Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,350
- 26,166
Kuna mambo si ya kuyabishania. Ni ukweli kuwa Zitto Kabwe ni kati ya wabunge vijana wa kwanza nchini Tanzania 'kuaminika' kwa vijana na watanzania kwa ujumla. Zitto amekuwa kielelezo cha uthubutu wa vijana katika uongozi hasa katika ujenzi wa hoja, kusimamia anachokiamini na kulipua jambo la kitaifa ambalo limejificha.
Zitto, Mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini na sasa Kigoma Mjini, ana historia kubwa katika siasa za vyama akianzia CHADEMA na sasa ACT-Wazalendo. Zitto amesema na kusemwa kisiasa katika hoja za kichama na kiserikali. Kutokana na kuaminika kwa Zitto mkoani Kigoma, Zitto alithubutu na hata kuweza kubadili Jimbo la uchaguzi na kushinda.
Binafsi, sijawahi kumkubali Zitto kwa maneno wala matendo yake. Nina sababu kubwa moja tu: Zitto hamalizi jambo lake analolianzisha. Kuanzia kashfa ya Buzwagi, mabilioni ya Uswisi, uhaba wa chakula na sasa ununuzi wa ndege, Zitto hajawahi kumaliza jambo lolote kwa maana ya kutoa mrejesho kwa kile anachokianzisha.
Tabia hii ya kuachia mambo njiani inamfanya Zitto kuonekana kama mropokaji na 'mtafuta kiki' pale ambapo watu hawamtaji wala kumzungumzia. Binafsi, sijawahi kumuamini mtanzania yeyote ambaye haitimishi jambo analolianzisha. Ndiyo maana, simuamini Zitto hata chembe kwa mambo yake anayoyaanzisha pamoja na kukiri kuwa ni Mbunge na mwanasiasa wa mfano, hasa kwa vijana.
Ili aaminike, Zitto anapaswa kuwa anatoa mrejesho au hitimisho ya mambo anayoyaanzisha. Tabia yake ya 'kuonjesha' tu mambo ya kitaifa haimjengi kivyovyote kisiasa na inamporomosha kuelekea kwenye orodha ya wanasiasa matapeli na walaghai.