Sababu za kulipuka mabomu haziridhishi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu za kulipuka mabomu haziridhishi...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jackbauer, Feb 18, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wakuu lazima ifike sehemu tuache porojo na tueleze mambo kisayansi.
  Tunaambiwa Milipuko iliyotokea mbagala na sasa gongo la mboto inasababishwa na uchakavu wa mabomu na pia joto kali.
  Naomba wakufunzi wa mambo ya milipuko watoe ufafanuzi juu ya haya;
  1.mabomu chakavu hupatikana tanzania pekee?
  2.je ni joto kiasi gani linahitajika kusababisha milipuko ya mabomu chakavu?
  3.wakati milipuko inatokea joto katika maeneo ya Mbagala au gongo la mboto lilikuwa kiasi gani?
  4.ni kwa nini hatusikii milipuko ya namna hii kwenye maeneo kama sudan au mali?haya ni maeneo ambayo huripotiwa kuwa na joto kali karibu kila siku(40+ degrees celcious).
  5.ni dalili gani hutokea kabla ya kutokea milipuko ya mabomu chakavu?
  6.ukweli ni upi?! Je bomu linapochakaa huongeza au hupunguza 'potency' yake?ina maana bomu chakavu lina uwezo mkubwa wa kulipuka kuliko bomu jipya?je hii ina maana wenye mabomu ya zamani kama sisi watanzania wana advantage katika vita?


  Wakuu wanaJf tujadili hili suala bila kuingiza siasa.tuongeze maswali ya kiutaalamu kwa wataalamu wetu wa kijeshi...  MUNGU UZILAZE ROHO ZA WAHANGA WA MILIPUKO YA MBAGALA NA GONGO LA MBOTO!!
   
 2. Mwanaitelejensi

  Mwanaitelejensi Senior Member

  #2
  Feb 18, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jeshi linaongozwa na washikaji wa Kikwete ambaye amechagua wasani wenzake sasa ndio tunaonyeshwa usanii wa hali ya juu. Ntamani kulia nchi ilivyotekwa na Mafisadi:mad:
   
 3. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu reasoning yako nimeipenda hasa hapo kwenye red!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Mhh bora wewe umesikia sababu ya joto na uchakavu!mimi nimemsikia eti sababu siku ile ilikua MAULID DAY!pia kawaida ilitakiwa wahusika wajiuzulu kupisha uchunguzi huru kufanyika,hajasema idadi ya mabomu,expiry date,baada ya mbagala hatua walizochukua kwa kambi zingine hata hivyo haya yakalipuka
   
 5. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #5
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kama sababu ni uchakavu wa mabomu - huu mimi naona ni uzembe, maana kama mabomu chakavu yanalipuka kirahisi si wangeyateketeza kabla hayajalipukia watu?
  hii sababu ya joto inaniacha kwenye mataa............. zile nchi za wenzetu zenye joto mpaka 40C wanatunazaje mabomu yao?
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  wenzetu Mgao wa umeme haupo kwenye kamusi zao/ ni dude lisilo fahamika hivyo basi wanaweza kudhibit joto kwa feni na AC
   
 7. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni kweli ndugu uko sahihi, miaka iliyopita nilienda japan, katika kuongea na mjapan mmoja aliniambia yeye toka zaliwe hajawahi kuona mgawo wa umeme na umeme kukatika, jamaa alikuwa na umri wa miaka zaidi ya 40
  Kwa hiyo wenzetu wako tofauti.
   
 8. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mtoa mada amesema tusiweke siasa katika hili lakini naona watu wengine wanaleta siasa na dini pia Kikwete ndiye aliyelipua mabomu? oh CDF ni mshkaji wa kikwete je angekuwa amemteua mtu ambaye si mwanajeshi kushika wadhifa huo tungesema nini sasa? Chief of Defence Forces hachaguliwi kama waziri anapaswa kuwa na vigezo stahiki na raisi lazima afuate taratibu zote zinazostahili akishauriwa na watu stahili. Ujue Ikitokea vita Mkuu wa majeshi ndiye anakuwa waziri wa ulinzi na ikitokea nchi iko matatani kisiasa yeye anakua ndiye rais ambapo jeshi limechukua hatamu. Hiyo ilika elimu ndogo kwa wale wanaoweka ushabiki wa kisiasa na dini.

  Napenda kutoa ushauri na angalizo katika kujadili hii mada nzuri kuwa tuwe makini sana ili kutoleta madhara kwa maadui wa nchi hii wakiwemo mafisadi na wahujumu uchumi.

  Mkuu wa usalama jeshini katika technical report yake hajazungumzia chanzo cha tatizo ila namna ilivyokuwa baada ya milipuko kuanza na kusema kuwa bado uchunguzi unafanyika kubaini chanzo. Hivyo kisayansi hapo sioni porojo wala majibu mepesi.

  Swala la kwamba kulikua na kukatika kwa umeme, mtu kafanya hujuma, wanajeshi wanahasira, mara mtu alitaka kuiba silaha haya yote ni mawazoyetu nikimaanisha porojo hakuna mwenye uhakika. Hata wataalamu wa mabomu wanaelezea vyanzo vya mabomu kulipuka lakini kwa ya gongo la mboto hakuna aliyeweza bainisha kuwa ni nini hasa kilichosababisha kulipuka kwa mabomu yale.

  Tofauti kati ya ajali ya mbagala na ya gongo la mboto kama nilivyomwelewa shimbo si ya kilichosababisha milipuko bali hali ilivyokuwa wakati tukio matukio yalivyotokea. Yale yalikua mchana haya ni uksiku, yale kulikua na shughuli za kijeshi zilikua zinaendelea (huenda walikua wanayapanga au wanapakua mzigo) lakini hii ya sasa kulikua hakuna shughuli yoyote iliyokua inaendelea.

  Kwa kumalizia ni kuwa mpaka sasa hatujaambiwa kilichosababisha mabomu kulipuka (explosive catalyst) mbagala na gongo la mboto . Naungana na Prof. Lipumba kuwa iundwe tume huru ya kuchunguza ajali hizo ila tu kuwe na mipaka maalumu au kuwe na uangalifu mkubwa kwa tume hiyo isijeingiliwa na maadui (hii ni kwa usalama wa nchi yetu).
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mkuu nimekugonge thanks!nasisitiza tuweke itikadi zetu za siasa au dini pembeni,tuulize maswali magumu halafu tuchallenge majibu marahisi.
   
 10. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Brg.Gen.Mndeme ametaja kitu kimoja cha kisayansi;amesema mabomu yanatakiwa yahifadhiwe kwa umakini lakini hapohapo yawe rahisi kulipuka pale yanapohitajika.therefore there is a very thin line of 'safety' as far as handling of explosives is concerned.
   
 11. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo ni usaniii tu utasikia sababu watakazo kuja nazo.... hapo taizo ni uzembe tu, hawa jamaa watoke wakafanye ushakaji huko kwao!!!
   
 12. E

  Ebony Guest

  #12
  Feb 18, 2011
  Joined:
  Messages: 0
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwanza kabisa wewe unadhihirisha kuwa ndiye mdini na mwanasiasa(umekosa uzalendo kabisa hadi ukamtaja Lipumba!) Unajua njia ya mwongo fupi sana! Hakuna mtu yeyote hapo juu alieingiza udini wala siasa katika hii hoja! Wote wameongea ukweli mtupu! Sasa kama umeguswa kwa kuwa Raisi na watu wake wa karibu ni wa dini fulani, au kwa hisia kwamba wanaopinga huu uzembe uliotokea juzi ni wanachama wa chama fulani, basi hayo ni MATATIZO YAKO BINAFSI! Watanzania we call a spade a spade! Unafiki hatutaki! Kama serikali inachemsha hatuwezi kuitetea eti kisa inaongozwa na mtu wa dini fulani! Huo utakuwa ni UJINGA NA UBINAFSI ULIOPINDUKIA.

  Nikirudi kwenye hoja tangulizi...ni kweli hayo maneno yametamkwa na maswali ya mtoa hoja ni ya msingi kabisa na yanafaa kujibiwa!

  Mwisho kabisa...NAPINGA KWA NGUVU ZOTE UUNDWAJI WOWOTE ULE WA TUME! Huko ni kupeana ulaji kusiko na manufaa kwa mtanzania. Hakuna haja ya tume! Wizara husika ikakague makazi ya watu walioathirika na walipwe fidia, kisha makambi yote yafanyiwe ukaguzi muafaka na kuamua either kuwatoa wananchi jirani nayo au kuhamisha makambi hapa mjini. Kwanza makambi na mji wapi na wapi bwana! Na kabla ya hayo yote kutake place, wahusika wa ngazi zote za kiusalama ambao kwa namna moja au nyingine wanaonekana walizembea kwa wazi baada ya tukio la Mbagala na kutochukua hatua yoyote basi WAWAJIBISHWE MARA MOJA. Hata kama ni wa ngazi ya juu kabisa ya Serikali.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  hivi tupo kwenye ulimwengu wa digital haya mabomu ya analog kwenye ulimwengu wa digital ya nn? hivi akuna antbom kuzui yasilipuke? kama tatizo ni joto kwann wasipeleke mikoani kama makambako, tukuyu nk? je akuna ukaguzi wa marakwamara kuangalia exp date na kuyategua bila madhara? je kama ni chakavu kwann wasiyaharibu na kununua mapya? kama ni umeme je ikulu kuna tatizo la umeme? je kwa umuhimu na hatari ya hayo mabomu na humuhimu wa ghala kuu la jeshi tanesko awakutakiwa kulipa kipaumbele kama wanavyotoa kipaumbele kulipa dowans?
   
 14. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  nikweli ni usanii mana watakaa sio kutafuta chanzo bali kutengeneza kauli yakujakutuambia ituingie akilini mana chanzo wanakijua ni uzembe ulikithiri na katu uwezi kuusema hadharani
   
 15. A

  Aaron JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,121
  Likes Received: 2,721
  Trophy Points: 280
  Yote tisa, kumi kwa nin maghara ya mabomu na silaa za moto yanawekwa karibu na makazi ya wananchi. Lazima serikali iwajibishwe kwa hili..!
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Br.Gen. Mndeme anasema kuna ukaguzi ambao ni 'routine'ambao hufanywa hapo ghalani,kwa upande mwingine anasema yeye alikua anaongoza ukaguzi ambao naweza kuita extraordinary siku 2 kabla ya tukio ingawa walikuwa hawajaandaa final report kabla ya mabomu kulipuka.
  Je ni kwanini walifanya ukaguzi usio wa kawaida kambini hapo?
  Ina maana waligundua uwezekano wa milipuko kutokea halafu wakakaa kimya bila kutoa tahadhari?kama hawakugundua dalili za kulipuka je hawaoni kwamba ni uzembe au kukosa ujuzi?
  Watanzania wanahitaji majibu ya maswali haya na mengine mengi ili tumtambue mtu wa kumuwajibisha.


  ONYO:wakati wa ubabaishaji umefikia ukingoni,wataalamu au wahusika lazima wawajibishwe kwa uzembe.sioni kwa nini tunaweza kuwawajibisha watumishi wa afya mfano mwananyamala na MOI huku tukiwaacha waliohusika na milipuko ya mbagala na G.mboto.
   
 17. t

  truth Member

  #17
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ??? uwiiiii! unalinganisha na sudan?, kumbuka sudan yanatumika kila yanaponunuliwa, kwetu yanachakaa kwa kuna hatuna vita za kijinga, tuwasaidie wanajeshi wetu mawazo ya kitaalam kama tunadhani kuna masuala tuna utalamu nayo ili watulindie taifa letu vyema. my friend keeping the high sprit of the military is to support them not blame them. sina uhakika kama unajua ugumu wa ujeshi! sijui umepita hata JKT mwenzangu?.
   
 18. t

  truth Member

  #18
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  labda wataalam mlioko kwenye cyberworld mtwambie wakati makambi hayo mawili yanajengwa how far were they from residence?, from strategic point of view .......???, unaweza kuwa smart katika polojo, lakini jiulize how many failures are their ktk mazingira yako ya kazi au biashara, unabahati kwamba you are not handling explosives you probably would have already killed us all!
   
 19. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  basi tuachane na sudan vipi kuhusu bamako Mali au vipi kuhusu ugiriki,russia ambapo kunakuwa na extremely high tempereture.huku utasikia joto linasababisha msitu kuungua na sio mabomu kulipuka.
  Sioni ubaya au aibu wakikubali hawana utaalamu na waombe msaada,isitoshe naamini nchi zote duniani zinapeana utaalamu na wataalamu wa mambo ya kivita.
  Kila taaluma(profession) ina ugumu wake sio jeshi tu.mkuu kama unadhani JKT yetu ya kipindi kile itatusaidia katika ulimwengu wa huu wa science na technology basi ujue umepotoka.
  Nitatoa support kwa jeshi letu sio kwa kuandika tu bali kuvaa magwanda wakati wa vita LAKINI siwezi kusupport uzembe uliotokea mbagala na G.mboto.I'M SERIOUS!!
   
 20. M

  Mboja Senior Member

  #20
  Feb 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mimi sioni mantik ya kuimba kila siku kwa huyu Kikwete eti wawajaibishe. Hivi wewe unaweza kumuwajabisha mshikaji wako. Mimi nina wasi wasi hata sisi wananhi tulie muweka madarakani tunaendekeza ushkaji, na ndio mana tunaendelea kuimuimbia ngonjera kila siku eti awawajibishe washkaji zake. Kwa usafi gani yeye alio nao? NI UMA UMUWAJIBISHE YEYE NA VIBARAKA WAKE!
   
Loading...