Sababu 5 Kwanini Wasichana Warembo Hawaolewi

Sababu 5 Kwanini Wasichana Warembo Hawaolewi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
1547149962708.png






Wanawake wengi warembo/wazuri husalia peke yao na kufa katika hali hiyo kutokana na sababu tofauti.

Wengi huwa na tabia za kuudhi hali ambayo huwafukuza wanaume walio na uwezo wa kuwaoa.
Umewahi kushangaa sababu za wanawake warembo zaidi kutoolewa?

Umewahi kujiuliza Nani anataka kupanda miwa kwenye shamba karibu na shule?(sijui kama hiyo miwa itabaki salama na jopo lote la wanafunzi lililopo hapo shuleni)


Wanaume sio wajinga na katika asilimia kubwa ya wanawake wanaoolewa huwa ni waajabu sana ukiwaangalia kwa machoni kwa jinsi walivyo, mpaka unakuta wengine wanajiuliza, ‘huyu mwanaume mzuri hivyo anamuoa mwanamke ambaye hawaendani’.

Ukiwa mzuri utapndwa na wanaume wengi ila watakupenda kwa lengo moja tu, ‘Mapenzi’ baada ya hapo utakuwa wa kuchezewa na kuachwa.
Kuna sababu tano ambazo huwafanya wanawake warembo/wazuri kusalia wapweke.



  1. Tabia
Wanawake kama hao huwa na tabia mbaya(uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri, marafiki) ambavyo hupelekea kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume. Wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani.


  1. Baadhi ya wanawake hao huwa na maringo sana
Eti hawawezi kuosha nyumba kwa kuogopa kucha zao zisikatike. Wengine hawaju kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.


  1. Ghali kuwatunza
Wanawake warembo huwa ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwa kubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali. Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.


  1. Wabinafsi na wenye chuki
Wanawake wa aina hiyo hufikiria dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanamume. Wanaume wengi hupenda kuhusiana na wanawake wa aina hiyo, ambao huwadharau kutokana na kuwa “wanapendwa” na wanaume wengi.
Wasichojua ni kuwa wanaume huwatumia tu na kuwaacha kutokana na tabia zao ili kutafuta mwanamke mzuri wa kuoa.

  1. Hawataki kuwa wazazi
Wanawake hao hupenda kusalia wakiwa wa kupendeza, hivyo huwa wanaogopa kuzaa wasipate mikunjo, wasinenepe au kuwa na matiti kulegea. Kwa kawaida, hakuna mwanamume anayependa kuoa mwanamke ambaye hawezi kumzalia, hasa kwa sababu ya utamaduni wa Kiafrika.
Kama una sifa za aina hiyo, huenda ni wakati wako kubadilika ikiwa unataka kupata mume.
 
Kuna mmoja hapa ninapokaa kuna genge sasa humlazimisha muuza genge ampelekee dagaa walikatwa vichwa tayari. Nazi ananunua iliyokwisha kunwa mchicha uliyochambuliwa. Nimeuliza kulikoni mwenye genge kasema eti anasoma chuo hajazoea hahaaaaa....hivi visichana shida sana

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Kuna mmoja hapa ninapokaa kuna genge sasa humlazimisha muuza genge ampelekee dagaa walikatwa vichwa tayari. Nazi ananunua iliyokwisha kunwa mchicha uliyochambuliwa. Nimeuliza kulikoni mwenye genge kasema eti anasoma chuo hajazoea hahaaaaa....hivi visichana shida sana

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Wanachuo wanawasumbua sana watu wa gengeni, bodaboda na wavibanda vya chips
 
Wanawake warembo wanasumbua sana. Siku moja niliopoa demu makali sana lakini alivyonisumbua sina hamu nao. Siku hizi huwa nawatizama tuu
......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
je wale wazuri walioolewa unawaweka katika kundi gani?
 
Back
Top Bottom