Saa Za Gear: Samsung Imechanganyikiwa?

Saa Za Gear: Samsung Imechanganyikiwa?

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
Samsung katika medani ya simu na vifaa vyake (accesories) imekuwa ni kampuni ya kufuata na sio ya kugundua au kutangulia. Ila mwaka jana miongoni mwa kampuni kubwa, yaani kampuni kama vile Apple, Google na Microsoft, Samsung imekuwa ya kwanza kutoa saa ya smart. Mwaka jana nyakati kama hizi samsung walitoa Galaxy Gear, kiasi fulani ilitikisa soko na kutishia kuwa kivutio kikubwa, hata hivyo mambo kadhaa hayakwenda kama Samsung walivyotarajia. Sasa Samsung inaelekea kiasi fulani imechanganyikiwa, mwaka huu wanaelekea kuwa hawajui wateja wanataka nini, hawana uhakika saa za smart ziwe na muelekeo gani, lakini pia hawajui watarajie nini kutoka kwa wapinzani wao huku Apple bado wakiwa kimnya, Sony Smartwatch 2 imeshindwa kuwa tishio, Google wametangaza Android ya Smart watch huku ikiwa na taswira ya Google Now, Samsung iko njia panda ikiwa imechanganyikiwa kama tutakavyochambua.

Kutoa Saa Tatu Kwa Mpigo
Samsung katika kile kinachoonekana kucha
​
nganyikiwa wametoa saa tatu kwa wakati mmoja, Gear 2, Gear 2 Neo na Gear Fit. Si kawaida ya Samsung au kampuni yoyote kubwa kufanya hivyo. kwa mfano katika simu ambazo ni zenye kutarjia mauzo mazuri kama vile Simu za Familia ya Galaxy S na Simu za familia ya Galaxy Note kutolewa wakati mmoja, hili hawajawahi kulifanya kwenye simu, kwani kwa kufanya hivyo ni kama kuzishindanisha zenyewe kimauzo. Hii ni hoja ya awali ya kuchanganyikiwa kwa Samsung katika soko la Smart Watch.


Kubadili OS na Kuacha Kuita Galaxy
Wakati Galaxy Gear imetoka ikiwa inatumia Android, saa tatu za mwaka huu zote zinatumia OS ya Samsung ijulikanayo kama Tizen. Hii maana yake ni kuwa, mosi; watumiaji wa Galaxy Gear wasitarajie kuendelezwa kwa saa hiyo kwa upande wa matoleo mapya ya Software na apps mpya, hivyo Samsung imewaangusha wale waliolipa karibu Shilingi 800,000.00 kununua saa hiyo hapo ilipotoka (kwa bei ya UK £300.00), pili Imewaangusha wale walioanza kutengeneza Apps za Galaxy Gear ambao walitaraji matoleo yatakayofuata ya saa hizo yataendelea kutumia OS hiyo, tatu; Imewaacha wateja wakiwa hawana uhakika kwa vile Tizen ni OS mpya mno na isiyotumika na kampuni nyingine yoyote lakini zaidi Google imeshatangaza Android ya saa. Hivyo kuna uwezekano mkubwa Samsung mwakani ikarudi kwenye Android.


Vile vile kwa Samsung baada ya kuacha kutumia Android wamelezimika kuliondoa jina (brand) la Galaxy, kwa vile jina hili ni maalum kwa gajeti za Samsung zinazotumia Android kama ilivyo jina la Ativ na Windows. Hivyo Gear zote tatu za mwaka huu hazina neno Galaxy katika jina.


Kamera Katika Saa
​
Gear ni saa ambazo huziwezi kuwa Smart kama hutakuwa na simu inayokubaliana nayo. Baada ya kutumia Galaxy Gear uzoefu wetu umeonyesha kuwa saa haihitaji kamera, siku kadhaa za mwanzo tulijaribu kuitumia kamera ya Galaxy Gear na baadae tukagundua kuwa si jambo lenye faida yoyote kwa sababu:
- Simu ina kamera nzuri kuliko kamera ya Galaxy Gear ambayo ina megapikseli mbili tu. Hivyo hakuna ambaye atatumia kamera ya hali ya chini na awache iliyobora.


- Huhitaji kuwa na kamera zaidi ya moja kwa wakati mmoja kwa vile tayari simu ina kamera na gajeti mbili hizi zinafanya kazi sambamba kwa maana ya kwamba wakati wowote utakapokuwa na saa na simu ni pacha wake.


- Utakapopiga picha inaletwa kwenye simu, sasa kwa nini usitumie tu kamera nzuri ya simu badala ya saa ambayo hata unapokuwa unataka kupiga picha nzuri ni kazi kuitumia kwa viel tayari saa umeshaivaa, kuitumia kidogo inakuwa shida.


Bila ya shaka Samsung hili wamelihisi, katika kuchanganyikiwa kwao ndio wameishia kutuoa Saa mbili zilizo karibu sawa tofauti ikiwa moja ina kamera na nyingine haina, yaani Gear 2 na Gear 2 Neo. Sisi tunaimani hakukuwa na sababu ya kuwepo kwa kamera kwenye saa hizi, kwa vile kimsingi kamera hii haina kazi yoyote, haifai kuchati wala si nzuri kwa picha, na video zake ni sekunde chache tu.


Apps
Wakati Galaxy Gear ilishaanza kuwa na apps kubadili kwa OS kuifanya Samsung ianze upya katika apps za gajeti hizi, lakini sio tu kuanza upya Samsung wameshatoa SDK ya Tizen kwa ajili ya watengeneza apps, pia Samsung imetangaza mashindano na kutenga UD$ milioni nne kwa washindi 64 watakaotengeza Tizen apps zinazotumia HTML 5. Lakini swali la msingi ni; kwa nini Samsung waanze upya mara mbili? Huku ndio kuchanganyikiwa tunakokuzungumzia.


Kazi za Saa
Kuchaganyikiwa kwengine kwa Samsung kumejitokeza kwenye kazi za saa hizi. Wakati Gear Fit ni fitness band, ina kazi kadhaa za smart watch, na wakati Gear 2 na Gear 2 Neo ni Smart Watch zina kazi zote za Fitness band. Hivyo kwa nini Samsung wanatuambia moja ni kwa ajili ya mazoezi na nyingine ni smart watch wakati zote tatu zina sifa za pande zote. Kwa mfano Gear Fit ina notifications, media control, timer, stop watch, hali ya hewa, find my gear na kalenda. hizi zote ni kazi za smartwatch, na kwa upande mwengine, Gear 2 na Gear 2 Neo zina Kipima mapigo ya moyo, , kutoaripoti za mazoezi ya aina mbali mbali kama vile kukimbia na kuendesha baskeli na pia zina pedometer, ambapo hizi ni kazi za fitness band. Ni wazi Samsung hawana uhakika wateja wanataka nini.


Ni ipi Kinara?
​
Swali la kujiuliza ni kuwa katika Gear tatu hizi za mwaka huu ipi ni kinara (flagship), ukiangalia bei na utendaji wa kazi jibu ni Gear 2, hii ndio ghali kuliko zote lakini pia ina mambo mengi kuliko zote ikiwa imeizidi Gear 2 Neo kwa kuwa na Kamera na pia imeizidi Gear Fit kwa kuwa ina uwezo wa kupokea simu. Hata hivyo wachambuzi wengi wa gajeti wamevutiwa na Gear Fit kimaumbile, Gear Fit ina kioo aina ya Super Amoled kilichopinda kufuata mzunguko wa mkono (curved), hivyo inapendendeza kuliko Gear 2 na Gear Neo zenye maumbile ya mraba. Kimaumbile (form factor) Gear Fit inavutia zaidi. Hivyo Samsung wamepoteza nafasi nzuri ya kuitengeneza kinara ya saa tatu hizi katika umbile lenye kuvutia.


Smartwatch au Fitness Band?
Sisi katika Gajetek tumekuwa tukijiuliza ni kifaa kipi kati ya hivi ndio ni bora zaidi kukivaa, jibu hutegemea kama wewe ni mtu wa mazoezi au la. Smart watch ni marejeo ya kazi za simu kwenye saa, hivyo kiuhakika ni suala la kujifurahisha zaidi kuliko kuwa na kifaa kinachofanya kazi za ziada. Lakini Fitness Band ni muhimu kwani si rahisi kuwa na simu mfukoni wakati unacheza mpira wa kikapu au kandanda hivyo smart watch ina kazi za ziada ambazo huwezi kuzifanya kwa simu hasa unapokuwa mazoezini.


Ipi Zaidi kati ya Gear tatu hizi?
Sisi katika Gajetek tumechagua Gear Fit kuwa ni saa bora zaidi kuliko Gear 2 Neo na Gear 2. Sababu zikiwa ni;

  • Maumbile ya kupendeza ikiwa na curved display

  • Bei ni nafuu

  • Ina skrini kubwa zaidi kuliko zote (1.84") GEar 2 na Gear 2 Neo zina 1.63"

  • Ni nyepesi zaidi ikiwa na gramu 27, Gear 2 ina gramu 68 na Neo ina gramu 55.

  • Unaweza kubadili mikanda ya rangi mbali mbali.

  • Betri yake hudumu hadi siku nne, Gear 2 na Gear 2 Neo ni siku tatu.

Usikose makala zijazo ambapo hivi karibuni tutaichambua kwa kina Gear Fit na kazi zake na hasa za kiafya kama vile kipima mapigo ya moyo, ubora wa usingizi, mazoezi mbali mbali na jinsi inavyofanya kazi pamoja na Samsung Galaxy S5.
​

Chanzo: gajetek habari
 
Back
Top Bottom