Sababu 4 zilizlifanya Qatar kutengwa na mataifa ya kiarabu

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,977
2,200
1.Kundi la Muslim Brotherhood
Baraza la ushirikiano wa mataifa ya ghuba, yanasema kuwa Qatar iliunga mkono upinzani wakati wa vuguvugu lililotokea kwa mataifa ya kiarabu.
Doha, ilionekana kama muungaji mkono wa makundi ya kiislamu, ambayo ilitaka kupata umaarufu katika baadhi ya mataifa ya kiislamu.
Kwa mfano, baada ya kuondolewa kwa Rais wa Misri Mohamed Morsi - kinara mkuu wa Muslim Brotherhood - ambaye alitimuliwa mamlakani mwaka 2013, Qatar iliwapa hifadhi wanachama wa kundi hilo ambalo limepigwa marufuku na utawala wa Misri.
Saudi Arabia na Milki za kiarabu UAE pia zilitaja Muslim Brotherhood kama kundi "la kigaidi".
Katika taarifa iliyochapishwa katika mtandao rasmi wa habari za utawala wa serikali ya Saudia, Qatar ililaumiwa kwa "kuzikubalia makundi kadhaa ya kigaidi na makundi yenye itikadi kali yenye nia ya kuyumbisha amani katika kanda ya mataifa ya kiarabu, kwa pamoja na makundi kama la Muslim Brotherhood, Daesh (Isis) na Al-Qaeda".
Hata hivyo, Wizara ya nchi za nje ya Qatari, ilisema kuwa hatua zilizochukuliwa na Riyadh, Abu Dhabi na Manama "hazikuridhisha na yanaegemea madai yasio na msimamo kabisa wala ukweli".
TTaaarifa hiyo aidha inasisitiza kuwa, Qatar inafaa "kujitolea " chini ya mkataba wa GCC na "kutekeleza majukumu yake ya kukabiliana na ugaidi na itikadi kali".
2.Mbinu ya Iran
Mzozo wa sasa ulianzishwa na taarifa iliyokataliwa iliyomnukuu Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, akikosoa "uadui" wa Marekani dhidi ya Iran.
Qatar ilisema kuwa wadukuzi wanatazamiwa kuchapisha maoni hayo katika shirika lake la habari la taifa.
Saudi Arabia, mpinazi mkuu wa taifa hilo la kiislamu, limekuwa likitatizwa kwa muda mrefu na umaarufu wa Iran katika kanda hiyo.
3.Mzozo nchini Libya
Libya imekuwa katika lindi la mzozo tangua kuangushwa kwa utawala wa Rais wa nchini Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Kiongozi mkuu wa jeshi ya Libya Khalifa Haftar, ambaye alipata uungwaji mkubwa kutoka Misri, Milki za kiarabu UAE na Qatar, aliilaumu Qatar kwa "kuunga mkono ugaidi".
Haftar anaongoza serikali iliyoko mashariki mwa Libya katika mji wa Tobruk. Ilihali Qatar inaunga mkono serikali pinzani iliyoko katika mji mkuu Tripoli.
4.Mzozo wa vyombo vya Habari
Mara tu taarifa tatanishi ilipotolewa ikimnukuu Emir wa Qatar mnamo Mei 23, vyombo vya Habari huko UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri yalianzisha ukosoaji mkubwa dhidi ya familia inayotawala Qatar.
Mataifa hayo manne yaliamua kwa kauli moja kuzima mtandao wa habari wa Qatar.
 
1.Kundi la Muslim Brotherhood
Baraza la ushirikiano wa mataifa ya ghuba, yanasema kuwa Qatar iliunga mkono upinzani wakati wa vuguvugu lililotokea kwa mataifa ya kiarabu.
And who are the sponsors of ISIS, Al-Qaeda, Nusra Front etc..Saudi Arabia, USA, Zionists. This is double standards
Both sides sponsor terrorism on opposing sides. So, this is what annoys the big brother Saudi Arabia. t the core of this is supremacy battle between Iran and Saudi Arabia. The rest are just hot air.
 
Yaonekana Trump alimpiga mkwara Saudia, amuundie zengwe Qatar, sababu USA wanasema Asad anapata sapoti kubwa kutoka kwa Qatar..sijajua Qatar atajinasua vipi na hizi fitna..
 
The main issue between Qatar and other middle East countries has nothing to do with Russia but but it's a game of superiority between Saudi Arabia and Iran and in extension the enemity between USA against/Israel(Zionists) and Iran. The Saudis are just fighting a proxy war ob behalf of USA and Israel(Zionists).
Whatever.
 
4.Mzozo wa vyombo vya Habari
Mara tu taarifa tatanishi ilipotolewa ikimnukuu Emir wa Qatar mnamo Mei 23, vyombo vya Habari huko UAE, Saudi Arabia, Bahrain na Misri yalianzisha ukosoaji mkubwa dhidi ya familia inayotawala Qatar.
Mataifa hayo manne yaliamua kwa kauli moja kuzima mtandao wa habari wa Qatar.
Wanalenga kuinyamazisha al-jazeera,wanadai ni hostile.
 
Wewe unaona hivyo vitambala vya FaizaFoxy kajifunga tangia mwaka 1970s hadi leo hajabadilisha Unafikili ni wa kisportsport!? Yaani yeye ni black ila ukimchana damu ni Mwarabu haaaaaa haaaa haaaa haaaaaa teeeh teeeh teeeh teeeh teeeh!

Ila, USA anatumia ujanja kuwachanganya wote ili awatawale vizuri bila wao kuelewa kinachoendela.
 
Saudi Arabia is the biggest sponsor of Terrorism. Who is bankrolling ISIS? who is supporting Manama? Kama wengine walivyosema..hii ni Vita ya Saudia na Iran. Mengine ni hot air hayana ukweli.

But what Saudia misses, is that it can never, NEVER win against Iran. They are trying whatever they can to lessen Iran's influence but unfortunately they are ill equipped to do so. Iran has an army. It has atleast resemblance of democracy. Angalia vita ndogo ya Yemen kuwaondoa Houthis..imemtoa Kamasi Saudia. Na ile vita haziishi leo wala kesho.

By the way Qatar hosts the largest US Base in the Middle East with more than 10000 troops near Doha. I am sure US is happy. Ukitaka kuwatawala hawa waarabu..just confuse them against each other and you win.
 
Saudia Arabia ipo mbali na Ugaidi na ndo Nchi inayopiga Vita Ugaidi kwa 100% serikali ya Saudia ime piga marufuku uchapishaji wa vitabu vya Ikhwan Muslimini (Muslim Brotherhood) na Usambazaji wake wala vitabu vyao havifundishwi Saudia kuanzia mashuleni mpka vyuoni
 
Hivi hizi nchi za mashariki ya kati viongozi wake wanakula maharage ya wapi sijui "fitna"zinaandaliwa na wao wanazidandia kama "sangara na ndoano"halafu baadae raia wanakuja kupata taabu.mimi naona Omani na wajanja wao..wanaangalia zanzibar tu.
 
Back
Top Bottom