Sababu ya kuwachukia wanawake & msamaha kwao.

Dec 11, 2020
62
157
Simulizi ya kweli iliyonitokea katika maisha yangu ya kimahusiano nitatumia neno "she".

Miaka kadhaa wakati nipo kwenye mahusiano mazito na mrembo mmoja.
shetani alinijaribu kupitia she mmoja ambaye alitokea kuwa karibu sana na Mimi ghafla.

Huyo she tulikutana kwenye ndege nje ya nchi Kama mjuavyo watanzania tunapokuwa nje ya nchi tunapoonana na watanzania wenzetu tunakuwa wamoja akaomba namba yangu kwa kuwa tulikuwa nje ya nchi na sote tulikuwa watanzania nilimpa.

Nakumbuka tulikuwa tunaelekea airport Moja hivi yeye akiwa anarudi Tz na Mimi nikiwa naenda nchi nyingine.

Zilipita wiki 2 ivi yule she akanitafuta na kuniambia alifika Tz salama huku akisisitiza tujuane vizuri.
Akiwa anajiexpress nikabaini kuwa ni mtu ambaye tumetoka mkoa mmoja Ila wilaya tofauti.

alionyesha heshima ya sayari ya Mars, alithamini muda wangu kupita kiasi, alionyesha upendo wa kiwango Cha sayari ya Mars, sms za kunijulia Hali zilikuwa zinaingia mithili ya sms za breaking news.

kwa wale wanaopenda vitonga Basi naweza kusema huyu alikuwa ATM. alikuwa tayari kunifuata nchi yeyote nje ya nchi yangu Tz kwa gharama zake tafasri yake ni kwamba alinipenda japo ilikuwa ni ghafla mno na Mimi nilikuwa na mtu wangu.

Hivyo sikumpa hiyo nafasi zaidi ya kumwambia ukweli wa kuwa nipo kwenye mahusiano mazito na mrembo mmoja na nilivyo mjinga siwezagi kutumika na mabibi wawili kwa wakati mmoja.

nikiwa kwenye process za kurudi Tz nilipoteza simu katika accident iliyotokea ilipelekea kupoteza mawasiliano namba zote zilipotea.

Baada ya kuona kimya kimezidi na online sipo akanitafuta social media na kupata jina langu Kisha akamfua inbox mtu ambaye ni rafiki yangu wa karibu.

niliporudi Tz nikiwa kwenye hospital fulani kuuguza majeraha yangu nikiwa na simu mpya & namba mpya ya Tz nikaona call ya unsaved namba ikiingia.

kumbe ni yule she alitafuta namba yangu mpya kutoka kwa rafiki yangu wa karibu social media kwa kumdanganya ety yeye ni mfanyakazi mwenzangu .

Yule she alinisumbua Sana na kutaka kuja kwangu lakini kwa heshima na uaminifu mkubwa niliokuwa nao kwa mtu niliyekuwa naye kwa relationship nilikataa kuonana naye kabisa maana alionyesha zahiri shahili yupo tayari 100% kulala na I.

To be honestly alinijali Sana kupita hata niliyekuwa naye kwenye relationship Kama ni marks alistahili 70% kwa 30%.

Laiti ningekuwa mtu wa Mambo mengi Basi ningefanya uasi usariti mkubwa sana.

Ashukuriwe MUNGU aliyeniepusha na hilo kwa kunipa hofu ya kuogopa usariti pamoja na akili za kuishi vizuri na mwanamke nimeweza kujifunza mengi Sana.

Nikilishtushwa na kukasirika Sana kuona yule she ananisumbua Sana licha ya Mimi kumwambia yule she kuwa nipo kwenye mahusiano tayari lakini alithubutu kuniambia anizalie japo Mtoto tu.

kwa hofu yangu na kuheshimu mahusiano niliyokuwa engaged niliona huyo she ni kirusi Cha kuharibu mahusiano yangu nikamwekea vikwazo ili asiweze kunipata hewani na kutoa taarifa kwa rafiki zangu.

Unaambiwa dunia haina Siri miezi 4 mbeleni yule she alijifungua mtoto kumbe kipindi ananisumbua alikuwa na ujauzito mchanga wa mtu mwingine so alitaka kuniuzia mbuzi kwenye gunia.

Kwa style hiyo aliyothubutu kutumia means wanaume wengi wanauziwa mbuzi kwenye Gunia na kulea watoto ambao sio wao kuweni wapole tu Siri ya mtoto anaijua mama la sivyo hakiki kwa DNA.

Bahati mbaya hospital aliyokuwa anahudhuria clinic kulikuwa na mtumishi wa hiyo hospital ambaye ni rafiki yangu ndiye aliyesimamia clinic check up za huyo she.

Ndiye alinisanua kwa kuvunja miiko ya kazi na kunifumbua macho plus ushahidi wa picha na video za she akiwa kwa clinic na n.k.

kubwa kuliko ni kwamba yule she alikuwa tayari ni mwathirika wa MWIKIU kwa mujibu wa Rafiki yangu ambaye ni mtumishi wa hiyo hospital, sikuamini niliomba kuthibitisha hayo kupitia huyo rafiki yangu namshuuru Sana alionyesha ushaidi wote.

Namshukuru Sana MUNGU kwa kuwa upande wangu na kunipa misimamo dhabiti kwani kwa akili yangu tu, kwa yule she nisingeweza kutoboa maana alikuwa mzuri Sana na mwenye kujitosheleza kwa kila kitu.

Sijisifu Bali Kuna muda Mimi mwenyewe najiuliza kwa nafsi nimewezaje kuruka mitego migumu hiyo sipati jibu naishia tu kusema ahsante Sana MUNGU.

Naamini wapo wanaume wengi waliopitia pito Kama langu na wakaishia kuanguka na kusariti wenza wao Sio kwa kupenda Bali kwa kuzidiwa maarifa na mbivu ovu za shetani.

WITTO:

Wanawake mlio kwenye mahusiano na mlio olewa waombeeni wenza wenu Maana mkono wa mwanamke makini una Baraka kwa mwanaume (maombi ni silaha).

Maana kuna mapito wanaume wanapitia kwa kweli kuchomoka ni ngumu Sana na wanasema hakuna mkate mgumu mbele ya chai kweli shetani ana nguvu Sana msichoke kuwaombea wanaume zenu.

Hapa nawasema wanawake sio kwa kuwatetea wanaume hapana Bali kwa kurejea mapito ya Mimi mtoa mada nikiwakilisha jinsia ya kiume.

MAUMIVU MAKALI:

Nilipata maumivu makali Sana mapaka nusu nimkosee mwenyezi MUNGU na imenichukua muda mrefu Sana kusahau hili tukio Mara baada ya kugundua usariti kutoka kwa mwanamke niliyekuwa naye.

Licha ya Mimi kuwa na misimamo na kuyapigania mahusiano yetu kwa kujilinda kumbe mwenzangu alikuwa na mtu ambaye pindi nikisafiri ndiye alikuwa mbadala wa Mimi.

Inauma Sana ndugu zangu unaweza hata kukufuru .

Wanasema Long distance relationship sio Nzuri lakini suala la kucheat ni tabia ya mtu kwani hata walio karibu nao wana cheat pia.

Binafsi niliamini mahusiano Salama na mzuri ni kutafuta mtu unayemfahamu zaidi na ikibidi awe ametoka familia unayoifahamu vizuri before ya yote. Na ndicho nilichokifanya kwani mwenzangu tulifahamiana vizuri tulitokea wilaya Moja.

Nilikuwa nawashangaa Sana watu wanaotafuta wenza wao kwa njia ya mitandao ya kijamii nikiamini si chochote si lolote lakini nimejionea wengi ndoa zao hazina wanaishi vizuri na maisha yanasonga.


Ndugu zangu Kuna wanawake wanajua kucheat mpaka ukishuhudia unaweza ukahisi upo ndotoni haijalishi ukimpata kwa njia gani. Mfano aliyekuwa wangu alikuwa anacheat huku akionyesha upendo wa kiwango Cha juu yaani Kama anakupumbaza vile ili umwamini Sana lakini nyuma ya pazia Kuna Giza nene japo kuwa niliona busy Sana nilijua kweli majukumu ya kazi kumbe sio.


Baada ya kutambua partner wangu sio mwaminifu na Kama mjuavyo maumivu ya usariti yanavyoumiza nilimwambia tusitishe kila kitu kila mtu aendelee na maisha yake.

Lakini aliniomba msamaha Sana na kulia Sana ugonjwa wangu upo kwenye chozi la mwanamke Nina huruma sana sipendi kuona mwanamke analia pamoja na kwamba kusariti kunaumiza Sana na wengi wanashindwa kusamehe.

ujinga wa huruma ukanifika nikamsamehe maana hakuna mkamilifu na nilitokea kumpenda Sana pia tulikuwa kwenye process za kufunga ndoa.

Baada ya hapo nikaomba twende tukapime Afya zetu Jambo ambalo lilimshtua lakini hakuwa na namna akakubali tukaenda.

matokeo ya vipimo yalikuwa mabaya kwa upande wake alikuwa mjamzito na mbaya zaidi naye alikuwa ameambukizwa MWIKIU.
niliumia sana zaidi ya Sana lakini nilimshukuru Sana MUNGU kwa kuwa nami kwa mara nyingine Tena.

Imani yangu dhidi ya wanawake ilifia pale maana sikuamini MTU ambaye nilimuamini Sana kuweza kufanya uasi Kama ule.

Basi sikuwa na namna niliamua kuachana naye japo niliumia Sana kwani nilimpenda na nilipoteza muda mwingi kwa ajili yake.

Toka hapo nimeshindwa kumuamini mwanamke yeyote Jambo lililopelekea nisiweze kujihushisha na mahusiano kwa muda mrefu Sana.

Ilifika hatua kazini na watu walionizunguka wakanilisema eti treni ilipita ikulu hivyo ikulu haifanyi kazi.

Lakini sikujali maana moyo wangu unajua umebeba nini ingawa Kama mwanaume niliona sio Jambo la kawaida kwangu maana hata hisia zilipotea kabsa.

Ikabidi nimuone doctor aliniambia ni saikology issue Wala sin tatizo lolote yaani ubongo wangu umeweka negative kwenye issue ya mahusiano namshukuru Sana naye ameplay part kwa kunitafutia mtalam wa saikology afadhali naiona.

Japo nina tatizo la stress Sana
Wenzangu wanasema nimekuwa mkali na Wala sikuwa hivi Tangu mwanzoni.


Baada ya muda mwingi kupita nimetafakari Sana na kuona hakuna haja ya kuwachukia wanawake wote kwa kuwavisha makosa ya wachache.

Nina amini wapo wanawake wengi wanaojitambua. Wenye hofu ya MUNGU na kujua thamani ya mahusiano & ndoa kwa ujumla.

Nafungua mlango rasmi kwa mwanamke serious mwenye sifa zifuatazo

1.mcha Mungu kweli kweli mwenye hofu ya MUNGU asilia sio kupretend.
2. Mrefu kiasi
3. Awe msafi Sana (in & out)
4. Umri 24-28
5.Elimu yeyote.
6. Mkristo
7.Asiyejua kucheat
8. Anayejua thamani ya mahusiano na ndoa.
9. Anayejua maisha ni nini, mwenye heshima, utii na uvumilivu.
10. Anayejitambua, awe na huruma na asiyeweza kunikumbusha yaliyopita.



Mengine ni ziada tu.

Naenda kufungua PM.
Ahsanteni Sana karibuni .
 
Too general. Ukiwachukia wewe usidhani wote tunawachukia mwanangu. Kila siku tunawapa majina mazuri kibao ukiachia mbali kuwahonga hata kwa kuuibia umma. Mpaka hapo huelewi mwanangu?
 
Too general. Ukiwachukia wewe usidhani wote tunawachukia mwanangu. Kila siku tunawapa majina mazuri kibao ukiachia mbali kuwahonga hata kwa kuuibia umma. Mpaka hapo huelewi mwanangu?
Rudia kusoma article yangu kwa utulivu Kisha rejea kwenye swali lako Kuna sehemu nafikiri hujaelewa vizuri ndugu.
 
Back
Top Bottom