Sababu Kuu Za utekaji Nchini Tanzania

Sababu Kuu Za utekaji Nchini Tanzania

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
795
Reaction score
1,848
TLS tuliitisha Mdahalo wa Kitaifa kuzungumzia Utekaji Baadhi ya sababu kuu zinazochangia utekaji kulingana na mjadala ule ni pamoja na

Udhaifu wa mifumo ya utendaji wa Jeshi la Polisi ( Colonial Mentality ) na kutotenganishwa kwa shughuli za Upelelezi na Uchunguzi kutoka Jeshi la Polisi na Kuwa Idara inayojitegemea na kujiendesha
Kukosekana kwa ufanisi katika vyombo vya usalama, ikiwa ni pamoja na upelelezi duni, rushwa, na ukosefu wa rasilimali, kumechangia wahalifu kuendesha vitendo vya utekaji bila kuogopa hatua madhubuti.
Uingiliaji wa siasa katika vyombo vya dola

Kuwepo kwa matukio ambapo vyombo vya dola vimetuhumiwa kushiriki au kufumbia macho vitendo vya utekaji, hasa kwa watu wanaoonekana kuwa tishio kwa mamlaka malalamiko haya tumeyasikia toka kwa Edgar Mwakabela,Mwamlima,Mdude Nyagali nk.

Kutokuwepo kwa uwajibikaji na haki kwa waathiriwa .

Hii inachangiwa na kukosekana kwa uwepo wa Taasisi ya kulisimamia Jeshi la Polisi haswa linapo lalamikiwa.Njia ya msingi ni kuiboresha Tume ya Haki za Bimadamu na Utawala bora kwa kuzipa Uhuru,Fedha ya kutosha,Kuajiri wataalamu na wapelelezi wake pamoja na kuwa na timu ya wanasheria wake wanao wajibika moja kwa moja kwa Tume hii.

Wengi wa waliotekwa au kutoweka hawajapata haki, na serikali mara nyingi haifanyi uchunguzi wa kina wa matukio haya na Polisi imekuwa ikitoa Majibu ya jumla jumla .Mazingira kama haya yanawapa wahusika ujasiri wa kuendelea na vitendo hivyo bila woga wa kuchukuliwa hatua.
Malengo ya kisiasa na udhibiti wa uhuru wa kujieleza

Baadhi ya matukio ya utekaji yameripotiwa kuwalenga wanaharakati, waandishi wa habari, na wanasiasa wa upinzani, jambo linaloashiria kuwa kuna nia ya kuzima sauti za upinzani na ukosoaji. Hii ni Mazingira kama ya upoteaji wa Kaina Soka na Wenzake,Madhila ya Kina Mdude Nyagali, Soka,Edagar Mwakamele,Mwalima ,Mzee Ali Kibao nk

Uhalifu wa kimfumo .
Uhalifu wa kupanga, kama vile magenge yenye nguvu, yanaweza kushiriki katika vitendo vya utekaji kwa lengo la kutisha, kupata fidia, au kusaidia ajenda fulani za watu wenye mamlaka.Lakini ni Mara chache magenge kqma haya kuteka wakosoaji .Haya yabakuwa na malengo binafsi yenye kulinda au kuendeleza magenge ya Kihalifu.
Kukosekana kwa sheria kali na Kukosekana utashi wa kuzitekeleza.

Ingawa kuna sheria zinazopinga vitendo vya utekaji, utekelezaji wake umekuwa dhaifu na hili pia linachangiwa na baadhi ya maamuzi ya Mahakama ambayo kwa mazingira yanatoa hifadhi kwa wenye dhamana ya kulinda uhai wetu kujificha na kukwepa wajibu wao, na hivyo kuruhusu vitendo hivi kuendelea pia nchi kutokuwa na mfumo thabiti na kuridhiwa kwa Mkataba wa Kimataifa kuhusu utekaji au upotezwaji wa watu.
cc.Mwabukusi
 
Back
Top Bottom