Sababu kwanini siwezi kuoa mwanamke ambae hana degree

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,108
27,092
Ukiona mwanamke ana degree maana yake ni kwamba mwanamke huyo ni mvumilivu na amevumilia mambo mengi sana.

Kapambana na umande wa shule ya msingi kapambana kuanzia form one hadi form six na kikubwa zaidi kapambana na changamoto zote za chuo kikuu kuanzia mwaka wa kwanza hadi anamaliza.

Hakika mwanamke huyu ni mvumilivu na ana staili kuwa mke wa ndoa kama ameweza kustahimili changamoto zote za chuo hawezi shindwa stahimili changamoto za ndoa na maisha kwa ujumla.
 
Maisha ya ndoa hayaangalii elimu alonayo mtu,cheo, umbo ama sura!

Sidhani kama wazazi wetu walikuwa na hizo elimu ni wachache sana, lakini wameweza kutulea na kuvumialia changamoto zooote za mke/mume.

Tumekuwa tukijiwekea matarajio fulani kwa watu ambao tunataka wawe wenzi wetu, kitu ambacho hutuumiza baada ya ndoa. Kile ulichotarajia unakuta sicho, na wakati huo uko kwenye ndoa tayari. Hicho ndo chanzo cha mifarakano kwenye ndoa nyingi.

Mke au mume wa maisha yako yupo ila nikumuomba Mungu sana akupe wa kufanana nawe
 
Na usisahau kuwa hao wenye bachelor unaowazungumzia wamecheza ligi zote kuanzia ndondo mpaka eufa kwa hiyo usitarajie kitu tight wala mnato OK? Pia, wamesoma ile elimu ya kiliberali inayowafanya waweze kuquote vimisemo vya kibepari vinavyotetea haki zao..kama vile feminism, gender, equality, responsibility, equal Right na takataka nyingine nyingi kutoka huko mbele. Hivyo usiangalie upande mmoja wa shilingi tu, badala yake igeuze na uangalie kilichopo upande wa pili.
 
Maisha ya ndoa hayaangalii elimu alonayo mtu,cheo, umbo ama sura!

Sidhani kama wazazi wetu walikuwa na hizo elimu ni wachache sana, lakini wameweza kutulea na kuvumialia changamoto zooote za mke/mume.

Tumekuwa tukijiwekea matarajio fulani kwa watu ambao tunataka wawe wenzi wetu, kitu ambacho hutuumiza baada ya ndoa. Kile ulichotarajia unakuta sicho, na wakati huo uko kwenye ndoa tayari. Hicho ndo chanzo cha mifarakano kwenye ndoa nyingi.

Mke au mume wa maisha yako yupo ila nikumuomba Mungu sana akupe wa kufanana nawe
Ndiyo, unatudanganya..
 
Back
Top Bottom