kitwala
JF-Expert Member
- Aug 31, 2012
- 1,476
- 1,066
Mimi ni mwalimu wa Hisabati na Fizikia na hadi muda huu nimefanya kazi ktk vituo(shule) 4 tofauti, 3 kati ya hizo ni za serikali na 1 ni binafsi. Katika safari yangu hii nimegundua mambo yafuatayo ambayo kwa namna moja ama nyingine yametuingiza kwenye hii fani na kutuingiza kwenye mkataba wa kitumwa:
HITIMISHO: Kwa sababu nilizoziainisha hapo juu ni vigumu sana kwa walimu kuungana na kudai haki zao. Rejea matusi ya aliyekuwa naibu waziri wa elimu Mwantum Mahiza na mwajiri wake JK wakati wa vuguvugu la mgomo wa walimu 2009/2010.
WALIMU MAAMUZI YA CHAMA GANI KIWE MADARAKANI YAMO MIKONONI MWETU, TUAMUE SASA KWA FAIDA YA VIZAZI VYETU.
NB: HUU NI MTAZAMO WANGU TU, UNARUHUSIWA KUPINGA AU KUBORESHA.
- Takribani asilimia 70 ya walimu wote Tanzania tunatoka familia za kawaida sana kiuchumi. Sababu hii inatufanya walimu tuwe watu wa kutegemewa na familia zetu na ikumbukwe kuwa familia nyingi za mazingira haya ni extended family. Hivyo utakuta kwa mshahara huo mdogo unasomesha wadogo zako na ndugu zako wengine kadhaa.
- Tatizo la ajira na ukiritimba ktk upatikanaji wa ajira. Sababu hii huwafanya watu wengi kusoma ualimu kwa ajili ya uhakika wa ajira. Kama huna ndugu idara flani ajira kwako ndoto.
- Gharama za masomo kwa elimu ya juu. Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu lakini sanjali na hilo imeweka priorities kwa baadhi ya fani ikiwemo Elimu. Hali hii imepelekea watu wengi wasio na uwezo wa kujigharimia masomo yao kuangukia kwenye mtego huu.
- Udahili ktk vyuo, baadhi ya fani zimekuwa na competition kubwa na huku vyuo vichache vikitoa/kufundisha fani hizo. Jambo hili huwafanya wengi kukosa nafasi na hivyo kuangukia kwenye kokolo la ualimu.
- Ni kada hii pekee ndiyo inayotoa nafasi nyingi za ajira kwa wakati mmoja ukilinganisha na kada zingine. Hivyo kuwa na watumishi wengi kuliko kada zote.
- Cut off point. Baadhi ya fani zinahitaji ufaulu wa namna flani hivyo kuwafanya wale ambao hawajaqualify kutafuta alternative ambao wengi wao huangukia kwenye ualimu.
- Ukosefu wa ajira mbadala, mfano mwalimu wa grade A(Certificate) hana alternative na kuajiliwa sehemu nyingine yoyote tofauti na serikalini. Hivyo kumfanya mwalimu huyu wa primary kuwa mtumwa kwa serikali yake kwa sababu akiikosa ajira ya serikali ndiyo basi tena labda akajiajiri mwenyewe.
HITIMISHO: Kwa sababu nilizoziainisha hapo juu ni vigumu sana kwa walimu kuungana na kudai haki zao. Rejea matusi ya aliyekuwa naibu waziri wa elimu Mwantum Mahiza na mwajiri wake JK wakati wa vuguvugu la mgomo wa walimu 2009/2010.
WALIMU MAAMUZI YA CHAMA GANI KIWE MADARAKANI YAMO MIKONONI MWETU, TUAMUE SASA KWA FAIDA YA VIZAZI VYETU.
NB: HUU NI MTAZAMO WANGU TU, UNARUHUSIWA KUPINGA AU KUBORESHA.