Sababu za serikali kubadili sifa za kada za afya

Sababu za serikali kubadili sifa za kada za afya

Nipe tofauti yake mkuu

FTC anasoma miaka miwili na Ordinary Diploma anasoma miaka mitatu.
1df26a765593e1260194faa95658be69.jpg
 
Mkuu labda wamefanya hivyo katika kuboresha mfumo wa elimu
 
Kwa wale ambao mmepitia tovuti ya nacte mtakuwa mmeona kuwa kwa mwaka huu wa masomo 2017/2018 sifa za kujiunga zimebadilika sana hasa kwa ngazi ya cheti ukitokea kidato cha nne.
nimebahatika kuongea na mdau mmoja ambae anatengeneza mitaala ya afya akiwa mkuu wa chuo fulani na ameniambiakuwa:
Serikali imeadili sifa ambazo kwa zamani zilikuwa ni sifa za Stashada(Diploma) na kuwa za certificate. Kimsingi ni kuwa SIFA HAZIJABADILIKA. Wanafunzi wamepewa uwanja mpana wa kuamua kuendelea na Diploma au kuishia na certificate pindi watakapokamilisha miaka miwili.
Tuelewane hapa: Mwanafunzi akimaliza miaka miwili ya certificate ataamua AMALIZIE MWAKA MMOJA ILI AWE DIPLOMA HOLDER AU AISHIE HIYO MIWILI AWE CERTIFICATE HOLDER na akitaka diploma atakuja kumalizia mwaka mmoja aliouacha njiani kwa sababu sifa anazo.
KUHUSU VYUO VISIVYO NA SIFA ZA KUTOA DIPLOMA. Chuo kisicho na uwezo wa kutoa Diploma kitalazimika kuhamisha wanafunzi watakaotaka kuendelea na Diploma kwenda kwenye chuo chenye uwezo na mafunzo hayo. Kwahiyo chuo kinachotoa certificate mfn: uuguzi kitachukua wanafunzi kama kawaida kwa sifa za sasa lakini kitaishia kutoa level ya certificate(miaka 2) LAKINI kwa wanafunzi watakao taka kuendelea itawalazimu kuwahamishia chuo cha diploma ili wakamalizie mwaka wao mmoja uliobaki.
KUHUSU WANAFUNZI WALIOPO VYUONI: hao wanaendelea na masomo kama kawaida (Miaka miwili na hawana sifa za kuendelea na diploma lada kwa mfumo wa sasa(in service) wa miaka miwili mpaka watakapoisha sokoni ndipo mfumo huu utakuwa umejifuta rasmi

Nitarudi baadae kujibu maswali kama yatakuwepo
Sijaelewa hapo kwa wanafunzi walioko vyuoni, ina maana kama wakimaliza Technician certificate (2) wanaweza kuunganisha na Ordinary Diploma (1 year) ilihali vigezo vya sasa vimebadilika? Je kuna umuhimu gan wa cheti chake cha O level kumzuia huyu mtu asiunganishe mara amalizapo certificate ilihali amemaliza NTA 5 na cheti chake chenye GPA nzuri tuu??
 
Hali ilivyo ni tete kwa vyuo vya uuguzi ngazi ya cheti visivyo vya Serikali. Hadi sasa tukiwa tunakaribia muda wa kufunga dirisha LA maombi, hawajapata waombaji kwenye sifa mpya zilizotangazwa za CCDD, je, huoni kama kuweka sifa za kufanana kwa diploma na na cheti ni mkakati wa makusudi wa Serikali kupitia Wizara ya afya/TNMC wa kufungua vyuo hivyo hivyo kuanzia kuathiri PPP ? Kwa nini upande wa uganga sifa za kujiunga clinical assistant na clinical officer ziwe tofauti huku uuguzi diploma na cheti zifanane? Nisaidieni jamani sijaelewa
 
We want best health practitioners.. Tena natamani uwepo mtihani kwa kozi zote za afya kabla mtu hajawa licensed

Private institutions zimeharibu sana mfumo kwa kutengeneza watu incompetent
 
Hali ilivyo ni tete kwa vyuo vya uuguzi ngazi ya cheti visivyo vya Serikali. Hadi sasa tukiwa tunakaribia muda wa kufunga dirisha LA maombi, hawajapata waombaji kwenye sifa mpya zilizotangazwa za CCDD, je, huoni kama kuweka sifa za kufanana kwa diploma na na cheti ni mkakati wa makusudi wa Serikali kupitia Wizara ya afya/TNMC wa kufungua vyuo hivyo hivyo kuanzia kuathiri PPP ? Kwa nini upande wa uganga sifa za kujiunga clinical assistant na clinical officer ziwe tofauti huku uuguzi diploma na cheti zifanane? Nisaidieni jamani sijaelewa
Kazi ipo mwaka, mwaka huu p. college vitakuwa empty
 
wadau naomba msaada mimi nilimaliza form four mwaka jana (2016) nikapangiwa kwenda kusoma HGK halafu mimi nilikua sipendi kabisa hii michepuo ya sanaa. sasa nimeomba kwenda chuo kozi ya afya. je nitachaguliwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom