Sababu za kuipinga Serikali ya awamu ya tano

Sababu za kuipinga Serikali ya awamu ya tano

mwalimu lyapongoka

Senior Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
173
Reaction score
207
Mara zote tumekuwa ni watu wa kubishana tu pengine bila uelekeo kamili nje ya milengo ya kisiasa na tukumbuke elimu ya uraia inazidi kuongezeka kwa wananchi kadili upinzani unavozidi kukuwa. Watanzania wamejua wajibu na stahiki zao nyingi kutoka serikalini Mara baada ya kukua kwa siasa za ushindani mkali.KATIKA uchaguzi wa 2015 hakuna mwananchi ambaye alikua hajui yafuatayo na yanatakiwa kushughulikiwa na serikali itakayopewa dhamana.
1.Rushwa imekithiri hasa kwa police,hospitalini wilayani n.k(100% ya wtz wanaguswa)
2.Ufisadi kuanzia ngazi ya juu kabisa na athari zake(100% wanafahamu)
3.mifumo mibovu ya elimu(_miundombinu na mitaala)
4.Maslahi na mazingira duni ya kuishi walimu
5.utawala mbovu wa sheria
6.Uzembe makazini
7.mikataba mibovu ya madini
8.KATIBA MPYA
9.HUDUMA ZA AFYA MBOVU KUPINDUKIA
10.MIFUMUKO YA BEI
11.MISHAHARA YA WATUMISHI
12.BARABARA
13.Umeme na maji baadhi ya maeneo Mengi nje ya miji
14.kumwezesha mkulima kwa kumletea teknolojia ya uzalishaji na masoko ya ndani na ya nje
15., ....
16.......
17.....
18.....
kama sijakkosea hii ndio reference point ya ku assess performance ya serikali ya awamu ya tano kama wamefanikiwa au wameshindwa
 
Dr Mpango kasema ukuaji wa uchumi mwaka huu umeshuka kutoka 7.7% mpaka 6.8%!!

Kwa lugha rahisi uchumi umedumaa NA HIKI NDIO KIPIMO HALISI CHA UTAWALA WA MAGUFULI MPAKA SASA!! hayo mengine uliyoandika ni upuuzi tu na siasa zisizo na maana!!
 
Kuna ambao hawawezi hayo kwasababu ya mshushuo mkali awamu hii.
 
Mimi naipinga serikali hii kwa sababu zifuatazo:

1. Haiheshima uhuru na haki za mwanadamu ikiwamo ya kuishi.

2. Haiheshima katiba na sheria za nchi ambazo ndio muongozo wa mifumo yetu kama taifa.

3. Haiheshimu mihimili mingine ya dola kama Bunge na Mahakama, hivyo kuingilia utendaji wa shughuli za kila siku kwenye mihimili hiyo.

4. Imeshindwa kupambana na hawa maadui wa hii nchi toka kupata uhuru wa nchi hii ambao ni:

(i) Ujinga
(ii) Maradhi na
(iii) Umasikini

5. Haitaki kuambiwa ukweli madhaifu yake na kinyume chake inataka kusifiwa, kupigiwa vigelele na nderemo.

6. Inaleta mgawanyiko mkubwa sana wa kiitikadi kwenye jamii tunayoishi.
 
Magufuli: WATZ NIOMBEENI
Watanzania: MZEE USICHANGANYE SIASA NA DINI UTAFUTWA

HUYU NI MTU WA HOVYO ZAIDI HAPA NCHINI
 
Mimi naipinga serikali hii kwa sababu zifuatazo:

1. Haiheshima uhuru na haki za mwanadamu ikiwamo ya kuishi.

2. Haiheshima katiba na sheria za nchi ambazo ndio muongozo wa mifumo yetu kama taifa.

3. Haiheshimu mihimili mingine ya dola kama Bunge na Mahakama, hivyo kuingilia utendaji wa shughuli za kila siku kwenye mihimili hiyo.

4. Imeshindwa kupambana na hawa maadui wa hii nchi toka kupata uhuru wa nchi hii ambao ni:

(i) Ujinga
(ii) Maradhi na
(iii) Umasikini

5. Haitaki kuambiwa ukweli madhaifu yake na kinyume chake inataka kusifiwa, kupigiwa vigelele na nderemo.

6. Inaleta mgawanyiko mkubwa sana wa kiitikadi kwenye jamii tunayoishi.
Bila kusahau double standard.
 
Back
Top Bottom