Mapenzi asilia Yana nguvu zaidi ya mapenzi ya kisasa

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,102
1,919
Mapenzi asilia nini? Ni mahusiano baina ya wapenzi yenye kufuata tamaduni fulani iliyopo kwenye jamii walipo au asili ya jamii wanayotoka wapenzi hao. Mfano, kama wapenzi watachagua kuhusiana kimapenzi kama wamasai, maana yake wataishi kwenye mapenzi Yao kwa kufuata tamaduni za kimasai.

Mapenzi ya kisasa ni mahnusiano baina ya wapenzi yenye kufuata tamaduni mpya za kisasa, mahusiano haya Niya kidijitali zaidi. Yanahusisha gharama kubwa ili kufurahishana kwenye mahusiano baina ya wapenzi wenyewe. Ni Yale mapenzi ya baby ninunulie hiki kwenye birthday party yangu nk. Ni mapenzi ya show zaidi.

Mapenzi asilia yanabaki kuwa mahusiano yenye nguvu zaidi ya mapenzi ya kisasa, kwasababu zifuatazo:-
1. Yanadumu zaidi kuliko ya mapenzi ya kisasa, wapenzi wanaoishi mahusiano asilia huvumiliana na hawana kesi nyingi.

2. Wanaume wengi huvutiwa na wanawake wanaoishi natural, ikitokea mwanamke akaanza kuishi kisasa, mwanaume hukosa kujiamini akiamini tayari mwenza wake anamdanganya

3. Wanawake wengi pia hufurahia wanaume wanaoishi natural,wengi huamini wanaweza mambo ya kikubwa kuliko wanaume wanaoishi maisha ya kisasa

4. Mahusiano asilia huonekana kama maisha ya kitarii, wapenzi wengi wanavutiwa kuishi maisha hayo kuliko Yale yakupelekana sehemu nzuri zaidi. Wapenzi hukumbuka zaidi matendo waliyotendeana kipindi walipokuwa kwenye mazingira asilia kama vile kufanya mapenzi shambani, porini, uchochoroni, kwenye maficho mbalimbali.
NB: Kupanga ni kuchagua, wewe unafurahia mahusiano ya aina gani?
 
Back
Top Bottom