SABABU TOP 10 ZITAKAZOUA UKAWA
¤UKAWA itakufa kabla ya uchaguzi au muda mchache baada ya uchaguzi. Zifuatazo ni sababu 10 zitakazoua umoja au kuufanya usiwe na nguvu (powerless and irrelevant)
1. MSINGI
Ili umoja udumu unahitaji msingi (foundation). Umoja wa UKAWA umejengwa kutokana na suala la bunge maalum la katiba ambalo hivi sasa halipo tena
2. UBAGUZI
Tanzania kuna vyama vyenye usajili wa kudumu 22. Ina maana vyama vya upinzani ni 21. Vyama vya UKAWA ni vi-4 tu. Vyama vya upinzani 17 havipo ndani ya UKAWA. Hivi vyama 17 vitapunguza sana umaana wa UKAWA hususan vikijitokeza vyama hata viwili vyenye nguvu kwenye baadhi ya maeneo. Na hapa naona chama cha ACT Wazalendo na ADC. ACT Wazalendo walikuwa tayari kujiunga na UKAWA. Ila CHADEMA hawataki. CUF, NCCR-Mageuzi na NLD hawana matatizo na ACT.
3. KUTOAMINIANA
¤Kutoaminiana kati ya vyama bado ni kukubwa sana. Chama kinachoongoza kwa kutoaminika ni CHADEMA. Bunge la mwaka 2005-2010 CUF kilikuwa chama kikuu cha upinzani bungeni huku Hamad Rashid Mohamed akiwa mkuu wa kambi ya upinzani na naibu wake akiwa Dr Slaa. Lakini bunge la 2010-2015 CHADEMA kilipokuwa chama kikuu cha upinzani hakikuwashirikisha wenzao. Walianza kuwaita CUF ni CCM B kwa vile tu wapo kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar.
¤Hii ilifuatiwa na CHADEMA kuiita CUF chama cha mashoga kwa vile tu ina ushirikiano na chama cha liberal nchini Uingereza (kwa kupitia hotuba ya John Wenje May-2013) jambo lililosababisha fujo kubwa ndani ya bunge.
¤CHADEMA inasemekana kuvitumia vyama vingine kwa faida yake binafsi. Kwa mfano uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 walikabaliana waachiane maeneo. Lakini CHADEMA wakaenda kinyume. Wakasimamisha wagombea kila mtaa na kitongoji ili baadaye waseme mgawanyo wa majimbo uzingatie ushindi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
4. KIKWAZO CHA SHERIA
¤Sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992 haijaweka mazingira ya kuwezekana kufanya coalition kama ilivyo Kenya.
¤Kenya inawezekana mgombea urais kutoka chama A na mgombea mwenza kutoka cha B. Ni kama ilivyo coalition ya Jubilee ambapo Rais Uhuru Kenyatta ni wa chama cha TNA na Makamu wa Rais William Ruto ni wa chama cha URP.
¤Kwa Tanzania mgombea urais wa UKAWA akitoka CHADEMA (kwa mfano) basi mgombea mwenza pia lazima atokea CHADEMA.
5. RUZUKU
¤Ruzuku kwa vyama inatokana na jumla ya idadi ya kura ambazo chama inapata kwenye uchaguzi wa rais na wabunge. Kwa mfano hivi sasa CHADEMA inapata tsh 200M kwa mwezi. CUF inapata tsh 117M kwa mwezi.
¤Chama kimoja (kwa mfano) kikisimamisha mgombea mmoja wa UKAWA, chama hicho kitapata kura nyingi na hivyo ruzuku kubwa kutokana na kuungwa mkono na vyama vingine.
¤Lakini hakuna utaratibu ndani ya sheria ya vyama vingi ya 1992 ambayo itaruhusu chama hiki kuvigawia vyama vingine sehemu hiyo ya ruzuku hata kama watakuwa wameandikishiana mikataba. Mikataba binafsi haipaswi kukiuka sheria za nchi.
¤Ikumbukwe pia mahesabu ya vyama vya siasa hukaguliwa na CAG kwa vile ruzuku zinatokana na hela za walipa kodi. Ugawanyaji huu wa ruzuku hauwezi kuwa na maelezo ya kueleweka kisheria na kikanuni.
6. VITI MAALUM
¤Suala la viti maalum ni kama la ruzuku. Idadi ya viti maalum vya chama hutokana na jumla ya idadi ya kura za urais na ubunge kwenye uchaguzi.
¤Chama kitakachosimamisha mgombea mmoja wa UKAWA kitapata nafasi nyingi za viti maalum kutokana na kuungwa mkono na vyama wenza ndani ya UKAWA.
¤Hakuna namna yoyote ya chama hicho kugawa baadhi ya nafasi hizo za viti maalum kwa vyama vingine ndani ya UKAWA.
7. USHIRIKISHWAJI MDOGO
¤Mamuzi ya vyama kuunda UKAWA ni makubaliano ya viongozi wao tu. Hayajawahi kushirikisha wanachama wa vyama vyao. Wanachama ni kama wanaburuzwa.
¤Tumeona wanachama wengi wa CUF wakinung'unikia sana huu mchakato mpaka kutaka kuandamana.
¤Kuna maeneo ambayo viongozi wamekubaliana jimbo lisimamishe mgombea wa chama A lakini wanachama wengi labda wanampenda mgombea wa chama B. Kwa mfano jimbo la Segerea wanaweza kumpa mgombea wa CHADEMA lakini labda wanachama wengi wa vyama vi-4 wangemtaka Julius Mtatiro.
8. NGUVU YA VYAMA
¤Kiuhalisia UKAWA ni CHADEMA. Vyama vingine vi-3 vinahitaji zaidi CHADEMA kuliko CHADEMA inavyowahitaji.
¤CUF ina nguvu Zanzibar ambako haihitaji msaada wa UKAWA.
¤Tanzania Bara, CUF ni dhaifu sana tokea mara ya mwisho mwaka 2000 (miaka 15 iliyopita) ilipokuwa na matokeo mazuri. Hivi sasa ina wabunge wawili tu bara yaani Salum Halfan Barwany (Lindi Mjini) na Suleiman Ali Bungala (Kilwa Kusini)
¤NCCR Mageuzi bila UKAWA nadhani hao wabunge wake wa-4 wanaweza wote kuwaponyoka. Machali kashahamia ACT Wazalendo. Labda
¤NLD hakuna haja ya kuizungumzia
¤Vyama ambavyo havina nguvu sawa ya majadiliano (Bargaining Power) sio rahisi kuwa na win-win situation.
9. MALENGO YA VYAMA
¤Kila chama lengo lake ni kushika dola. Hii ni kwa vyama vyote hata APPT Maendeleo.
¤Sio kweli kwamba lengo la chama cha upinzani ni kuiondoa CCM tu madarakani.
¤Chama kimoja kikishika madaraka kwa msaada wa UKAWA, sio kwamba vyama vingine vitaridhika.Na vyenyewe vitataka kukitoa chama hicho madarakani. Ni kama MMD ya Frederick Chiluba iliiondoa UNIP ya Kenneth Kaunda madarakani.
Lakini hivi sasa MMD pia haipo madarakani.
10. EXODUS
¤Kuna uwezekano mkubwa wa wagombea ubunge wa vyama vya UKAWA kukimbilia vyama vingine.
¤Hii ni kwa sababu kwa watu wengi, vyama ni platform tu siasa kwa vile sheria bado haijawezesha ugombea binafsi.
¤Mtu aliyejiwekeza kwa miaka mi-5 kugombea ubunge halafu akashindwa kugombea ubunge kwa vile tu viongozi wake wamekubaliana kuachiana majimbo, basi mtu huyo ni rahisi kuhamia chama kingine hususan ACT Wazalendo ili kujaribu bahati. Na ndio maana ACT inasubiri kwanza michakato ya CCM na CHADEMA iishe ndio na wenyewe watangaze wagombea wao.