Sababu ya Diamond kuwazidi wasanii wenzake kwenye kutoa vipaji vipya

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
384
2,525
Nataka niwamegee siri kidogo kwa nini Diamond ataendelea kuwaburuza wasanii wenzake kwenye kuinua na kuvitoa vipaji vipya.

Nikichukulia mfano wa msanii wake Zuchu.

1. Ameakikisha Zuchu ana nyimbo za kutosha tena kali za kuwashawishi wananchi yani kasimamia kwenye basics kwamba msanii ni nyimbo.

2. Alijiandaa kumtoa Zuchu lakini alikuwa anasubiri wakati sahihi na huu wakati wa corona umekuwa sahihi sababu shughuli nyingi za muziki zimesimama hivyo yeye na timu yake wana nafasi ya kutosha kuweka nguvu kwa Zuchu.

3. Uwekezaji, unaona kabisa Diamond anawekeza sio tu pesa bali muda wake na nafasi yake kuakikisha watu wanampokea msanii wake. Ukipita page yake ya Instagram unaweza sema ni fanpage ya Zuchu.

4. Qualities, unaona kabisa kila kitu anachofanya kwa msanii wake anahakikisha kinakuwa na kiwango cha staa mkubwa. (Mfano ni instalive ya Zuchu jana.) Hii inasababisha hata washabiki kumuweka msanii kwenye kiwango cha kina Nandi, Rubby na Vanessa ndani ya muda mfupi.

5. Branding; Kwanza kahakikisha Zuchu ni brand inayojitegemea angeweza kuamua Zuchu aje na nyimbo kashirikisha wasanii wote wa Wasafi kina Rayvanny Lavalava Mbosso na Diamond mwenyewe lakini ametaka wampokee Zuchu kama Zuchu. Zuchu yupo kila kona ya mitandao ya kijamii na followers wanaongezeka kwa maelfu kila saa na kila mtu ana muongelea Zuchu.

Kwa kifupi Zuchu ameiteka bongofleva tayari na pengine anaweza kuwa malkia mpya wa muziki east africa.

Hii ni kinyume na wasanii wenzake angalla Harmonize juzi kamtoa msanii wake kesho yake nae anaachia wimbo wake bedroom remix kashirikisha wasanii kibao. So anamnyima msanii wake jicho la kutazamwa watu obvious watatazama kazi ya Hamo na wasanii wengine wakubwa. Na hapo hapo anatangaza album yake kiukweli ni kama hajajipanga anawachanganya fans wake waweke concentration wapi.

Ali Kiba yeye anapokosea ni kila akimtambulisha msanii wake anataka aimbe nae, kiasi watu hawaamini tena msanii wake mpya wanamsikiliza yeye

Pia Ali style yake ya utoaji nyimbo ndio anaitumia kwa wasanii wake wachanga. Mtu kama Ki2ga tangia atoe Masozy watu wamekuja msikia tena baada ya mwaka as if nae ni staa. Anakuwa anaanza upya kila siku.

Msanii wa Kiba akienda kutambulisha nyimbo Kiba anakuwa pembeni hii ni mistake kubwa sana sababu yeye anawafunika wasanii wake. Anawatkiwa awaache wasimame wao kama wao yeye awape backup support.

Wasanii wa Kiba awana matukio wala awapo active mitandaoni yani ukitaka kuwasikia basi utafute nyimbo wameshaaminishwa wao ni team mziki mzuri so wameishia hapo. Huyu msanii wake mpya unaweza shangaa next week usimuone tena mitandaoni Kiba atakaa kimya na menejimenti haifanyi lolote kumsukuma aonekane.
 
Huo ndo ukweli, na kuongezea hapo, management ya Diamond ni watu wa Mziki.. Tofauti na Harmonize au Alikiba ambao kwenye swala la muziki wao ndio wao.. Pia Diamond anapenda kusikiliza na kushauriana na team yake kabla ya kufanya jambo lolote ndio mana unaona wanapeana support sana.
 
Wewe ndio umemjua Rayvan akiwa wcb , sisi tumemjua kumjua kuanzia akiwa TipTop connection ... Na Rayvan ametolewa na shindano la super nyota la clouds fm ndio akachukuliwa na TipTop ...

Nenda kasikilize wimbo wa Madee "Pombe Yangu " yule anaeimba "Sio Mimi eeeeh " ni Rayvan

Sent using Jamii Forums mobile app
kwan toka umsikie kwenye pombe yako hiyo, na sasa kwan uoni kuna utofauti ,
 
Punguza jazba mkuu, dunia yote inajua Rayvanny wimbo wake wa kwanza kumtambulisha mainstream ni Kwetu akiwa chini ya label ya WCB. Pengine bila Wasafi usingekuja kumsikia kabisa Ray, watu kutolewa na label fulani sio kwamba hawakuwa na mapito yao.
Wasanii wote wanaotoka wanamapito yao, hivi unajua kwamba Nandy alikuwa WCB kabla ajachukuliwa na Ruge? Harmonize alikuwa na album kabisa kwa Mazuu records kabla ajachukuliwa WCB.

Punguza chuki, appreciate.
Acha Pumba wewe labda Nandy wa uko Kwenu Nanjilinji..

Safari ya mziki kwa Nandy Ilianza pale alipopata Deal la kwenda kushiriki mashindano ya "Tecno Own the stage, tena alikua Chuo (CBE)
akiwa kwenye kipindi cha mithiani aliamua kufanya maamuzi magumu kuacha chuo na kwenda kushiriki mashindano hayo ya Tecno hali iliyomkosanisha na familia yake kuacha chuo kisa mziki.

Baada ya kurudi Tanzania aliitwa na Ruge ofisini kwake na kumwambia aje na CD za nyimbo Zake anazohisi ni kali

Baada ya Ruge kusikilizia alizivunja CD na kuzitupa kwenye dustbin na kumuuliza Nandy kama yupo tayari kuanza upya, Nandy akasema Yes Boss

Baada ya hapo Akaingizwa THT

Ebu twambie huyo Nandy aliyekua WCB ni yupi na Mwaka Gani?
 
Huna unalojua wewe dogo

Nandy kakaa sana bench WCB, hata ile sauti ya kike ya "Wasafi record" alikua yeye. Badae alichoka kusugua benchi akajikataa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom