaume wanaofuga ndevu nyingi kama rick ross halafu kichwani wananyoa upara pembeni juu wanaacha nywele.. Zile style za Saidi wa Mwanza. Halafu hapendi uvae mara kwa mara suruali za vitambaa, yani anataka uvae jeanz halafu zile za kuchanwa chanwa magotini..

Ingawa mm ndevu ninazo nyingi lakini mazingira yangu ya kazini hayaniruhusu kunyoa style za namna ile. Tukawa tunapishana, namwambia mimi ni daktari, nahudumia wazee na vijana, tena kwa asilimia kubwa wagonjwa wangu ni wazee na kina mama watu wazima, muonekano wa namna hiyo ntaonekana muhuni.

Tulishindwana nikabwaga. Sasa hivi amefanywa mchepuko na dereva malori na kamzalisha bila kumuoa!
Dah pole mkuu!
Huyo shemeji mbona sababu zake hazijai hata kwenye kiganja?
Hulka zake ni za kustaajabisha!
 
Sababu zinazowafanya wapenzi/wenza kuchokana.

1. Mazoea ya kupitiliza ( wengi uwapumbaza na kucha kutenda yale yalio wafanya mwanzo waonane bora iwe ngono, chakula, ukaribu, mawasiliano nk. Mfano umezoea kunyonywa matiti au uume alafu mwenzako saizi anaona kinyaa ni tatizo.

2. Kumlinganisha uliyenaye. Hakuna sumu kama kuwaza kuwa na kitu usichokuwa nacho, ukiwa umempenda mwanamke mwenye makalio madogo alafu ukataka uliyenaye awe na makalio makubwa / kipato cha mchicha sasa unataka biriani. Kumpenda mwanaume wa namna fulani alafu unaanza kump masharti awe namna fulani nk.

3. Kuishi kwa mategemeo makubwa. Kumchukulia binadamu mwenzio yeye ni malaika, anapokukosea huwa unakuumiza kwa kishindo, ile thamani uliyompa utoka mara moja.

4. Kutojua unachokifanya. Ukiwa kwenye mahusiano alafu hujui umefuata nini nalo ni tatizo au unafanya mapungufu yako na hujali kama wewe ni mtu wa mtu ni tatizo, umalaya ama kudanga ni hulka ila siyo sababu ya kumchoka uliye naye. Anayejua anachokifanya ni msiri wa mapungufu yake na dhambi zake kwa mwenza wake.

5. Kuziweke sehemu za siri dhamana kwenye mapenzi. Tutambue ngono unaweza ipata kwa mtu yeyote, sasa unapokosa kingine bora cha kufanywa upende au upendwe ni janga.

6. Mawasiliano mazuri wewe na mwenzako. Kuna watu wanaishi kwa kusikia sana ya nje kuliko ya mwenza /mpenzi wake, kwenye uamuzi siyo utoke kwa mwenziye bali utoke kwa ndugu, rafiki au yeye. Anapenda kutishia "nitakuacha" "naondoka" "nitajiua". Kupaza sauti na kujiona wewe upo sahihi kuliko mwenzio.

7. Kuwaza mabaya na hatima ya mahusiano. Sasa hivi kila mahusiano unakuta wanawaza ipo siku tutaachana, sasa uliwazalo mjinga ndilo linalokutokea. Mtu ameoa/ameolewa lakini anashindwa kufanya maisha yake, muda mwingi anamuwazia mabaya tu mwenziye kama kusalitiwa, kuchunwa, hapendwi n.k.

8. Kuishi kwa nafasi moja katika maisha. Watu tunapaswa wapenzi/wenza wetu wawe pia masela wetu, ndugu zetu, washikaji wetu, washauri wetu, wachekeshaji wetu nk ila unakaa na mpenzi/mwenza hana nafasi nyingine muhimu zaidi ya mapenzi ni shida mtachokana tu.

9. Uoga wa maisha. Ebwana karne hii siyo wanaume siyo wanawake wanapenda mseleleko. Mtu ubinafsi kaweka mbele, hajiongezi, awazi kujenga kwa maslahi ya mwenzie, asaidia chochote ni shida.

10. Kutotambua uliyenaye. Kisaikolojia matatizo ya fedha yanafanya wapenzi kushikana na kupambana sana kimaisha. ila wanapopata fedha, matatizo mengine uzaliwa haswa ya kihisia, ni lazima mtambuane hata angalau inatosha. Unapomjua mwenzio hakupi shida mengine utayapuuza tu maana hayokuwa mageni kwako.

11. Kuwa mtu mwenye ahadi zisizotimia. Kuna watu wamewapa kabisa wapenzi/wenza wao "mr/ miss promise yaani bwana/bibi ahadi. Kuanzia ahadi za maisha, majukumu, ndoa, kuridhishana, zawadi, kufanya au kumfanyia kitu fulani. Vipo vimambo vidogo ila vinakera kama kupiga simu kwa mpenzi alafu anakujibu " ngoja kidogo, muda siyo mrefu nakupigia, alafu hapigi ndiyo ntolee".

Mapenzi ili yaende lazima mengine uyaache yaende yaani uyapuuze ila ukitaka kila kitu kiwe sawa mtavurugana tu na thamani zitashuka tu. Ndio maana inashauriwa muwe na utamaduni wa kuzungumza mahusiano yenu na mstakabali wa maisha yenu mara kwa mara. Kuzungumza ni tiba, kwani uwapa muda wa kukumbushana na kuboresha mawasiliano yenu yanayovunjika.
Mie sichokagi
 
Mkichokana msiachane kwa uadui maisha ni mzunguko zimwi likujualo kesho mtapeana connection za maisha kama sio nyie watoto zenu. Ukiwa boss muajiri huwezi mtosa mtoto wa ex wa ujanani aliyekutunuku
Hakuna ktu km hcho kwa mtu mbinafs
 
Back
Top Bottom