Sababu ya Wamaasai kupewa kazi za ulinzi

Habari wanajamvi

Leo katika kutafakari kidogo, Nimejiuliza maswali mengi kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai hususan waishio mijini.Je,Ni kwanini kabila hili linapendelewa sana na wenye nyumba,ofisi,taasisi mbali mbali kama shule,kampuni binafsi n.k katika nafasi hii muhimu na nyeti ya ulinzi.

Bila shaka wengi wetu tumewashuhudia maeneo mbalimbali hasa katika kampuni binafsi na kwenye mageti ya nyumba kubwa kubwa wakiwa na silaha zao (rungu) wakiendelea na shughuli za ulinzi kuruhusu na kuamua nani apite au asipite.Lakini pia nimejiuliza kwanini kazi hii wasipewe ndugu zetu wachaga,wajaluo,wazaramo n.k.Jibu nililokuja nalo kichwani ni sifa kuu na heshima waliojijengea hawa ndugu zetu wamaasai katika kipengele cha "uaminifu".

Ni mara kadhaa sana utamuona mmasai akipokea rushwa au akifanya ufisadi wowote kwa lengo la kujinufaisha.Wamaasai ni waaminifu mno na sifa hii imewafanya kuaminiwa na taasisi pamoja na kampuni hizi.Mmasai sio mtu wa tamaa kutaka kujipatia hongo ili labda aweze kununua gari kali,au nguo,Nyumba n.k kwa kifupi ni watu wa kuridhika na hali waliyonayo.

Unaweza kudhani labda ushupavu na uwezo wao wa kupigana ndio unawapa hizo kazi lakini sikubaliani na hili kwakuwa pia yapo makabila kama wakurya,wameru n.k yanayojua kupigana sana lakini hawapati kazi hizi kama wamaasai.Nawasilisha!
Niliambiwa na afisa mmoja wa Polisi.
Usije thubutu kuajiri mmasai lubega kama mlinzi popote.
Aliniambia wana kesi nyingi ambazo walinzi wa kimasai wanashirikiana na majambazi na wakisha tekeleza uhalifu hawapatikani hata kwa dawa.

Alinambia wamasai hao lubega hawana fixed adddress yoyote na hivyo akitoweka huwezi mpata popote na polisi huwa hawana mahali popote pa kuanzia kuwatafuta.
Mmasai lubega is a person of no fixed abode, kwa hiyo ni security risk.
 
Wamasai wa sikuhizi hawaaminiki hushirikiana na majanbazi na alipiga tulip humuoni anahamia kwa wamasai wa kenya
 
Masai wapo Zanzibar hadi wameanza imba taarabu na mdumange wanacheza
 
Habari wanajamvi

Leo katika kutafakari kidogo, Nimejiuliza maswali mengi kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai hususan waishio mijini.Je,Ni kwanini kabila hili linapendelewa sana na wenye nyumba,ofisi,taasisi mbali mbali kama shule,kampuni binafsi n.k katika nafasi hii muhimu na nyeti ya ulinzi.

Bila shaka wengi wetu tumewashuhudia maeneo mbalimbali hasa katika kampuni binafsi na kwenye mageti ya nyumba kubwa kubwa wakiwa na silaha zao (rungu) wakiendelea na shughuli za ulinzi kuruhusu na kuamua nani apite au asipite.Lakini pia nimejiuliza kwanini kazi hii wasipewe ndugu zetu wachaga,wajaluo,wazaramo n.k.Jibu nililokuja nalo kichwani ni sifa kuu na heshima waliojijengea hawa ndugu zetu wamaasai katika kipengele cha "uaminifu".

Ni mara kadhaa sana utamuona mmasai akipokea rushwa au akifanya ufisadi wowote kwa lengo la kujinufaisha.Wamaasai ni waaminifu mno na sifa hii imewafanya kuaminiwa na taasisi pamoja na kampuni hizi.Mmasai sio mtu wa tamaa kutaka kujipatia hongo ili labda aweze kununua gari kali,au nguo,Nyumba n.k kwa kifupi ni watu wa kuridhika na hali waliyonayo.

Unaweza kudhani labda ushupavu na uwezo wao wa kupigana ndio unawapa hizo kazi lakini sikubaliani na hili kwakuwa pia yapo makabila kama wakurya,wameru n.k yanayojua kupigana sana lakini hawapati kazi hizi kama wamaasai.Nawasilisha!
Ilikua zamani mamasai ya siku hizi yameelimika yanapiga dili za magendo malindoni mpaka mali zinaomba poo.
 
Mmasai shujaa akiwa porini anauwa simba kwa mkono wake.mmasai huyohuyo akija mjini anasuka nywele wanawake nguvu hana
 
hawanaga time ya kupañga nyumba,so wanapolinda ndio sehemu yao ya kupumzika
mchana wanauza sendo, usiku wanalinda. Jamaa ni watafutaji. Wachache sana wanapanga chumba cha kuishi hasa kama anaishi na mke.
 
Uliona wapi mmasai jeshini?
Mkuu labda huifahamu vyema historia ya Jeshi

Yupo aliyewahi kuwa mnadhimu mkuu wa Jeshi. Lt. Gen. Gideon Sayore.

Kuna Col. Metili. Kwa uchache.

Wamasai wapo wengi tu Huko Jeshini. Na wanaimudu tu vyema hiyo kazi kama wengine.
 
kuna uwezekano mjumbe takwimu hana pia ..yaweza kuwa
 
Ni kweli kabisa.Yaani mmasai akiambiwa na boss wake hapa asipite mtu hakuna njia aise hata aje mkuu wa mkoa hapiti! Pia inasemekana wamasai kwao kuua simba ni swala la kawaida labda huenda ndiyo sifa inayowapa kazi mjini
hawacheki na kima
 
Back
Top Bottom