Sababu za kuto chagua upinzani 2010

Una maanisha chama mbadala kwenye uchaguzi?
what is your point, najaribu kuelewa lakini bado sijakupata/

Unashindwa kuelewa nini mkuu? Kwani vyama vyote vinaingia kwenye uchaguzi ili iweje? I fail to understand your confusion. Labda tuanze hivi. Wewe ukisikia the term "chama mbadala" unaelewa nini? Au maana ya mbadala ni nini?
 
Kuomba ridhaa ya kuongoza nchi ni kama kuomba kazi. To get the best employee you must scrutinize and look into a person's record.
I have commented on every point you gave (hivyo ndivyo ulivyotaka uliposema watu hawajibu hoja); I expected your response on every comment, not just on the conclusion, otherwise hutakuwa tofauti na hao uliosema hawajajibu hoja zako!
 
Yes kuna mfumo huo. Kulikuwa na mfumo unaopendelea chama tawala Kenya mpaka juzi kati tu ila wenzetu waliweza kuovercome. Kama tatizo lia julikana upinzani unafanya nini kupambana na hili? Kama Kenya waliweza sisi tushindwe nini? CCM ni tajiri maybe because muda mrefu wao walikua chama pekee, lakini ni sisi tuliotaka upinzani tukijua yote haya. Tuta lia lia mpaka lini? What are we doing about it?

Hivi unataka tufuate mfano wa Kenya? Afadhali hata ungesema Zambia na Malawi. Of all places Kenya?!! Have you lost your mind? Kwa hiyo unataka Wasukuma Wanyamwezi na Wahaya waseme sasa zamu yetu? Na kisha hapo tuchinjane (japo mpaka sasa hivi tunachinajana) Haya sawa wameiondoa KANU je kunatawalika huko Kenya?
 
I was no referring to Kenya's tribalism but the fact that hey were able o ake ou he establishment and say no o he status quo.
 
I have commented on every point you gave (hivyo ndivyo ulivyotaka uliposema watu hawajibu hoja); I expected your response on every comment, not just on the conclusion, otherwise hutakuwa tofauti na hao uliosema hawajajibu hoja zako!

Hoja zipi mkuu? Are you joking? You said "Tusihukumu upinzani mpaka uipe nafasi" then I replied o you tha kuomba ridhaaya kuongoza ni kama kuomba kazi sasa hoja ipi nyingine unaaka ujibiwe? I replied according to wha I quoed...go & look back.
 
Nani, CHADEMA ??? Hawana chochote, chama cha mtu na mkwewe !!!! Au mnataka tuibue walivyo mkolimba Chacha Wangwe kwa kuwa alikuwa anakwenda Dar kutoboa siri zao za ufisadi. Achana na hawa Mafia. Mtajuta baada ya miezi saba tu. Amini ninayowaambia. Mkitaka zaidi nipo kilingeni.
 
Kuna sababu nyingi naona ni heri serikali ya chama cha mapinduzi kuliko serikali ya chama chochote cha upinzani tulionao. Hii ni kwa sababu hata kama CCM kime tupa baadhi ya sababu ya kuto kichagua bado naamini upinzani haujatupa sababu ya kuwa chagua na hilo ndilo la muhimu kuliko yote.

1.Upinzani mara nyingi umebaki kusema nini CCM haijafanya badala ya kukazania kutuambia nini wao wata fanya tofauti. Ni vigumu sana kuwa sikia wapinzani pale kunapo kuwa hamna maneno dhidi ya upinzani. Upinzani wetu upo REACTIVE badala ya kuwa PROACTIVE!

2.Vyama vyetu vya upinzani ni vyama vya uchaguzi tu. Ni vyama vichache na mara chache sana vinavyo jinadi kabla ya uchaguzi.

3.Wengi wa wapinzani walio kuwaga CCM na serikalini hawana track record nzuri na wengi wao inaelekea siyo wapinzani wa kweli bali wali hama kambi baada ya kuona hawana masilahi CCM.

4.Japo vyama vya upinzani havipo madarakni lakini bado kuna baadhi ya vitu wangeweza kufanya kusukuma gurudumu la maendeleo nchini. Sija sikia chama chochote cha upinzani kikiwa na program zozote za kijamii. Sijawahi(I could be wrong) kusikia chama chochote cha upinzani kikichangia aidha hali au mali wakati maafa yanapo tokea. Kumbuka kutoa ni moyo si utajiri.

5.Hata upinzani kuna baadhi ya watu ni mafisadi. Tumesikia wengine ambao wame pata utajiri wao kwa biashara zisizo halali au hata kuiba fedha za vyama vyao. Je hawa wakipewa serikali hawata endeleza ufisadi huo huo tena katika njia kubwa zaidi?

Baada ya kutafakari kwa muda mimi naona bado CCM ni chama "bora" kuliko chochote cha upinzani. Naamini kabisa kwamba bila baadhi ya watu wanao ichafua CCM bado kingekua chama imara. Nadhani baada ya enzi za Nyerere kuisha kule kupokezana kwa madaraka kulienda kwa kundi bovu badala ya kundi imara na kundi hilo ndiyo lime set precedent ya mambo yote yanayo tokea sasa. Bado sijaona upinzani wa kweli Tanzania. Ni mtazamo wangu tu.

Hapa hakuna jipya Mwanafals ni kibaraka cha mafisadi tumekushutukia sababu zako hazina msingi wowote
 
Hapa hakuna jipya Mwanafals ni kibaraka cha mafisadi tumekushutukia sababu zako hazina msingi wowote

Call me whatever you want. Sijaona hoja yako. Sababu zangu zina msingi sana kwa mtu mwenye upeo. Jibu hoja kwa hoja. BTW sawa mimi ni kibaraka cha mafisadi....do something about it.
 
Nani, CHADEMA ??? Hawana chochote, chama cha mtu na mkwewe !!!! Au mnataka tuibue walivyo mkolimba Chacha Wangwe kwa kuwa alikuwa anakwenda Dar kutoboa siri zao za ufisadi. Achana na hawa Mafia. Mtajuta baada ya miezi saba tu. Amini ninayowaambia. Mkitaka zaidi nipo kilingeni.

We tupe zaidi tu mkuu kama una valid and provable reasos. Maaaa siku hizi mtu usipo kuwa upande wa upinzani tu unaitwa "kibaraka wa mafisadi". We dare talk openly. If you can prove your words nena tu mkuu.
 
Siangalii shilingi kwa upande mmoja bali natoa hoja ya upande mmoja na mwenzangu kama wewe akitoa upande mwingine wote hunufaika na kuelimika.

Sawa kaka nakubalina na wewe
Sikusema maneno yangu ni sheria ndiyo maana nikasema ni maoni yangu. Kuhusu BOT,EPA, RADAR my friend hizo zime fumuliwa zote na chama kimoja i.e. Chadema na nyingi ni za mtu mmoja aitwae Dr. Slaa. Sijaona much evdence kwamba hizo kashafa zilikua juhudi za chama bado naona ni juhudi za mtu mmoja. Mtu mmoja bado hanipi sababu za kukichagua chama kizima.
Chama ni watu. Jaribu fikiria perfomance ya Dr slaa kama angekuwa CCM.Jiulize Sitta Angekuwa spika kutokana na upinzani ingekuwaje.Kuna wabunge wengi wako CCM lakini chama kinakwaza Perfomence yao.

Kwa msingi huu ndio naona kuliko kuchagua the so called mbunge mzuri wa CCM bora NiChague Mbunge Mbovu wa upinzani. inawezekana sijui kujieleza lakini mbona mi naona formula ni simple. Huuoni kuwa Perfomance ya mbunge akiwa CCM Inakuwa neutralised.

Ok.....CCM ni reactive kwa nani? Maana mimi nimesema upinzani ni reactive to CCM je CCM ni reactive to who? Huja explain bado.

CCM ni Reactive kwa upinzani hizi kashafa tunazoongelea zimeudiwa tume lini? CCM ni reactive kwa events ambazo zingekuwa managed vizuri proactively . Mfano Tatizo la mgawo wa umeme limekuwepo toka lini?

Yes kuna mfumo huo. Kulikuwa na mfumo unaopendelea chama tawala Kenya mpaka juzi kati tu ila wenzetu waliweza kuovercome. Kama tatizo lia julikana upinzani unafanya nini kupambana na hili? Kama Kenya waliweza sisi tushindwe nini? CCM ni tajiri maybe because muda mrefu wao walikua chama pekee, lakini ni sisi tuliotaka upinzani tukijua yote haya. Tuta lia lia mpaka lini? What are we doing about it?

Tuna machache ya kujifunza kwenye mfumo wa kenya. Ni kuwa vyama vinahitaji kushirikiana..Lakini sioni kama sucesss ya opposition ya kenya imejengeka katika misingi ya demokrasia. Ni Kisasi, Ukabila.

Kulia lia tutalia sana. Wenye machozi machache tunaona wanshika silaha but thanks God watanzania hatuko hivyo.Kuhusu waht are we doing ndio kama hivi mimi na wewe tunapeana. Changamoto iliyopo ni hoja kama hizi kuwafikia na kuwahusisha wanachi wengi zaidi. mashuleni, vijijini na mjini.

Mkuu mwizi ni mwizi tu. Ina maana una endorse "mwizi" ampokee "mwizi" mwingine? Na mwizi huiba kutokana na kilichopo karibu yake. Uta nihakikishiaje mpinzani mwizi akiingia given the chance nae hata iba kama wezi wa CCM wa sasa? Na je mimi niamini vipi mtu ambae ana weza kuiba kidogo hata iba kingi akipata nafasi?

Lakini kuna tofauti ya mwizi na jambazi. Kuna tofauti ya mwizi aliyeshakuwa na network kubwa ya kitaifa na kimataifa na uzoefu wa kuiba na yule ambaye hana mtandao wala hujampa ridhaa ukaona anaiba. Kuna tofauti ya mwizi anayeiba mchana kweupe. Wizi ni wizi lakini so far naona kwa hawa wenzetu ndio Chukua Chako Mapema. N ukweli CCM itakuwa nzuri zaidi ikikaa pembeni japo kwa miaka mitano tu hen ikarudi.wamelewa madaraka

Sijasema ni chama bora bali ndiyo chama nafuu kati ya tulivyo navyo. Na kama Chadema ikishindwa kumuadhibu mtu hicho ndicho unadhani kinafaa kuongoza serikali? Ukubwa wa umri si sababu. Kumbuka utu uzima siyo umri bali upeo na busara.

comparison yako sio ya haki. unafuu CCM unakujaje wakati hatujawai kuona bunge au serikali ya upinzani? Unafuu unakujaje wakati 90% ya wabunge ni CCM yet tunaona ........

na kama unataka kuona unafuu zaidi wa CCM basi tulifanye bunge letu liwe na atleast 40-50% ya upinzani.hapo nadhani ndo wote tutaipenda CCM.

Busara nayoona CCM wanayo ni kutatua matatizo. yao kichama zaidi,hata yale yenye maslahi ya taifa.CCM ina miaka 40 yet bado inatikiswa na watu wachache. kwa nn CUF yenye umri mchache isitikiswe na mtu. Suala na umri halikwepeki lazima tuweke vigezo vingi iliji tujue huu unafuu unaosemwa uko wapi

Mbunge mbovu ni mbunge mbovu haijalishi anatoka CCM au upinzani. Mbunge mbovu haongezi value yoyote wala efficiency bali nae ni strain katika economy kama mbnge mbovu wa CCM.

Hili nimelishalijibu Kimahesabu jaribu kujiuliza
If dr Slaa= CCM
If Sitta wa = Speaker from Opposition
IF Richard Ndasa= Opposition
If prof Mwandosya = oppostion.

Jibu ni simple no mmater how Good CCM MP is ile kuwa CCM ina mneutralise.

Nashukuru mkuu kwa maoni yako na walau wewe ume jaribu kutoa hoja kliko wengine walio kuwa wakipinga tu bila msingi wowote. Natumai huu mbadilishano wa mawazo utaendelea.

Changamoto tuliyonayo nikuwahsirikisha watu wa aina zote wasiokuwa na acess ya jamii forum amabao ni wengi. I wish ninegkuwa nina uwezo wa kuchapisha thread bora na kusisambaza kwa kina mama vijana ,wanafunzi wa jimboni au mtaani kwetu wajue watu tuanajdli nini na wao waelewe. na wao wajadili wafanye maamuzi wakiwa na taarifa sahihi za kila upnade bila ushabiki wa chama

NB
Wananchi wengi hawajui uziri na ubaya wa upizani na wala hawajui uzuri na ubaya wa CCM. Ndio maana CCM inapata ushindi.
 
Hoja zipi mkuu? Are you joking? You said "Tusihukumu upinzani mpaka uipe nafasi" then I replied o you tha kuomba ridhaaya kuongoza ni kama kuomba kazi sasa hoja ipi nyingine unaaka ujibiwe? I replied according to wha I quoed...go & look back.

Fine, you replied according to what you quoted, but you deliberately decided to quote only the last sentence! Kwa kuwa unauliza "hoja zipi mkuu" nazirudia hapa kwa manufaa yako, kwa kuwa unajifanya hukuziona:
Hoja zako nimeziacha in black na zangu nimeziweka in pink
Kuna sababu nyingi naona ni heri serikali ya chama cha mapinduzi kuliko serikali ya chama chochote cha upinzani tulionao. Hii ni kwa sababu hata kama CCM kime tupa baadhi ya sababu ya kuto kichagua bado naamini upinzani haujatupa sababu ya kuwa chagua na hilo ndilo la muhimu kuliko yote.

1.Upinzani mara nyingi umebaki kusema nini CCM haijafanya badala ya kukazania kutuambia nini wao wata fanya tofauti. Ni vigumu sana kuwa sikia wapinzani pale kunapo kuwa hamna maneno dhidi ya upinzani. Upinzani wetu upo REACTIVE badala ya kuwa PROACTIVE!
Upinzani unaposema CCM hawajafanya kitu fulani ambacho walipaswa kukifanya, maana yake wao wangekuwa madarakani wangekifanya. Ukumbuke kuwa wanapokemea maovu kama ya ufisadi maana yake ni kuwa wao wakiingia madarakani watakemea ufisadi na kuwachukulia hatua mafisadi. Hili wamelizungumza mara nyingi. Yawezekana hukuhudhuria mikutano ya operesheni sangara!

2.Vyama vyetu vya upinzani ni vyama vya uchaguzi tu. Ni vyama vichache na mara chache sana vinavyo jinadi kabla ya uchaguzi.
Kumbuka kuwa mara tu baada ya uchaguzi, kinachofuatia ni utekelezaji wa sera na ilani ya chama kilichoshinda. Haiwezekani na itakuwa siyo busara chama kikaanza kupinga immediately baada ya uchaguzi. Mshindi anapewa muda wa kutekeleza aliyoahidi na baada ya muda fulani akionekana kuyumba ndipo kukosolewa kunaanza kujitokeza; inapokaribia mwisho wa miaka 5 ndipo anapopimwa kama ametekeleza au vipi na hapo ndipo upinzani unapojitokeza wazi, kuonyesha namna aliye madarakani alivyovurunda

3.Wengi wa wapinzani walio kuwaga CCM na serikalini hawana track record nzuri na wengi wao inaelekea siyo wapinzani wa kweli bali wali hama kambi baada ya kuona hawana masilahi CCM.
Hii ni 50, 50 maana hatujui maslahi waliyokosa CCM ni yapi - inawezekana maslahi waliyoyataka ni ya kuwanufaisha wananchi na hivyo walipoyakosa wakaona bora watoke! Kwamba hawana track nzuri - inabidi ujustify. Kama track ya Mrema si nzuri - kwa vipi? Kwamba track ya Mbowe si nzuri - kwa vipi? nk. Tupatie specific instances ili tujadili vizuri.

4.Japo vyama vya upinzani havipo madarakni lakini bado kuna baadhi ya vitu wangeweza kufanya kusukuma gurudumu la maendeleo nchini. Sija sikia chama chochote cha upinzani kikiwa na program zozote za kijamii. Sijawahi(I could be wrong) kusikia chama chochote cha upinzani kikichangia aidha hali au mali wakati maafa yanapo tokea. Kumbuka kutoa ni moyo si utajiri.
Kwamba wewe hujasikia haina maana hawachangii (you're wrong). Je maafa ya Mbagala CUF hawakuchagia. Sema wanachochangia ni kidogo lakini pia ndiyo mapato ya vyama vyao yalivyo. Kwanza mimi nafikiri proportionately CCM ni kama haichangii maafa ukilinganisha na mapato yake -ruzuku, majengo tuliyoyajenga wote, viwanja tulivyojenga sote tena kwa michango ya kulazimishwa kwa hata asiye mwanachama nk.
5.Hata upinzani kuna baadhi ya watu ni mafisadi. Tumesikia wengine ambao wame pata utajiri wao kwa biashara zisizo halali au hata kuiba fedha za vyama vyao. Je hawa wakipewa serikali hawata endeleza ufisadi huo huo tena katika njia kubwa zaidi?
Hapa unaonyesha uzembe wa serikali iliyo madarakani! Na hizi ndizo kelele za wananchi. Kwa nini fisadi asichuliwe hatua? kama mtu kaiba fedha hata zikiwa za chama chake si sheria iko wazi? kwa nini aachwe tu? Kama mtu ana biashara isiyo halali, kwa nini aachwe tu? Haijalishi yuko upinzani au yuko CCM au yupo serikalini achukuliwe hatua stahiki. Tunailaumu serikali kwa kundekeza kulindana. Hata ambao wamepelekwa mahakamani, ushahidi unapelekwa dhaifu kiasi kwamba lazima waachiwe tu. Angalia suala la Rada; Uingereza inafikia mahali pa kuilazimisha kampuni yake kuilipa Tanzania lakini sisi wahusika akina Chenge wanapeta tu - ati mhusika mkuu hajakamatwa! Hii ni aibu kwani kama hajakamatwa hawa wengine si wawekwe ndani? Mahakama na sheria si zina kipengele cha kuhukumu in absentia yaani bila kuwepo mahakamani?
Eti "Je hawa wakipewa serikali hawata endeleza ufisadi huo huo tena katika njia kubwa zaidi?" Unakiri kuwa CCM kuna mafisadi, ila unaona bora waendeleze ufisadi ule ule kuliko kuwapa wapinzani kwa hofu tu kuwa wataendeleza ufisadi kwa njia kubwa zaidi! Hii ni hoja dhaifu sana - hivi hii nchi ni ya CCM tu - tuwaache waendeleze ufisadi? mwingine yeyote si sawa? kwani hawa nao si watanzania? Kibaya zaidi tunawahukumu kabla hatujawapa madaraka!! Labda hatujui kwa nini tunafanya uchaguzi kila baada ya kipindi fulani. Unachagua huyu akivurunda unamtoa unaweka mwingine akivurunda unamtoa, unarudisha wa mwanzo labda atakuwa amejifunza kitu nk.

Baada ya kutafakari kwa muda mimi naona bado CCM ni chama "bora" kuliko chochote cha upinzani. Naamini kabisa kwamba bila baadhi ya watu wanao ichafua CCM bado kingekua chama imara. Nadhani baada ya enzi za Nyerere kuisha kule kupokezana kwa madaraka kulienda kwa kundi bovu badala ya kundi imara na kundi hilo ndiyo lime set precedent ya mambo yote yanayo tokea sasa. Bado sijaona upinzani wa kweli Tanzania. Ni mtazamo wangu tu.
CCM hakiwezi kuwa chama bora. Mwenyewe unakiri kuwa "Naamini kabisa kwamba bila baadhi ya watu wanao ichafua CCM bado kingekua chama imara" Chama kisicho imara kitakuwaje bora?
Unazidi kuonyesha ubovu wa CCM
: "...baada ya enzi za Nyerere kuisha kule kupokezana kwa madaraka kulienda kwa kundi bovu badala ya kundi imara na kundi hilo ndiyo lime set precedent ya mambo yote yanayo tokea sasa." Asante sana. Unakiri kuwa kupokezana madaraka kumeenda kwa kundi BOVU, bado unasema CCM ni bora? na kwamba kundi hilo bovu lime set precedent ya mambo yanayotokea hivi sasa (ingawaje hukuyataja, kwa mtiririko ni yote maovu yanayofichwa kukiwemo kulinda mafisadi). Halafu unaendelea kuitetea CCM? You're contradicting yourself!
My question to you is - how do we break that precedence.
Maoni yangu - tuchague upinzani ili CCM ikae nje ya madaraka ijifunze, hawa wakivurunda tunawatoa tunaweka wengine, wakivurunda tunawatoa tuna rudisha CCM nk. TUSING'ANG'NIE KITU AMBACHO TAYARI TUNAONA KINA MATATIZO.
Tusiuhukumu upinzani kabla hatujaupa madaraka!

Nadhani nimekufumbua si macho tu bali na akili/fikra pia
 
Na mimi naomba mheshimiwa, kuongeza yafuatayo:
1. Kama Upinzani unavyokosa umoja nje ya serikali hivi sasa ukiingia serikalini utakuwa pia hauna umoja kama vile tunavyoona huko Kenya na Zimbabwe;
2. Hawa ni watu wenye njaa kali na hivyo tutegemee ufisadi mkubwa zaidi kuliko uliwahi kutokea huko nyuma;
3. Baadhi ya viongozi wa upinzani wanaonesha picha za ngono kwenye migahawa au klabu zao na hivyo kuonesha ni wapi watakapowapeleka wasichana na wavulana wetu wakishika madaraka;
4. Karibu kila kiongozi wa upinzani ananunulika kwa bei fulani, hili linaonesha pia wakiwa viongozi wa umma bado wataendelea kununuliwa na hasa wale wenye pesa ndani na nje ya nchi;
5. Karibu viongozi wote wa upinzani hawajui kusoma, kutafakari na kuandika taarifa na hoja mbalimbali za msingi, kwa hiyo wakija madarakani tutakuwa na uongozi wa wajinga;
6. Viongozi wa upinzani isipokuwa kwa Ndesamburo kule Moshi, Kilimanjaro hakuna aliyewahi kuanzisha mradi binafsi au wa kikundi wa maana hapa nchini kwa hiyo wakiingia madarakani wachache sana watakuwa na akili ya ujasiriamali, uwekezaji na uendelezaji watu kutokana na rasilimali walizonazo;
7. Kama walivyo viongozi waliopo madarakani viongozi wa upinzani wanoona pia bughudha au usumbufu kukutana na watu wa hali ya chini na masikini kwa ujumla ili kusikiliza matatizo yao na hivyo hawajui shida na matamanio na matarajio ya wale wanaotaka kuwaongoza kama walivyo wenzao leo kwa hiyo hapa hapatakuwa na mabadiliko yoyote. Utatoka uongozi unaojali maslahi yake yenyewe kwanza, ukaingia uongozi ambao pia unajali maslahi yake kwanza na siyo yale ya wale waliowatuma;
8. Hakuna mwanasiasa wa upinzani hata mmoja, ukimuondoa Maalim Seif, ambaye anakubali kukaa kijijini kwao kwa mwezi mmoja au zaidi, wote wako mjini kwa hiyo wakija madarakani nao pia wataendeleza miji na sio vijiji;
9. Hakuna Chama Chochote cha Upinzani kilichokubali kufanya makao yake makuu kuwa Ddoma kikiwemo hicho kipya cha CCJ. Kwa hiyo kama yalivyo mambo mengi mengine vyama hivi ni vya wajanja wachache wa mjini Dar es salaam kutaka kuila nchi toka jiji la maraha;
10. Hakuna chama chochote isipokuwa CHADEMA kilichozungumzia kuipa mikoa haki na uhuru wa kujitawala yenyewe kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya haraka ya mikoa husika. Hii ina maana serikali ya upinzani nayo itataka na itakubali ukiritimba wa kuitawala nchi hata kama haipelekwi mbele kutokea Dar es Salaam.
Nimezungumza, wengine nao wazungumze- Mwalimu Jr.
 
Soma tovuti ya Chadema kwa kusudi la kujua maadhimio yao...

mwambie awe anatembelea tovuti za vyama mbalimbali kujua policies and strategies for a better Tanzania. sio tui anakuja na tusababu twake humu and then anasema watu wanachangia bila valid arguments, they dont need to kwa sababu kwenye tovuti kuna kila aina ya sera za kila chama; kaka if you wanna know what CHADEMA will do to the nation please abide to some of your routines on visiting chadema's website www.chadema.net, you is gonna get all infos kuhusiana na sera za chama pamoja na mengineyo, kama huduma kwa jamii patokeapo majanga n.k, vision ya chama na Tanzania as a whole.
 
usitegemee wapinzani wote watakuwa kama dr slaa au mtikila au Rashid Muhamad.Katika jimbo bora tuchague avarage opposition MP kuliko the so called Best perfoming CCM MP. kuwa CCM kunawa-neutralise hawa wanaoonekana kuwa ni wabunge bora kuliko wale waupinzani.

Kuongeza idadi ya wapinzani hata wanaolala bungeni ita add value kuelekea mabailiko ya kweli.

Kuanza kuwatafuta wapinzani kwa kuwalinganisha na Dr slaa, au M, Rashid sio sahihi.

Ndugu,hitimisho ya yote tunayojadili humu ni kuwa wapinzani hao wapate kura huko kwenye majimbo yao.

Hata tukijaza thread mpaka page 1000, mimi na wewe it is our desire ikiwezekana wabunge wote wawe upinzani! sala ni je wananchi wanakuwa convinced vipi kupiga kura?

Ushindi wa asilimia 80 wa JK haukuendana na urais tu, tulishuhudia pia wabunge wa CCM kufurika bungeni

swali ambalo mimi na wewe tujadili ni je: upinzani utawezaje kupata kura? utawezaje kuwashawishi wananchi?.Tukishindwa kujibu haya basi ni wazi tumeshindwa vita hii.

Na je project hii itachukua miaka mingapi? mwaka 1995 ndiyo mwaka pekee ambapo upinzani ulipata asilimia 40 ya kura, na tulidhania baada ya hapo, mwaka 2000 na 2005 asilimia zingeongezeka, lakini upinzani umeendelea kudorora kdiri miaka inayoendelea!

watu wameshapitia hizo tovuti kama wengine wanavyoshauri humu, na njia pekee ya kuonyesha upinzani uko accepted ni kupata kura!

I see no harm on these kind of threads if the intention is to make us aware how we can actually win people so that they can vote for opposition!

Kuna upole fulani uko upinzani ambao huo ndio unatuua, 'compromise', yes serikali', ukondoo fulani ambao kuubariki na kuita upinzani ni sawa na ku-endorse CCM waendelee kutawala milele!
 
Wewe huna cha kusema cha maana na pia nakuomba usome kazi ya vyama vya Upinzani ndio unaweza kujua kazi yake na pia tofautisha na programme ay vyama kama NGO's na miradi please nakuomba usome tena nini maana ya vyama ya upinzani, au ndio na wewe umekuwa kada siku hizi jamani???
 
Na mimi naomba mheshimiwa, kuongeza yafuatayo:
1. Kama Upinzani unavyokosa umoja nje ya serikali hivi sasa ukiingia serikalini utakuwa pia hauna umoja kama vile tunavyoona huko Kenya na Zimbabwe;
2. Hawa ni watu wenye njaa kali na hivyo tutegemee ufisadi mkubwa zaidi kuliko uliwahi kutokea huko nyuma;
3. Baadhi ya viongozi wa upinzani wanaonesha picha za ngono kwenye migahawa au klabu zao na hivyo kuonesha ni wapi watakapowapeleka wasichana na wavulana wetu wakishika madaraka;
4. Karibu kila kiongozi wa upinzani ananunulika kwa bei fulani, hili linaonesha pia wakiwa viongozi wa umma bado wataendelea kununuliwa na hasa wale wenye pesa ndani na nje ya nchi;
5. Karibu viongozi wote wa upinzani hawajui kusoma, kutafakari na kuandika taarifa na hoja mbalimbali za msingi, kwa hiyo wakija madarakani tutakuwa na uongozi wa wajinga;
6. Viongozi wa upinzani isipokuwa kwa Ndesamburo kule Moshi, Kilimanjaro hakuna aliyewahi kuanzisha mradi binafsi au wa kikundi wa maana hapa nchini kwa hiyo wakiingia madarakani wachache sana watakuwa na akili ya ujasiriamali, uwekezaji na uendelezaji watu kutokana na rasilimali walizonazo;
7. Kama walivyo viongozi waliopo madarakani viongozi wa upinzani wanoona pia bughudha au usumbufu kukutana na watu wa hali ya chini na masikini kwa ujumla ili kusikiliza matatizo yao na hivyo hawajui shida na matamanio na matarajio ya wale wanaotaka kuwaongoza kama walivyo wenzao leo kwa hiyo hapa hapatakuwa na mabadiliko yoyote. Utatoka uongozi unaojali maslahi yake yenyewe kwanza, ukaingia uongozi ambao pia unajali maslahi yake kwanza na siyo yale ya wale waliowatuma;
8. Hakuna mwanasiasa wa upinzani hata mmoja, ukimuondoa Maalim Seif, ambaye anakubali kukaa kijijini kwao kwa mwezi mmoja au zaidi, wote wako mjini kwa hiyo wakija madarakani nao pia wataendeleza miji na sio vijiji;
9. Hakuna Chama Chochote cha Upinzani kilichokubali kufanya makao yake makuu kuwa Ddoma kikiwemo hicho kipya cha CCJ. Kwa hiyo kama yalivyo mambo mengi mengine vyama hivi ni vya wajanja wachache wa mjini Dar es salaam kutaka kuila nchi toka jiji la maraha;
10. Hakuna chama chochote isipokuwa CHADEMA kilichozungumzia kuipa mikoa haki na uhuru wa kujitawala yenyewe kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya haraka ya mikoa husika. Hii ina maana serikali ya upinzani nayo itataka na itakubali ukiritimba wa kuitawala nchi hata kama haipelekwi mbele kutokea Dar es Salaam.
Nimezungumza, wengine nao wazungumze- Mwalimu Jr.

Forget other parties, I can testify, Cahdema wana watu potential kabisa kuweza kuongoza hili taifa, they can by anyway replace CCM, no matter how CCM looks like. They have good policies. Weakness ulizozisema zinaweza kusafishika.

Tatizo langu ni kuwa they are ot strong enough to shake CCM! wapole na compromisation nyingi! akina odinga, morgan walitakiwa wawepo chadema. Na ni dhambi kubwa kuwaza kuwa upinzani utatokea CCM!
 
Ushauri kwa wapenzi wa CCM- chagua upinzani ili CCM kifufuke, uozo uishe na kiwe bora

Ushauri kwa wapinzani - Unganisheni nguvu zenu kwenye ubunge, ni bora ukubali chama chako kikose wabunge ikiwa yuko mpinzani mwingine anayeweza kuwabwaga CCM.

Ushauri kwa Watanzania - Zanzibar, wapeni CUF nchi yao. CCM inajali zaidi maslahi ya bara. CUF ndiyo wanaZanzibar halisi. Ndio watakaoweza kuondoa kero za Muungano na siyo wapiga porojo wa CCM.

Ushauri kwa watanzania- Bara - CCJ mmeona wenyewe ni wanafiki, wana CCM walioanzisha CCJ wamejificha na kutanguliza watu wengine kabisa. Hii inafanana na EPA. Waliochukua mshiko wametanguliza watu tofauti, 'they made you to chase ghosts''

Ushauri kwa watanzania wote - Tuchague upinzani kwa nguvu zote, hapo ndipo serikali zetu zitakuwa na adabu. Tuchague chama kimoja cha upinzani chenye mwelekeo japo kidogo tu, tuwape support waing'oe CCM na ufisadi wake. Adabu lazima irudi nchi hii.

Mkishindwa hata hili basi......nitaichukua nchi mwenyewe kibabe.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom