John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 113
- 222
Sababu za Kumheshimu Mchungaji Wako
Mchungaji ni Nani
Wachungaji ni watu maalum walioteuliwa na kuchaguliwa na MUNGU kulichunga na kulilisha kundi lake kupitia mafundisho ya Neno la Mungu, maonyo na Maombi (Yohana 21:15-17). Na hawa wanafanya kazi mfano wa zile za kikuhani katika nyumba ya Mungu. Isipokuwa wenyewe hawawapatanishi watu kwa damu za wanyama, bali kwa damu ya BWANA YESU kupitia Neno Lake.
Uchungaji ni moja ya huduma ambayo Yesu Kristo aliitoa ndani ya Kanisa lake pamoja na huduma nyingine nne ambazo ni Mtume, Nabii, Mwinjilisti na Mwalimu, kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe (Waefeso 4:11-12). Hivyo, Mchungaji ni mtu aliyetolewa kama zawadi kwa kanisa ili makusudi afanye kazi ya kuwakamilisha watakatifu pamoja.
Mamlaka za kidunia
Kila mahali pana mamlaka yake, na mamlaka hizo huwa ni wajibu kwa walio chini yake kuzitii. Kwa mfano, katika familia, Mungu ameweka mamlaka, baba awe kichwa, na mama msaidizi wake, hivyo ni wajibu wa watoto kuwatii wazazi wao. Familia haiwezi kusimama kama mtoto atataka nafasi ya baba, kwamba yeye ndio atoe maamuzi ya mwisho, au ajiamulie la kufanya, awapangie wazazi wake majukumu ya ndani, hilo haliwezekani.
Vile vile, katika ngazi ya utawala wa kidunia, Mungu kaziweka mamlaka na anataka watu wote wazitii, kwa sababu hazijaamuriwa na mwanadamu, bali yeye Mungu mwenyewe.
Warumi 13:1-2: 1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu. 2 Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu; nao washindanao watajipatia hukumu.
Tito 3:1-2: 1 Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa kila kazi njema; 2 wasimtukane mtu ye yote, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote. Sasa hizi ni mamlaka za kidunia.
Je, Mungu hana mamlaka?
Mungu pia ameweka mamlaka yake duniani, ambayo ni kuu kupita hizo zote, na kupitia hiyo huwahudumia watu wake. Na anataka tuitii na kuitetemekea kwa sababu ni yeye mwenyewe atendaye kazi kupitia hiyo.
Mungu ameweka mamlaka hiyo kupitia nani?
Hii ni kupitia wachungaji wetu/waangalizi wetu, ndani ya kanisa. Ni vema kufahamu kuwa kiongozi ye yote wa kiroho (anayeisimamia kweli) hakujiteua mwenyewe kwenye nafasi hiyo. Mitume wa Yesu hawakujichagua wao, bali walichaguliwa na Mungu mwenyewe.
Mtu ye yote aliyepewa maono ya kuanza kanisa, na ukajikuta upo chini yake, au kateuliwa na Roho Mtakatifu mwenyewe ndani ya kanisa (Matendo 14:23), huyo ni wa kumtii sana. Kama vile unavyowatii watawala au mazazi wako kwenye familia, haijalishi atakuwa na mapungufu kiasi gani, au umri wake ni mdogo au mkubwa kiasi gani, awe mwenye uwezo au asiye na uwezo kiasi gani. Wewe unatakiwa kuwatii tu.
Kwa nini uwaheshimu Wachungaji
1. Wanajitaabisha kwa ajili yako kukuchunga, kukuonya na kukuombea
Hivyo wajibu ni wako kurudisha moyo wa upendo, na kuwasikiliza.
Tuzingatie maandiko:
1Wathesalonike 5:12-13: 12 “Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; 13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi”.
1Timotheo 5:17-22: 17 Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha. 18 Kwa maana andiko lasema, Usimfunge kinywa ng’ombe apurapo nafaka. Na tena, Mtenda kazi astahili ujira wake.
19 Usikubali mashitaka juu ya mzee, ila kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu.
20 Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.
21 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, na mbele za malaika wateule, uyatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.
22 Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.
2. Watasimama mbele ya kiti cha hukumu siku ya mwisho kutoa hesabu juu yako
Hivyo ni wajibu kuonyesha moyo wa kunyenyekea kwao.
Waebrania 13:17: "Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana
wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi".
Madhara ya Kutowasikiliza/Kutowatii Wachungaji
1. Watafanya kazi ya Mungu kwa kuugua
Katika kitabu cha Waebrania 13:17 anasema: "ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi". Na matokeo yake utendaji kazi ndani ya kanisani utakuwa hafifu. Ukishaanza kuonyesha tabia ya kutosikiliza unachoelekezwa, unapewa jukumu hutekelezi, hurudishi mrejesho, unafanya tofauti na wengine, yeye anataka uende kulia wewe unaenda kushoto, yeye anafundisha hiki wewe unafundisha kile. Fahamu kuwa jambo hilo litamhuzunisha kiongozi wako. Na hivyo kupelekea hamasa ya kuhudumu kupungua. Na madhara yake ni kuwa Mungu hukata utendaji kazi wake mahali hapo,
2. Utajisababishia adhabu kwa Mungu
Wakati ule Haruni na Miriamu dada yake, walimnenea Musa maneno mabaya kwa sababu ya mke wake ambaye hakuwa myahudi. Mungu aliwaadhibu kwa kumpiga ukoma Miriamu, kwa sababu tu hiyo ya kutoonyesha adabu kwa mtumishi wake.
Kitabu cha Hesabu 12:7-8 kinasema: 7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; 8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?
Ni kosa kumnenea vibaya mchungaji wako. Epuka masengenyo na uasi na matabaka ndani ya kanisa. Uonapo kosa muombee, au mfuate umweleze uwapo naye peke yake. Hilo litamjenga zaidi badala ya kutoa lawama na manung’uniko. Adui hutumia sana njia hii kuleta mafarakano na magomvi, na mapigo kanisani.
Kwa hiyo, mheshimu Mchungaji wako, zaidi ya Rais wa nchi, kwa sababu yeye ni balozi wa mbinguni, na Mungu atakuinua (1Petro 5:1-6).