Sababu kubwa ya vijana wa Mbeya kuwazidi nguvu polisi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sababu kubwa ya vijana wa Mbeya kuwazidi nguvu polisi.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ozzie, Nov 13, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Bila shaka ni tukio la kwanza na la aina yake, kwamba polisi walishindwa kuwathibiti vijana wa jiji la Mbeya ambao walikuwa wakipambana nao kwa zaidi ya masaa ishirini. Kila sehemu ilisikika milio ya risasi na mabovu ya kutoa machozi. Hofu ya risasi ilisababisha kijana Mushi mkazi wa Uyole ayumbeyumbe akiwa pembezoni mwa barabara kuu na kusababisha agongwe na gari, na mpaka sasa kakatwa mguu wa kulia. Tukio hili lilihitaji msaada zaidi wa polisi toka wilaya za mkoa wa Mbeya, pia toka mkoa wa Sumbawanga, Iringa na Dar es Salaam.
  Kwa hakika vijana hawa ambao wamevikwa jina la wamachinga (japo ukweli wamachinga walikuwa wachache sana; na wengi wa vijana hawa ni wale waliozaliwa kipindi cha miaka ya mwishoni mwa themanini na mwanzo wa miaka ya tisini) wamekatishwa tamaa ya maisha na utawala ulioko madarakani.
  Ghasia zilianza maeneo ya Mwanjelwa wakati wakiwa na harakati za kujadiliana kuhusu kutimizwa kwa ahadi yao ya kupatiwa eneo la kufanyia biashara toka mamlaka za jiji na mkoa. Askari kadhaa wa jiji hawakufurahishwa na kusanyiko la vijana hawa kwa kuwa lilifanyika eneo ambalo wao walikuwa wameweka doria na pia lilipigwa marufuku kufanyia biashara za kimachinga. Hili likaleta majibizano yaliyosababisha vipigo vilivyoishia kuleta FFU na tukaishia kupata hadithi iliyopo mpaka sasa.
  Walianza kwa kufunga barabara kwa njia nyingi ikiwa ni pamoja na kutumia mawe, kuchoma matairi n.k. Eneo la mama John ndio kulikuwa na pingamizi kubwa kwa kuwa waliweza kung’oa miti mikubwa iliyopo kandokando ya barabara kama tembo vile na kufunga njia.
  Vijana hawa walipata nguvu kubwa pale Jeshi la Wananchi walipokuwa wakipita maeneo ya Soweto na Mama John walipoomba wafunguliwe njia kwa muda ili waweze kupita kwa kuwa wao ugomvi huo ulikuwa hauwahusu. Wanajeshi hao walikuwa wanapita barabara kuu iendayo Iringa, ambapo mwanzoni walikuwa wakipita kwenye service road mpaka walipofika sehemu ambayo iliwalazimu watumie njia kubwa ambayo ni kiunganishi cha eneo wanalokwenda. Hii ikawa sababu kubwa ya vijana wa Mbeya kupata nguvu. Ingawa kuna matukio yaliyoripotiwa kwa wanajeshi kutumia nguvu kwa baadhi ya watu, lakini haikuwa sana vile.
  Vijana hawa walikuwa na ushirikiano wa kustaajabisha na wakaweza kupambana na polisi. Madereva taksi wa Soweto wanasimulia kwamba kwenye kituo cha daladala cha Soweto, ambako kuna container la taka kama la tani kumi hivi, liliwezwa kuwekwa barabarani baada ya majaribio mawili ya vijana hawa kushindwa. Baadaye, waliamua kuvunja mabango ya mahoteli mashuhuri, pamoja na kituo cha mafuta Oilcom Soweto ili watumie machuma yake kubebea hili container ambalo ndani yake lilikuwa lina moto wa kuteketeza taka.
  Tunashukuru mapambano yameisha, tunawapa pole majeruhi na ndugu wa marehemu Kelvin Mwalongo. Bila shaka kila mtu ataona kuwa raia wamekuwa washindi dhidi ya polisi na serikali kwani serikali inazidi kupata ujumbe ya kwamba kutumia mabavu si njia sahihi. Na kwamba watu wameshawachoka, hivyo waanze kuwasikiliza wananchi na hasa vijana. Hili ni somo kubwa kwa watawala!!!!
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Pamoja na uzuri wa mada yako hujasema ni nini kimewatuliza vijana na kufikia muafaka japo wa muda.Nakushauri fanya editing kidogo.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Shukrani mkubwa kwa taarifa yako mkuu
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  badala wagombane na wazazi wao walio warithisha umaskini wakati wengine wanawarithisha utajiri
   
 5. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Nadhani hata hao polisi nao walikuwa upande wa wamachinga
  katika bango hili kuna ukweli ndani yake
  386523_241433489251932_100001558489297_681046_1251734107_n[1].jpg
   
 6. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hivi kweli unaona kuna dalili ya watawala wetu kusikiliza kwa nia ya dhati kilio cha wananchi?

  Hawa watawala wana macho ila hawaoni; wana masikio lakini hawasikii!
   
 7. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kweli akili ni nywele sishangai avatar yako inaonyesha huna nywele hivyo huna akili pia
   
 8. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Walitulizwa na mbunge wao! aliwaomba waache vurugu wakatii!!
   
 9. M

  Mwadada Senior Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Asante kwa taarifa. Bila shaka welevu wataanza kufanyia kazi hali inayosababisha machafuko ya namna hii.
   
 10. bmx

  bmx Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  fisadi mkubwa wee
   
 11. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  umeona eeeeeee
   
Loading...