Sababu chache za ndoa nyingi kutodumu

Sababu chache za ndoa nyingi kutodumu

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,474
Reaction score
4,007
Wana JF

Nimegundua kuwa ndoa nyingi hazidumu na miongoni mwa sababu za ndoa hizo kuto dumu ni:

1. Pamoja na msichana/mvulana kumlazimisha mwanaume amuoe kwa sababu familia yake ni tajiri au ina uwezo hivyo huelewa kuwa hataishi kwa shida kwakuwa wana uwezo watawasaidia,

2. Pamoja na msichana/ mvulana kumpenda sana mwenzi wake na kuona hawezi kupoteza iyo chance inabidi atumie kila njia ikiwemo ya kuenda kwa mganga amsaidie ili amuoe/aolewe,

3. Pamoja na kulazimisha kutokana na uwezo binafsi wa fedha au mali bila ya kujali kama mmoja atakuwa tayari kumlinda mwenzie wakati wowote wa shida na matatizo,

4. Pamoja na wengi kupitia misukosuko na matatizo ambayo hawakutarajia hivyo kushindwa kuelewa kuwa yaweza yakawa ya muda na baadae kupokea neema za mwenyezi Mungu na kusimama tena au zaidi ya walivyokuwa,

5. Pamoja na wengi kutokuwa wavumilivu katika shida za muda zinazotokea hivyo kuamua kutema big G kwa karanga za kuonjesha,

6. Pamoja na wengi kuto elewa maana ya ndoa,

7. Pamoja na wengi kutarajia makubwa kitu ambacho hakitokei kwa muda alio pangilia na kuamua kujitoa,

8. Pamoja na wengi kutokuwa na uzoefu wa kumlea mwenzi katika maisha ya kila siku (mwanamke kujua wajibu wake katika ndoa na mwanaume kujua wajibu wake katika ndoa),

9. Pamoja na umri wa kuoa au kuolewa kuwa mdogo hivyo kuwa na tabia za utoto ambazo mmoja hatozipenda na kuona kero au usumbufu,

10. Pamoja na kuvamiwa na kuruhusu majini kuvamia ndoa hivyo kuwa sambaratisha,

11. Pamoja na kutokuwa waaminifu kwa kila mmoja na kuridhika na hali ya kila mmoja kitandani au kushindwa kuelekezana,

12. Pamoja na msichana kutoka kwao bila ya kufundwa hivyo kufanya ambayo siyo au yasiyo mpendeza mwanaume na kushindwa kuomba ushauri ambao utakao msaidia kwenye ndoa yake,

13. Pamoja na kuwa na tama zilizo pitiliza na hivyo kudaiwa pesa nyingi ambazo mwenza hana uwezo wa kulipa na badae kusababisha chuki na kuamua kuachana,

14. Pamoja na msichana kutamani mwanaume na sio kumpenda badae huwa naye kwa maslahi zaidi,

15. Pamoja na kutokuwa na chaguo sahihi ya mwanaume au mke ambaye anaendana na mmoja wao.
 
Una miaka mingapi kwenye ndoa???

Hekima na busara ni mazao ya 'umepitia yapi na mangapi katika maisha, ambapo mengi ulipata ufumbuzi wake'.

Hekima na busara si MVI wala umri, UNA MUDA GANI KWENYE NDOA YAKO???
 
Back
Top Bottom