Sababu za Hispania kuteua Waziri anayeshughulika na mapenzi

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Moja ya habari iliyomake headline kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni pamoja na hii iliyotokea Hispania ambapo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mariano Rajoy amethibitisha uteuzi wa Edelmira Barreira kuwa Waziri wa mapenzi.

Sababu zilizotajwa ni pamoja na hofu waliyonayo wanasiasa juu ya idadi ya watu inayoendelea kupungua tena kwa kasi ya kutisha.

Sababu nyingine iliyotajwa ni kuwa wanandoa
wanashiriki mipango ya uzazi pia hawana nafasi na wapenzi wao, hii inatajwa ndio imesababisha idadi ya watoto wanaozaliwa kupungua sana.

Aidha takwimu za hivi karibuni zimeitaja Hispania kama moja wapo ya mataifa yanayoongoza kwa kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa.

Waziri wa elimu wa nchi hiyo hivi karibuni aliwasilisha ripoti yake kwa serikali kwa baraza la mawaziri akilalamika kwamba madarasa ya shule hayana idadi ya kutosha ya watoto na akaonya
kwamba huenda ikaathiri Spain kiuchumi katika
miaka ijayo.

Katika kushughulikia ishu hiyo kwa haraka Waziri mkuu wa taifa hilo Mariano Rajoy amemteua Edelmira Barreira kuwa waziri anayeshughulikia mapenzi. Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na
kuuchochea umma kurudi vitandani na kusaidia
kutengeneza watoto ili kuijaza tena Hispania.

Chanzo: Millardayo.com
 
Kazi kubwa ya waziri huyo mpya ni kuja na mbinu za mikakati ya kuwahamasisha na
kuuchochea umma kurudi vitandani na kusaidia
kutengeneza watoto ili kuijaza tena Hispania.
aisee job true true yaani kule wanatafutiana mbinu za kuhamasishana kurudishwa vitandani wakati hapa kuna raia wanashinda vitandani 24/7/30....
 
Back
Top Bottom