Sababu za kufeli kwa matibabu ya chunusi , vipodozi na mtu kushindwa kupona tatizo lake

said rashid

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
203
112
acne.jpg
chunusi 2.jpg

Umewahi kutumia vipodozi kutibu chunusi au tatizo jingine na kukosa matokeo unayoyataka kisha ukabadilisha na kuanza kutumia vya aina nyingine? Hujawahi kumuona mtu mwingine akifanya hivyo?

Bila shaka imewahi kukutokea au umewahi kuona na kusikia ikitokea kwa mtu mwingine.
AFYA ZAIDI CONSULTANTS tumewahi kutibu watu wengi sana wa aina hiyo. Mtu amesumbuka sana na chunusi na kutumia dawa na vipodozi mbalimbali lakini hajapata matokeo mazuri, wengine tatizo la Mba, wengine madoadoa usoni na mwilini, wengine michirizi, wengine makunyanzi, wengine mafuta mengi usoni na wengine ngozi kavu na kadhalika.

Baada ya kuongea nao vizuri ana kwa ana au kupitia simu na kuwapa elimu na ushauri wa vitu vya kufanya na dawa na vipodozi vya kutumia wote wakapona vizuri ndani ya muda mfupi tu. Kama na wewe au mtu mwingine atakuwa na tatizo kama hilo basi awahi mapema AFYA ZAIDI CONSULTANTS kwa ushauri na kutibu tatizo lake haraka. Piga simu namba 0659528724 au 0784082847 na utahudumiwa na kupona haraka iwezekanavyo

SABABU ZA KUFELI KWA MATIBABU YA CHUNUSI AU VIPODOZI
Sababu kuu ni kukosa elimu na ushauri wa kitaalam wa matumizi sahihi ya vipodozi na jinsi ya kutibu chunusi na matatizo mengine ya ngozi. Kama tulivyoona kwenye somo lililopota juzi, chunusi husababishwa na kuchochewa na sababu mbalimbali. Maambukizi ya bakteria, mafuta mengi, homoni za uzazi, kuziba kwa matundu ya kupitia mafuta na baadhi ya vyakula, pia matibabu yake hutegemea na chanzo cha chunusi zenyewe. Ukitumia dawa au kipodozi cha kutibu tatizo jingine tofauti na chanzo cha chunusi husika basi ni dhahiri chunusi hizo hazitapona.

Sababu za kufeli kwa vipodozi na matibabu ya chunusi ni pamoja na
1. Matumizi Ya Vipodozi Feki Na Visivyo Na Ubora Unaotakiwa
Amini usiamini, kuna vipodozi visivyo salama, vipodozi feki na vipodozi visivyo na ubora unaotakiwa ambavyo vipo vinauzwa katika maduka mbalimbali Tanzania. Endapo utakuwa na chunusi na kutumia vipodozi hivyo basi ni dhahiri chunusi zako hazitapona. Pia zinaweza zikaongezeka na kuwa kubwa na nyingi zaidi, au unaweza ukapata matatizo mengine

Pata ushauri wa kitaalam. Tumia vipodozi halisi, bora na vilivyo salama
2. Matumizi Ya Vipodozi Visivyoendana Na Ngozi Yako
Binadamu tuna aina tofauti za ngozi. Kuna wenye ngozi kavu, ngozi za mafuta, ngozi za kawaida na ngozi mchanganyiko. Huwezi kupona chunusi endapo utatumia vipodozi visivyoendana na ngozi yako.
Pata ushauri wa kitaalam. Jua aina ya ngozi yako kisha tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
3. Vipodozi Visivyokuwa Kwa Ajili Ya Tatizo Lako
Hili hutokea mara nyingi sana. Ukitumia vipodozi ambavyo ni kwa ajili ya kuchubua ngozi au kuongeza maji kwenye ngozi basi huwezi kupona chunusi. Kadhalika na vipodozi vingine maalum kwa ajili ya matatizo mengine
4. Matumizi mabaya ya vipodozi
Ukitumia vipodozi vibaya huwezi kupata matokeo mazuri. Kwa mfano, kama kipodozi ni cha kupaka usiku tu na wewe ukapaka na mchana na jua kali basi ni dhahiri hautapata matokeo mazuri, na unaweza ukapata madhara
5. Kutotumia vipodozi kama inavyotakiwa
Kama inatakiwa kutumia kipodozi kwa muda wa miezi mitatu na wewe ukatumia kwa mwezi mmoja basi hautapata matokeo mazuri. Kama unatakiwa kutumia dawa na vipodozi aina mbili au tatu na wewe ukatumia cha aina moja peke yake pia hautapata matokeo mazuri.
Utajuaje jinsi ya kutumia vipodozi kama inavyotakiwa?

Pata elimu na ushauri kutoka kwa wataalam wa urembo na vipodozi – AFYA ZAIDI CONSULTANTS
6. Matumizi ya vipodozi vingine vinavyoharibu ngozi au ufanisi wa vipodozi vingine
Endapo hautajua na kutumia vipodozi vinavyoingiliana kikazi basi hautapata matokeo mazuri hata kidogo. Kwa mfano, matumizi ya poda na losheni kwa pamoja. Ni lazima utumie vizuri, vinginevyo mmoja hatofika vizuri kwenye ngozi na atashindwa kufanya kazi vizuri. Matumizi ya vipodozi vikali na vinavyoharibu ngozi wakati unaendelea na matibabu ya chunusi yataharibu ufanisi wa matibabu ya chunusi na hata kuzizidisha chunusi hizo.

CHA KUFANYA ILI KUPONA KABISA CHUNUSI NA MATATIZO MENGINE YA NGOZI
Sasa kupona ni rahisi. Cha muhimu zaidi ni kupata elimu na ushauri sahihi wa vitu vya kufanya na vitu vya kutumia ili kupona chunusi na matatizo mengine. Pata ushauri wa kitaalam kwanza kabla ya kununua vipodozi au kushauriwa na watu wasio wataalam. Kwa AFYA ZAIDI CONSULTANTS, ada ya elimu na ushauri wa kitaalam ni Shillingi elfu mbili tu (2,000/=) kwa sasa ambayo utatuma kwa Tigopesa 0659528724 au Airtel money 0784082847 na utapewa elimu na ushauri papo hapo ofisini au kupitia simu yako ukiwa popote ulipo Tanzania. Tupigie leo ili upone kwa uhakika ndani ya muda mfupi tu.


Ili kupona chunusi na matatizo mengine ya ngozi fanya mambo yafuatayo
1. Jua chanzo cha chunusi zako au tatizo lako la ngozi na vitu vinavyoziongeza
2. Pata elimu na ushauri wa kitaalam kutoka kwa wataalam. Sio kila muuza vipodozi ni mtaalam au anavijua vipodozi vizuri, ongea na wataalam
3. Jua aina ya ngozi yako kisha tumia dawa na vipodozi vinavyoendana na ngozi yako
4. Tumia vipodozi sahihi kwa tatizo lako
5. Usitumie vipodozi feki, visivyo salama na visivyo na ubora
6. Usichanganye vipodozi vinavyoingiliana kikazi na kupunguziana ufanisi
7. Tumia vipodozi vizuri kama ilivyoelekezwa
8. Kuwa mvumilivu. Tumia vipodozi kwa muda wote ulioambiwa

Pata ushauri wa kitaalam kwanza kabla ya kununua vipodozi au kushauriwa na watu wasio wataalam. Kwa AFYA ZAIDI CONSULTANTS, ada ya elimu na ushauri wa kitaalam ni Shillingi elfu mbili tu (2,000/=) ambayo utatuma kwa Tigopesa 0659528724 au Airtel money 0784082847 na utapewa elimu na ushauri papo hapo, aidha ana kwa ana au kupitia simu yako popote ulipo Tanzania. Tupigie leo ili upone kwa uhakika ndani ya muda mfupi tu.

AFYA ZAIDI CONSULTANTS tunakutakia afya njema na muonekano mwororo…………
 
Mi nkjua ata tunaonana physically uone ngozi yangu na unipe ushauri....kumbe ela kwnza alafu uka google ndo untumie kwny cm
 
Mi nkjua ata tunaonana physically uone ngozi yangu na unipe ushauri....kumbe ela kwnza alafu uka google ndo untumie kwny cm
Kwa watu wote waliopo Dar es salaam na maeneo ya jirani tunawakaribisha ofisini kwetu Ilala Bungoni na Temeke Buza. Hao tunaweza kuwahudumia physically kwa kuwapa elimu, ushauri na dawa au vipodozi vya kutumia wakiwa ofisini kwetu.
Kwa waliopo mikoa ya mbali au wasioweza kuja ofisini kwetu hao tunawapa elimu na ushauri wa kitaalam na kuwaambia dawa au vipodozi vya kutumia kisha wananunua huko waliko.
Angalia option ipi ni nzuri kwako kisha karibu sana!
 
Back
Top Bottom