Sababu za NDOA yangu kufikia TAMATI

Sababu za NDOA yangu kufikia TAMATI

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
Tumeoana miaka 10 iliyopita wote tukikutana UDSM tukiwa active members of Christian fellowship. Tulihakikisha hatufanyi makosa ya kuwa na ndoa isiyodumu na hivyo tukawa tunasoma vitabu vingi vinavyohusu ndoa na haswa vile vya kidini. Tulikutana mara ya kwanza kimwili siku ya harusi yetu" HONEY MOON" na tumeishi vema kwa upendo hadi baada ya kupata mtoto wetu wa pili. Hali ilianza taratibu kwa wife kubadika tabia haswa akawa mvivu wa kitandani. Tuliweza kuwa na migogoro mingi iliyo fanya tumshirikishe msimamizi wa ndoa almost three times na wazazi bila mafanikio.

Tuliendelea kukwaruzana katika hilo eneo ingawaje si kwa kiwango kikubwa sana kwani kwa kiasi uwajibikaji wa mke ktk six by six haukuwa mbaya.

Ten years later wife akapata ujauzito na kumzaa our last born. Kipindi cha ujauzito kilikuwa kigumu sana kwa baba lakini akavumilia kwa sababu najua matatizo ya ujauzito ingwaje pia wife alijituma kwa kiasi kikubwa. Mwaka mmoja baada ya mtoto kuzaliwa hali imekuwa mbaya mno mno kiasi cha kufanya sex kufanyika very rarely.
Visingizio vya wife kusema amechoka anakesha akinyonyesha vikawa ndivyo visingiziyo vipya na sex ikawa adimu mno. Hii ikasababisha kuwepo mgawanyiko wa ndani kwa ndani kati yangu na wife kwani kitu kilichokuwa kinawaleta pamoja hakikuwapo tena. Majibu kati ya wife na mume yakawa dry dry huku baba akiwa na kinyongo na kuona wife anamfanyia maksudi. Wife akaipuuza ile hali ya mume kuwa katika hali ya huzuni na kukosa raha kana kwamba kila kitu kiko sawa sawa . Ghafla siku moja kifua kilipokuwa hakiwezi tena kustahimili na hali ikiwa haina dalili la kutenga maa mume akamfukuza wife kwani haoni kwa nini aendelee kuwepo. Mume anaanza Mchakato wa kuoa akiwa ameamua kubaki na watoto wake 3 na tangu wife apekekwe kwao hajawahi piga simu wala kuahidi kubadilika. Mume anadaia kuwa mkewe HANA UHUSIANO NA MWANAUME MWINGINE bali kiburi , uvivu na dharau.

Je sababu alizotaja huyu men zinatosha kusambaratisha ndoa? Naomba mchangie.

KISA HIKI NI CHA KWELI KABISA SI HADITHI YA KUTUNGA NA KIMETOKEA HAPA TZ
 
Uwezekano ni mkubwa wa huyo mke kuwa amevamiwa na mapepo ya mahaba,anahitaji
msaada wa kiroho zaidi kuliko nguvu na hekima nyingi,kwani hapo alipo yawezekana kabisa
haoni kama ana tatizo kwa sababu si matakwa yake ila analazimishwa kuwa hivyo na hayo mapepo.
 
Uwezekano ni mkubwa wa huyo mke kuwa amevamiwa na mapepo ya mahaba,anahitaji
msaada wa kiroho zaidi kuliko nguvu na hekima nyingi,kwani hapo alipo yawezekana kabisa
haoni kama ana tatizo kwa sababu si matakwa yake ila analazimishwa kuwa hivyo na hayo mapepo.

Hiyo ni possibility mojawapo kwani kuna nyakati usiku anaota kunamwanaume amelala karibu yake.
 
:bolt:Hapa ngoja nitoke haraka kwanza sina uzoefu na haya makitu nisije nikatoa ushauri negative nikavunja ndoa takatifu aliyounganisha MUNGU na mwanadamu alishaambiwa asiitenganishe, wajuaji watakuja kushauri
 
hapo kaka ni nguvu za giza tu,na nafikiri inatokana na kushuka kiimani.mlipokuw ktk njia huku mkiwa mmetangaza vita na shetani naye alikuwa anawaangalia anawasubiria kwenye 18 zake akafanikiwa kupata upenyo,akatimiza kile alichoapiA kuwa lazima awakomeshe. iko wApi ile njia ya zamani?
 
hii biashara ya kufunga ndoa ukifikiri itadumu milele naona haiuzi.....si uishi na mwanamke/mme kwanza kama miaka saba ndio mfunge ndoa........ndoa bado sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
ZAIDI YA KUMLAUMU NA KUONA HAFANYI JITIHADA ZA KUONGEZA MARUFUNDI KITANDANI ulifanya nini kingine ukiwa mume?
-ulishawahi kufikiri kumsaidia kupunguza hayo majukumu?
-ulishawahi kumuonyesha kuwa unaelewa kuwa makujumu yameongezeka?
-ulishawahi kumuonyesha kuwa wewe ni yule yule na hujabadilika kutokana na majukumu yake?
-ulishawahi kumhamasiha kihisia au ulibaki kusubiri yeye tu akae mguu pande?

-
 
Kama wanaamini waliunganishwa na Mungu, basi wamrejelee Mungu
 
hapo kaka ni nguvu za giza tu,na nafikiri inatokana na kushuka kiimani.mlipokuw ktk njia huku mkiwa mmetangaza vita na shetani naye alikuwa anawaangalia anawasubiria kwenye 18 zake akafanikiwa kupata upenyo,akatimiza kile alichoapiA kuwa lazima awakomeshe. iko wApi ile njia ya zamani?

ponit nzuri sana mkuu ila avatar yako mmmmnh
 
aiseeee babayangu kwanza jiulize kwanini mwanamke akatae tendo la ndoa kunamawili pingine wewe mwanaume haumwamdai vya kutosha au unamwacha njia panda that wai anakataa mara kwa mara
 
aiseeee babayangu kwanza jiulize kwanini mwanamke akatae tendo la ndoa kunamawili pingine wewe mwanaume haumwamdai vya kutosha au unamwacha njia panda that wai anakataa mara kwa mara

this may be very true
 
Majanga in full swing.
Kuna mtu naona hapo hajakomaa kimakuzi na maadili.
Hilo janga halitaisha mpaka kutokee muafaka wa hawa wawili.
 
^^
Akimkimbia Atakutana na mwingine ambaye atakuwa na tatizo lenye jina tofauti na sura tofauti.
Muiteni Mungu Upya.
^^
 
zidisha maombi ili mkeo afunguliwe....inawezekana pepo limeingia katika ndoa yenu.........na pia mkumbushe mkeo mwanzo jinsi mlivyokuwa mnaishi na unamiss sana hivyo vitu.....
 
Nionavyo mimi ni kuwa wadau wengi sana wanataka kutoa majibu rahisi rahisi katika masuala magumu kama haya.Kwa maoni yangu, Ndoa nyingi ambazo zimetokana na msukumo wa mob psychology chuoni kama vile kuabudu pamoja, dansi au kufanya field pamoja, hazidumu kwakuwa hazijengwi katika msingi wa uhalisia wa maisha (realistic). Kwa uzoefu wangu, ndoa nyingi zinazohimili shida ni zile ambazo wanandoa walimaliza masomo yao na kwenda kufanya kazi kwa muda angalau wa mwaka mmoja wakaliona ombwe la kukosa mwenza na wakahitaji kujaza ombwe hilo.
Ndoa za namna hiyo hudumu zaidi kuliko zile ambazo msingi wake umejengwa kwa kutamaniana chuoni tu!
Mfano mzuri na wa rafiki yangu ambaye tulimaliza naye zamani kidogo hapo UD na tulikuwa tukiomba na kuabudu pamoja pale chapel ghorofani. Alitokea kupendana na dada mmoja na kila mtu akiamini kuwa ni chaguo la mwenzie toka kwa Mungu. Wakati ukAfika baada tu ya kumaliza chuo wakafunga ndoa na sherehe kubwa ikafanyika pale Tambaza sec hall! Ilikuwa ni sherehe ya kufana sana! Wote walipata kazi moja akiwa wakili wa serikali na mwingine akiwa afisa uhamiaji.
Nasikitika kusema kuwa siku baada ya siku MAMBO YAKAWA SIMPLY HAYAENDI! Mpka ikafikia dada anasema anafikiria upya wazo la kushika mimba na mumewe! Hatimaye ndoa ile ikavunjika kwa furaha sana kutoka kwa kila mmoja wakiwa hawajapata mtoto na kila mtu akawa huru! Kila mmoja ukimwuliza nini shida hajui ila anataka kuwa peke yake basi! So ndoa kwangu mimi ni zaidi ya tamaa ya mwili tu, UPENDO,UVUMILIVU,KUMJUA MWENZA zaidi yake na hasa kwa mwanaume kuwa sterling wa ndoa! Mwanaume anatakiwa sana kuilinda ndoa yake kwa kumpenda, kumvumilia na kumwongoza mwenzie. Tumaini la mke liko siku zote kwa mume so mume anatakiwa awe activator wa penzi kwa ku click icon ya kurefresh love and life in general!!!
 
hii biashara ya kufunga ndoa ukifikiri itadumu milele naona haiuzi.....si uishi na mwanamke/mme kwanza kama miaka saba ndio mfunge ndoa........ndoa bado sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
hakuna safari yoyote ya hapa duniani ambayo haina kupanda wala kushuka ....hata mkiishi miaka 30 ndipo mfunge ndoa ...tatizo kama hili linaweza kujitokeza.....muhimu ni kumwomba Mungu pale unapokutana na gumu lolote basi akusaidie kulishinda hilo jaribu....na kuvuka salama........mana kwake hakuna lishindikanalo...
 
Back
Top Bottom