Richard Mlangi
JF-Expert Member
- Sep 10, 2012
- 380
- 194
Katiba mpya sio ilani ya CCM, na CCM wanajitahidi kuipinga kwa vitendo ikiwamo kuyakataa maoni ya wananchi na kuweka maoni yao (ambayo kimsingi ni katiba iliyopo sasa) na kuhakikisha kila kifungu kinamaslahi kwa ccm na hivyo kuvuruga mchakato mzima wa kuandika katiba mpya.
Kwa mtazamo wangu, sababu za kufanya hivyo ni kuwa;
1. Udhaifu wa Katiba ya sasa (au hiyo wanayoandaa) unakifanya Chama tawala kushika hatamu ie mihimili ya dola ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali inakuwa chini ya Chama tawala.
2. Udhaifu wa Katiba ya sasa unaondoa utaifa miongoni mwa Watanganyika na hivyo kurahisisha matumizi mabovu na hata uporaji wa rasilimali za taifa ie hakuna Mtanganyika anayejihisi kuwa na wajibu kwa ardhi na rasilimali za Tanganyika maana Tanganyika haina mambo yake.
3. Udhaifu wa Katiba ya sasa unawafanya watendaji wakuu wa serikali kuwajibika zaidi kwa Chama kuliko Wananchi ie Chama kina uwezo wa kumuwajibisha kiongozi lakini sio Wananchi.
4. Udhaifu wa katiba ya sasa unawapa nguvu zaidi wanasiasa katika jambo lolote lenye mustakabali kwa taifa na kuwaacha kando wataalamu au wazalendo wasio na vyama.
5. Udhaifu wa katiba ya sasa hauweki mipaka au separation of powers kati ya mihimili ya dola ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali hali ambayo inafanya mihimili yote kuwajibika kwa mtu mmoja ambaye ni mwenyekiti wa chama tawala.
Mambo hayo yana faida kubwa sana kwa CCM !