Sababu za mgomo wa cbe dodoma.

Jan 13, 2011
37
10
Mengi yameongewa kuhusu mgomo uliotokea CBE Dodoma na mimi nimeona vema niwape picha halisi ya mgomo huo.
Mgomo ulianza Jumatatu ya tarehe 07/03/2011 na kumalizika Jumatano tarehe 09/03/2011. Siku ya j3 na j4 walioshiriki mgomo ni wanafunzi wa shahada tu, na siku ya j5 mgomo ukawa wa chuo kizima kwa kuhusisha wanafunzi wa ngazi zote (certificate hadi postgraduate).

Sababu za mgomo:

1. Utaratibu mbaya wa utungaji wa mitihani.
CBE ina kampas tatu (Dar, Mza na Dom) zinazojitegemea katika shughuli zake za kila siku. Utaratibu wa utungaji wa mitihani kwa mujibu wa prospectus ya chuo (ukrsa 85), kila kampas mwalimu aliyefundisha anatakiwa kutunga mtihani na kuuwasilisha kwa mkurugenzi wa mafunzo ili ifanyiwe external moderation na kurudishwa kwa kampas husika ili ufanywe na wanafunzi wa kampas hiyo.
Cha kushangaza huyu mkurugenzi wa mafunzo badala ya kusimamia taratibu za mitihani kufanyiwa moderation, yeye anateuwa watu wa kutunga mitihani mingine kutokana na mitihani iliyowasilishwa kwake kutoka hizi kampas tofauti na kutoa mtihani mmoja kwa kila somo, utakaofanywa na wanafunzi wa kampas zote tatu.
Hili hutuletea kero nyingi sana na ni kinyume na maelekezo yaliyopo kwenye prospectus ndo sababu ya kulipinga.

2. Ada kupanda katikati ya muda wa masomo
Ada ya chuo imepanda ghafla tukiwa katikati ya kipindi cha masomo. Hii imepelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kulipa ada kamili kwa wakati na hivyo kuzuiliwa kufanya mitihani. Hili sisi tuliona si sahihi na tukaamua kulipinga. Uongozi wa chuo haukutusikiliza hivyo tukaamua kugoma.

3. Kutoshirikishwa katika vikao vya maamuzi vya chuo.
Utaratibu ulioandikwa na unaotumika katika vyuo vingi; vikao vya maamuzi vya chuo hushirikisha viongozi wa serekali za wanafunzi lakini katika chuo chetu hili ni tofauti. Viongozi wa serekali hawashirikishwa katika vikao muhimu kama; Governing body, Body of Examinors, Students Affairs Committee, na Curiculum and Examinations Committee.
Hili tumelidai kwa muda mefu tukapuuzwa hivyo tukaamua kukomaa kwa njia ya kugoma.
4. Unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya waalimu
CBE kuna waalimu huwa wanajihisi wako juu ya sheria na wanaweza wakamfanyia mwanafunzi yeyote jambo loloti bila wao kuhojiwa. Kwa mfano wapo wanafunzi 86 kati ya 136 wa mwaka wa 2 waliofelishwa kwa makusudi somo la Principles of Economics, na mwaka huu mwalimu huyohuyo katika somo hilohilo amekataa kuwapa coursework wanafunzi wa mwaka wa 1 ambao nao walikuwa wanatakiwa wafanye mitihani hii. Hili lilituudhi sana na ikawa sababu tosha ya kugoma ili wizara ichukue hatua juu ya huyu mtumishi wake.
Pia huyu mwalimu ambaye ni mkuu wa idara amekataa kuwasajili baadhi ya wanafunzi wa stashahada ambao walikuwa wanaingia mwaka wa pili. Hii imewaghalimu wanafunzi hawa kurudi makwao hadi mwakani ndiyo wajisajili kuingia mwaka wao wa 2. Hii inakera sana, inauma sana na inaudhi sana.

...................... itaendelea
 
Back
Top Bottom