Dah hapa ndio hizi dini huwa zinanichanganya.
Kila mtu HUVUTIA KWAKE.
Nilisoma na ustadhat mmoja, alinifundisha vizurii kuhusu uislamu na kuamini uislamu ili uende mbinguni.
Ila wakati huohuo nyumbani nikawa nipo karibu na aliyeokoka mmoja akawa ananifundisha safii Mambo ya kikristo na kwenda mbinguni.
SASA NIKABAKI KUJIULIZA, HAWA WATU WANATOFAUTIANA KWA SENSE AU WAMEKUSUDIA KUCHANGANYA MAMBO YA MUNGU?
#YNWA
Sijakuelewa.Hata hivyo Bwana Yesu katika Yoh.14:6 amesema,
" Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi."
So the answer is simple,muamini Bwana Yesu urithi Ufalme wa Mbinguni,mkatae uwe condemned to Eternal Hell.
Finally,hebu soma hii⬇️.Je ungependa kuwa associated with such a faith,be your own judge.
Uhusiano wa Uislamu na Majini !
NB:Maoni yaliyotolewa hapa sio ya muandishi,ni maoni yatokanayo na Quran.Mahali ambapo maoni ya Biblia yametumika,muandishi ameweka wazi.
Katika moja ya mambo yenye kutushangaza sana sisi Wakristo ni kwamba hatuchangamani kabisa na majini au Mashetani wala hatuna uhusiano nayo.Kinyume na hilo wenzetu Waislamu wana uhusiano mkubwa na wa karibu na majini na mashetani na kwa ujumla Masheikh na Maalimu wanatumia Quran kutibu au kulaani watu(
al-Badir).Waislam hutumia nguvu za majini ambazo ni nguvu za giza. Muhamad pia alitumia nguvu hizo za giza. Kuna wakati ambapo Wakristo kutoka Narjan Kusini mwa Saudi Arabia walimtembelea Muhamad kujadili mambo ya dini kwa siku kadhaa baada ya Wakristo kukataa kusilimu.Muhamad akasema “njooni hadharani tukusanyike pamoja wana wetu na wana wenu,wanawake zetu na wanawake zenu,sisi na ninyi kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana kwa Mungu iwashukie waongo! (
surat al Imran 3:61).Muhamad alitaka kuwalaani Wakristo kwa jina la Allah na Wakristo walaani kwa jina la Yesu kuona nani mwenye nguvu.Wakristo walikataa kwani hawakuitwa kulaani bali kubariki tu.
Kuna hadithi pia kuwa Muhamad alikwenda Yerusalemu.Akafika pale lilipokuwa Hekalu la Wayahudi. Wenyewe Waislamu hupaita Baittil Maqdis.Muhammad alitumia usiku moja kufika kwa kutumia mnyama aitwae “Buraq.” Mnyama huyu ni Jinni lenye sura ya mwanamke mzuri na mwili wa Farasi (Soma kitabu, Maisha ya Nabii Muhamad uk 28 kifungu cha mwisho).Jambo hili lilimfanya akataliwe zaidi na watu wa Makka wakisema ni mchawi mkubwa na hawako tayari kumuamini mchawi.Hizi ni khadithi chache tu ambazo zinatudhihirishia kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya Uislamu na Majini, Mashetani na mambo ya uchawi au ushirikina katika Uislamu.
Tutachambua mtazamo wa Quran kuhusu viumbe hao ikiwa ni pamoja na mashetani,malaika na majini.
Mtazamo wa Quran kuhusu Mashetani, Majini na Malaika
Waislamu wanaamini kuwa kuna viumbe walioumbwa na Mungu ambao hawaonekani kwa macho ya kibinadamu.Viumbe hawa wamegawanyika katika makundi makuu matatu.
1.Shetani
Shetani ambae hutambulika pia kama ibilisi(Iblis), ameitwa hivyo kwa sababu alilaaniwa na Allah kwa kukataa kumtii Allah alipoamriwa kumsujudia Adamu mara baada ya kuwa amemuumba (
Surat al-baqara 2;28-38 na al aaraf 7;10 na al khaf18:50).
Kutokana na laana hiyo,alipewa muda na Allah ili awapotosho watu. Alipewa ruhusa baada ya kuomba kufanya hivyo(
al-aaraf 7;16-17).Hata hivyo Allah alitoa into kwamba yeyote atakaye mfuata Shetani ataingia motoni. Hivyo kwa Waislamu, Shetani ni adui mkubwa na muamini humlaani kila Mwislamu anapotaka kufanya jambo lolote.Pia hujikinga na Shetani kwa kusali dua hii,
“aaudhubiiIlah mina shaytwaani rajiim,” yaani najikinga kwa Allah, na Shetani apigwae mawe.Shetani hupigwa mawe kwa kuwa Ibrahimu na mwanawe Ishmael walimpiga mawe punde alipotaka kuwadanganya wasiitii amri ya Allah ya kutaka kumtoa Ismail dhabihu.
Mashetani ni kundi kubwa sana na baba yao majini ni Shetani.Vitabu maarufu vya Kiislamu vinathibitisha jambo hili.Soma
(Itqaan fiy’uluwmi al-juzuu 4 uk 374,hadith 5,553).
2.Majini
Kumbuka Shetani alikuwa miongoni mwa Majini(
al-kahf 18;50),hivyo Shetani ni Jinni na Jinni ni Shetani.Quran inafundisha kuwa viumbe hawa waliumbwa kwa ndimi za moto(
al-Hijir 15;26-27,ar –Rahman 55:14-15). Wote wanafanana na Shetani kikazi na wote kazi zao zinafanana.Hivyo Majini yana nafasi kubwa sana katika Uislamu.Kujaribu kuwatenga Majini na Mashetani ni kiini macho tu, kwani Majini yalisilimu (
surat 72;1-14),ingawa kuna kundi lingine halikuslimu.Hata hivyo Allah aliwatumia wote katika kazi mbalimbali.Mfano kumsaidia Sulemani katika kazi zake mbalimbali za ujenzi,kumletea johari na vito vya thamani toka baharini,kumjengea nk.Soma (
Surat al anbiyaa 21;81-82).Allah alikuwa mlinzi,yaani msimamizi.Allah pia huwatumia Majini kufarikisha watu. Aliwatumia huko Babeli na kufundisha watu uchawi. Hawa mashetani huitwa
Haruta na Maruta.Soma (
al-Baqara 2;102). Aidha katika namna ya kushangaza,Allah alimletea kila Nabii maadui aliowatuma mwenyewe,yaani Majini na Mashetani (
surat al anam 6;112 na al-Hajj 22;52).Baadhi ya madhehebu kama Ahmadiyya walipogundua kuwa Majini ni Mashetani na Mashetani ni Majini,walianza kukataa dhana hii na Sheikh Farsiy,ambaye anawakanusha vikali. Waislamu wanatambua kuwa Majini ni ndugu zao na ndio maana moja ya mashart ya swala katika kumalizia kikao cha mwisho kiitwacho
(atahiyat), lazima kwa kila Muislamu asalimie pande zoote mbili yaani kwa kugeukia kushoto na kulia,kushoto ni kumsalimia Muislamu mwenzako na kulia ni kusalimia kundi kubwa la Majini ambayo hujumuika na Waislamu katika swala (
arshad-alMuslim).Hii ni lazima hata kama Mwislamu atakuwa peke yake wakati wa swala,kwani Majini hujumuika nae.Aidha Muhamad anasema, kila muislamu anapozaliwa anapata ulinzi toka kwa Majini na Mashetani (
soma al-muslim,Miskat). Majini yana ufahamu mkubwa sana wa Quran na Uislamu, yameslimu Muhamad alipokwenda kwa Majini na kuanza kuwauliza mambo ya uislamu.Majini yalijibu vizuri kuliko wanadamu soma (
surat al ahqaf 46;29-30).Soma pia ufafanuzi wa aya hiyo chini katika Quran ya Farsiy.Kwa ujumla hutakutana na jinni ambalo lina jina la Kikristo.Majini yote yana majina ya Kiislamu anaeleza Desmon Mkumbo, mmoja wa wataalamu wa huduma ya Biblia ni jibu Tanzania.Majini pia huhubiri Uislamu kwa nguvu na huhusika kusilimisha watu.Ikiwa pepo limekupagaa ukipelekwa kwa Sheikh au Maalim akusomee duwa, utapewa masharti ya kubadili dini,jina, kusilimu au kuswali.Haya ni maagizo ya Majini.Mwenye masikio na asikie!
3.
Malaika (malaikat)
Hili ni kundi la tatu katika imani ya Kiislamu kuhusu viumbe wasioonekana.Kumbuka Waislamu huamini Malaika na inasemekana kuwa Allah aliwaumba viumbe hao kwa nuru.Idadi yao Biblia inasema ni 10,000×10,000×1000×1000.Quran inasema haijui!Kazi yao kufuatana na Quran ni kumsifu Allah.Biblia inaongeza kuwa kazi yao pia ni kuwalinda Watakatifu na watakao rithi wokovu.
Wapo Malaika wa muhimu watano nao ni 1.Jibril:huyu ndiye Malaika mkuu.Allah humtuma kuwasiliana na manabii wake.Quran humuita Roho Mtakatifu (
surat an nahl 16:102). Ni Roho wa Mafunuo na Nguvu,Laylatul-Qadr (
surat al qadr 97;1-4).
2.Mikail:huyu yuko chini ya jibril
(al baqara 2;98).
3.Israfiil ni malaika anayeaminika sana,anasifika sana hatajwi katika Quran lakini anaaminika kuwa ndiye atakaye puliza parapanda siku ya mwisho.
4.Izrail: Pia hatajwi katika Quran,lakini anaaminika kuwa ndiye mtoa roho za watu (
al anam 6:61).
5.Hamalat al arsh:Hawa wako nane na inaaminiwa kuwa watabeba kiti cha Allah siku ya hukumu (
al- haqqah 69;17).
Waislamu huamini pia wako malaika wengine watano ambao hujulikana kwa kazi zao.Hao ni 1.Hafadhan:hulinda binadamu kutoka katika mikosi na balaa kwa mujibu wa Muhamad katika hadithi zake anadai wako kumi.
2:Katibun:hawa huandika habari za mtu.Wako wawili,mmoja huandika habari za matendo mabaya na mmoja mema.Wa mabaya hukaa kushoto,wa mema hukaa kulia.Kila mtu anao wawili (
az-zukhuf 43;80 na qaf 50;17-18).
3.Malik:Ni mlinzi wa moto wa Jehanam(
az-zukhuf 43;77).
4.Ridhiwan hulinda pepo (
paradiso).
5.Munkar na Nakir hawa ni wakali sana. Huuliza maswali kaburini.Mtu anaezikwa,huulizwa maswali juu ya Uislam.Hivyo Muislamu anapozikwa,Masheikh humfundisha namna ya kujibu maswali hayo, ili kumuepusha na adhabu ya malaika hao.Haieleweki jinsi mtu aliyekufa anavyoweza kufundishwa kujibu maswali.