Sababu ya Wamaasai kupewa kazi za ulinzi

Sababu ya Wamaasai kupewa kazi za ulinzi

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
3,186
Reaction score
6,124
Habari wanajamvi

Leo katika kutafakari kidogo, Nimejiuliza maswali mengi kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai hususan waishio mijini. Je, ni kwanini kabila hili linapendelewa sana na wenye nyumba, ofisi, taasisi mbali mbali kama shule, kampuni binafsi n.k katika nafasi hii muhimu na nyeti ya ulinzi.

Bila shaka wengi wetu tumewashuhudia maeneo mbalimbali hasa katika kampuni binafsi na kwenye mageti ya nyumba kubwa kubwa wakiwa na silaha zao (rungu) wakiendelea na shughuli za ulinzi kuruhusu na kuamua nani apite au asipite.

Lakini pia nimejiuliza kwanini kazi hii wasipewe ndugu zetu Wachaga, Wajaluo, Wazaramo n.k. Jibu nililokuja nalo kichwani ni sifa kuu na heshima waliojijengea hawa ndugu zetu Wamaasai katika kipengele cha "Uaminifu".

Ni mara kadhaa sana utamuona mmasai akipokea rushwa au akifanya ufisadi wowote kwa lengo la kujinufaisha. Wamaasai ni waaminifu mno na sifa hii imewafanya kuaminiwa na taasisi pamoja na kampuni hizi. Mmasai sio mtu wa tamaa kutaka kujipatia hongo ili labda aweze kununua gari kali, au Nguo, Nyumba n.k kwa kifupi ni watu wa kuridhika na hali waliyonayo.

Unaweza kudhani labda ushupavu na uwezo wao wa kupigana ndio unawapa hizo kazi lakini sikubaliani na hili kwakuwa pia yapo makabila kama Wakurya, Wameru n.k yanayojua kupigana sana lakini hawapati kazi hizi kama Wamaasai.

Nawasilisha
 
Kwasababu ukimuajiri mmoja usiku wanakuja wengine 10 kwahiyo ulinzi ni uhakika
Yaani wewe!!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Yaani wewe!!
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Sababu hapo ni very simple. Wamasai huwa wanatamaduni ya kukutana na simba kupambana nae ili kuprove uwezo wao......so hii imewajengea picha ya ushujaa kuwa kama mtu anaweza pambana na simba basi hawezi shindwa pambana na binadamu......


Balaa lake ukipiga risasi hewani huwa wanatoka nduki
 
"Ni mara kadhaa sana utamuona mmasai akipokea rushwa au akifanya ufisadi wowote kwa lengo la kujinufaisha."
Lowasa kama mfano
 
Nimezaliwa na kukulia kaskazini, nimeishi na kukuwa na wamasai, hii jamii ya kimasai kwanza haina woga wa kupambana na mwizi au raia, hawa jamaa wanamsimamo balaa kutokana na mwongozo wanaopewa na boss wake. Akisema hakuna ni hakuna.

Swala la uaminifu inategemea ila kweli hawa jamaa hawana tamaa. Ukiajiri mmsai mmoja jiandae kupokea wengine kama watatu hivi kijiji wanabebana sana.

Changamoto walioyonayo sasa hivi ni kuongezeka kwa matukio ya ujambazi wa bunduki.
Ni kweli kabisa.Yaani mmasai akiambiwa na boss wake hapa asipite mtu hakuna njia aise hata aje mkuu wa mkoa hapiti! Pia inasemekana wamasai kwao kuua simba ni swala la kawaida labda huenda ndiyo sifa inayowapa kazi mjini
 
Uliona wapi mmasai jeshini?
Yupo mmoja luten alikuwa OC wa kombania yetu katoboa masikio kabisa ila kuna siku tuko darasi katusimulia jinsi walivyomnyanyapaa kuwa ni unfit lakini alipambana hadi akapata jeshi.
Yuko poa sana yaani tulimpenda maana yale majivuno alikuwa hana haya mpenda haki kwa wote hdi mimi nilimshngaa.
Kama huamini njoo in box nikupe jina lake umsachi fb yuko huko umwone wenyewe ili uamini ninachokuambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajamvi

Leo katika kutafakari kidogo, Nimejiuliza maswali mengi kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai hususan waishio mijini.Je,Ni kwanini kabila hili linapendelewa sana na wenye nyumba,ofisi,taasisi mbali mbali kama shule,kampuni binafsi n.k katika nafasi hii muhimu na nyeti ya ulinzi.

Bila shaka wengi wetu tumewashuhudia maeneo mbalimbali hasa katika kampuni binafsi na kwenye mageti ya nyumba kubwa kubwa wakiwa na silaha zao (rungu) wakiendelea na shughuli za ulinzi kuruhusu na kuamua nani apite au asipite.Lakini pia nimejiuliza kwanini kazi hii wasipewe ndugu zetu wachaga,wajaluo,wazaramo n.k.Jibu nililokuja nalo kichwani ni sifa kuu na heshima waliojijengea hawa ndugu zetu wamaasai katika kipengele cha "uaminifu".

Ni mara kadhaa sana utamuona mmasai akipokea rushwa au akifanya ufisadi wowote kwa lengo la kujinufaisha.Wamaasai ni waaminifu mno na sifa hii imewafanya kuaminiwa na taasisi pamoja na kampuni hizi.Mmasai sio mtu wa tamaa kutaka kujipatia hongo ili labda aweze kununua gari kali,au nguo,Nyumba n.k kwa kifupi ni watu wa kuridhika na hali waliyonayo.

Unaweza kudhani labda ushupavu na uwezo wao wa kupigana ndio unawapa hizo kazi lakini sikubaliani na hili kwakuwa pia yapo makabila kama wakurya,wameru n.k yanayojua kupigana sana lakini hawapati kazi hizi kama wamaasai.Nawasilisha!
Mlinzi mwaminifu hata kama ni goigoi ni bora mara kumi kuliko baunsa asiye na uaminifu.
 
Yupo mmoja luten alikuwa OC wa kombania yetu katoboa masikio kabisa ila kuna siku tuko darasi katusimulia jinsi walivyomnyanyapaa kuwa ni unfit lakini alipambana hadi akapata jeshi.
Yuko poa sana yaani tulimpenda maana yale majivuno alikuwa hana haya mpenda haki kwa wote hdi mimi nilimshngaa.
Kama huamini njoo in box nikupe jina lake umsachi fb yuko huko umwone wenyewe ili uamini ninachokuambia

Sent using Jamii Forums mobile app
Nipe jina lake inbox bas
 
Back
Top Bottom