Sababu ya mbwa kujipeleka kwa Chatu

Sababu ya mbwa kujipeleka kwa Chatu

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
11,250
Reaction score
24,083
Hii nimetoa Facebook.

DAR ES SALAAM;MIONGONI mwa nyoka wanaoogopwa sana na watu, ingawa hana sumu ni yule aitwaye chatu.
-
Huyu ni mmoja wa nyoka wakubwa zaidi duniani mwenye uwezo mkubwa wa kubana na hatimaye kumeza mawindo yake makubwa yaani wanyama.
-
Inaelezwa na baadhi ya watu kuwa, nyoka huyu anayedaiwa kuwa mkubwa kuliko wote duniani, ana nguvu ya asili inayomfanya mbwa amuonapo, ajipeleke mwenyewe na hatimaye kumezwa.
-
Hata hivyo, vyanzo mbalimbali akiwamo mwandishi wa kitabu cha ‘Bustani ya Mbwa’, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya mbwa, Dk Eugyne Emmanuel anasema si kweli kwamba mbwa hujipeleka kwa chatu kumezwa.
-
Vyanzo mbalimbali vinasema macho ya mbwa ni kama kamera za zamani, yaani uwezo wake wa kutambua rangi unaishia kwenye rangi nyeusi na nyeupe.
-
“Mawindo ya chatu huanza kwa kuweka mtego wa kipande cha mwili ambacho huwa na mng’aro sana. Kinachomponza mbwa ni kutaka kubaini akionacho ni nini na hapo ndipo hujikuta ameingia kwenye 18 za chatu.”

----
Imeandaliwa na Joseph Sabinus
#HabarileoUPDATES

Ninachojua/Kufahamu.

Kwa maelezo ya mtalaamu au mwandishi hapo juu yanaweza kuwa sawa au sio.

Iko hivi kwa uelewa wangu binafisi chatu humvutia mbwa,fisi na hata nyani kwa harufu anayoitoa na si mabaka kama ni mabaka au rangi yake basi ni kwa kiasi kidogo sana.

Mfano unaweza ukawa porini ghafla unahisi harufu ya wali au ndizi sasa ukiwa na mbwa atanza kuifutilia ile harufu na ghafla pasina kutegemea mbwa akiwa anashangaa shangaa hujikuta yupo kwenye Target ya chatu.

Hali kadharika kwa nyani huvutiwa kwa harufu ya ndizi yaani kitu anapenda!

Kwa fisi harufu ya mzoga mzoga na hayo hufanyika pale tu chatu anapoona windo tarajiwa!

Kwa binadamu ni mara chache sana ila mara nyingi humvutia kwa rangi zake inasemekana huwa anabadirisha rangi muda huo wewe kama binadamu ukiendelea kushangaa maajabu yake mara unajikuta ushanasa.(Hii sijaithibitisha maana haijawahi kunitokea)

Nahitimisha kwa kusema huenda huyo mwandishi hapo juu amezaliwa mjini na kukulia mjini akagoogle na kuandika kitabu chake cha BUSTANI YA MBWA.

Kwa maelezo niliyoyatoa mimi binafisi ndivyo nilivyoona kwa macho yangu. Tukio la.mwisho kulishuhudia ni mwaka 2014 kandokando ya mto Ruvu kisalawe Gwata!

Nikiwa na mbwa wangu natembea tembea nilihisi harufu kali ya ubwabwa na mbwa ikampa wazimu kuifuatilia na haikupita muda mbwa katoweka kumbe alirudi kufuatilia ile harufu Maana mwanzo mimi nilibaini kuwa huyu atakuwa chatu tu.

Baada ya kumkoswa ilibidi nirudi kwenye eneo lile nilihisi harufu ya wali wala haikunichukua muda kuona chatu mkubwa akiwa anamalizia kummeza mbwa wangu.
FB_IMG_1757215142314.jpg
 
Back
Top Bottom