Sababu zinazosababisha watu wasifanikiwe

Sababu zinazosababisha watu wasifanikiwe

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
745
Reaction score
1,504
Dr.Joshua Grubb
(PhD) mtaalamu wa saikolojia alifanya utafiti katika chuo kikuu cha Western Reserve kutaka kujua sababu mojawapo inayochangia watu wasifisafinikiwe kutimiza Malengo waliyojiwekea.

Moja ya sababu kubwa aliyoigundua ni hali ya kuwa “disappointed “.
Hii inatokea pale ambapo matarajio ya mtu yanapishana na uhalisia wa jambo Kwa mujibu wa utafiti huu ilionyesha kuwa “millennials” (Kizazi cha sasa) kinapata changamoto kubwa sana katika eneo hili kwa sababu ya matarajio Makubwa ya kutaka kuishi katika mazingira yaliyokamilika katika Kila Kitu.

“Dissapointment” hutokea pale ambapo unafanya biashara ukitarajia upate faida mara mbili Halafu unapata hasara na mtaji unapoteza, unatarajia mahusiano uliyoanza yatakuwa na furaha sana lakini yanageuka kuwa mateso, unatarajia kwa 100% kupata kazi uliyoomba badala yake unaikosa, unatarajia Kipaji chako kitaonekana kwa juhudi unayofanya lakini hakuna anayeona n.k

Njia Mbili za kuishinda hali hii ni moja kila wakati unapokuwa “disappointed” Kumbuka iko Njia nyingine ya kufanikiwa,usikate tamaa kwa sababu ulichotarajia hakijatokea. Mbili, usimchukie na kuendelea kumjadili “aliyekudisapoint” UKifanya hivyo utaendelea kudumaa hapo ulipo na akili yako haitapiga hatua kwenda mbele.

Leo kuna WATU na MAZINGIRA yatakudisapoint pia. Wakati Mwingine mambo hayo yatatokea asubuhi mapema kabisa-USIKUBALI SIKU YAKO IHARIBIKE, Take Control.

#Nanauka
 
Solution dont put too much expectations to thing which you can not control or manage...i.e expecting high sales, expecting a good relationship just go with the flow
Thanks for your advice
 
Kabla hujafanya biashara ya mamilioni unatakiwa uanze biashara ya laki. Biashara ni kama maisha huanza mdogo na kuwa mkubwa, leo mtu kaambiwa ukiwa na mtaji wa milioni 10 basi umetoka kimaisha. Wakati huyu hata biashara ya laki 1 hajawahi kufanya, kuhusu relationship ukimpata mbuzi kwenye kioo cha Facebook. Kuna wenzio wengi wamemuona wewe mmoja kati yao tu, usiwekeze pasipo wekezeka. Ukiona mwanamke/mwanaume anaomba hela kwako kila wakati hakupendi wewe anapenda hela yako tu.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Tatizo la watu wengi ni vile kudhani kwamba they are soo much special for life to care for them, consider them worthy, etc
Kujiona wewe ni wa thamani sana na unastahili kila jema na zuri ni ni gateway to disappointments.
Consider urself just as normal as others only backed by luck. This will help you go thru disappointment and see the second chance.

Uzi mzuri
 
Don't touch what you cannot have and don't grab what you cannot take...

Think big, keep your mind positive always...



Cc: mahondaw
 
Tatizo la watu wengi ni vile kudhani kwamba they are soo much special for life to care for them, consider them worthy, etc
Kujiona wewe ni wa thamani sana na unastahili kila jema na zuri ni ni gateway to disappointments.
Consider urself just as normal as others only backed by luck. This will help you go thru disappointment and see the second chance.

Uzi mzuri
Ofcourse ni challenge haswa kwa vijana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom