Sababu baadhi ya Walimu kupoteza mvuto kwenye jamii

Sababu baadhi ya Walimu kupoteza mvuto kwenye jamii

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
Kabla ya Miaka ya 2000 thamani ya taaluma ya Ualimu na Waalimu ilikua juu ikielekea kufanana na ya wabunge na wafanya kazi wengine katika serikali.

Enzi za nyuma waalimu walikua watu wa kusikilizwa na Kupewa Nafasi katika mambo mbalimbali ya kijamii hata pale mabishano yalipotokea Mwalimu aliitwa ili Kutoa sulusho na alisikilizwa.

Katika maeneo Mengi Nchini Jamii iliona Fahari kuwa na Mwalimu hivyo mwalimu alihakikishiwa Usalama hata Kupewa ardhi, mifugo ili aishi kwa Raha ahisi kuwa yupo nyumbani hata Kama hayupo maeneo ya kwao.

Kijijini kwetu Mtoto wa mwalimu alithaminiwa kua mtoto wa mtu mwerevu na kioo Cha Jamii Hilo halikupingika na kila mtu kwenye jamii.

Kwanzia miaka ya 2000 thamani ya Waalimu ikaanza kushuka taratibu na Jamii ikaanza kuiona Kama taaluma ya Uhuni iliyopoteza mvuto chanzo ikiwa Ni tabia mpya zilizoibuka kwa kizazi Cha Waalimu wa Karne ya 21.

Mfumo wa Utoaji kipaumbele kwa ajira za Ualimu wa Rais Jakaya kikwete ulichangia kwa kiasi fulani Waalimu kupoteza heshima kwa jamii Hii ni kutokana na ingizo jipya la Waalimu vijana ambao hawakupikwa Vizuri katika misingi Bora ya maadali ya Ualimu huko vyuoni.
Tabia na mwenendo mbaya wa waalimu ikapoteza Imani kwa Jamii ikaanza kuona kuwa ni taaluma ya kihuni, Waalimu wakaanza kupuuzwa kwa kiasi fulani.

Muenendo mbovu wa baadhi ya Waalimu wenyewe wawapo mashuleni umesababisha wapoteze mvuto kwa jamii, mfano jinsi wanavyo ishi na Wanafunzi pasipo kufuata maadili ya taaluma Yao kwa kujihusisha na Mahusiano ya kimapenzi na Wanafunzi wao kitu Ambacho ni kinyume na Sheria na kina itia aibu taaluma ya Ualimu.

Pia Ukatili na Uonevu unaofanywa na Waalimu mashuleni umechangia kuwapotezea heshima na kufanya watu kuwaona Waalimu Kama watu waonevu na wakatili wanao adhibu watu pasipo kuwasikiliza, wanaobambikiza makosa kwa Wanafunzi ili kuwafukuza Shule.

Kitendo Cha baadhi ya Waalimu kuwa waonevu kimefanya Wanafunzi wawaone Waalimu kua watu wakatili na wasio na utu, mfano Waalimu wa nidhamu na malezi kwa Wanafunzi ni miungoni mwa Waalimu wasio na utu kwa Wanafunzi na Ni Vinara wa Uonevu mashuleni.

Mimi mwenyewe Sitasahau nilivyowahi kubambikizwa Kesi ya kumfanyia kiburi mwalimu wangu aliekua anafundisha moja ya somo la sayansi Shuleni kwetu nikapewa adhabu nzito pamoja na kuchapwa mbele ya umati wa Wanafunzi wote Shuleni hapo.

Waalimu wengi wamekua wakijificha kwenye kivuli Cha udogo wa mishahara Yao kua ndio chanzo Cha wao kupoteza heshima kwa jamii lakini Sio kweli katika Hilo maana hata Waalimu wakilipwa mshahara sawa na mawaziri lakini wasipobadili muenendo wao bado Jamii haitawaheshimu Kama zamani.

Waalimu ni watu muhimu katika taifa lolote Lile duniani hivyo Waalimu wa Tanzania hawana budi kubadilika na kujiheshimu ili taaluma Yao iheshimike na wao waheshimike pia Kama ilivyokua hapo awali.

Peter Mwaihola
1666759750422.jpg
 
Mambo yalianza kuporomoka ktk idara hiyo kuanzia 1974/5 . Pale Azimio la musoma (UPE) ilipoanza kufanya kazi bila waalimu wa kutosha. Na hivyo kulazimika kuchukua drs waliofeli kuendelea na masomo, na kupewa kozi ndogo kwa mratibu wa elimu kata. Nakuwafanya kuwa waalimu. So from then teaching ilionekana kama ya malooser. Ikaja na hiyo project ya JK pale UDOM .

So tumeingiza wasiohusika kwenye taaluma kwa sababu za ajira .
 
Ugumu wa Maisha ndo umezaa yote hayo ...

Ujira Mdogo kwa waalimu huku mkiwapa majukumu mazito ya kufundisha watu walioshindikana kitabia nenda shule za Serikali mjionee
 
Back
Top Bottom