RwandAir Bankrupting Rwanda

Kenya

South Africa

Mozambique

Egypt
 
Katika mambo ambayo nimeshindwa kabisa kumwelewa Rais Magufuli ni kuamua kupeleka hela yetu yote, ambayo ni kidogo na inapatikana kwa shida, kwenye miradi ambayo ni ya hasara au faida yake ni ya muda mrefu sana.

Ndege
Mataifa ambayo yana opportunities nyingine zenye uwezo wa kuwaletea faida, hayapotezi kuwekeza kwenye usafiri wa anga. Nchi kama Rwanda, Burundi, Holland, Ethiopia, UAE (Dubai) wana sababu za msingi kuwekeza sana kwenye usafiri wa anga. Mataifa haya yana upungufu wa vivutio asilia vya utalii, maeneo madogo ya ardhi, hawana madini, wala mafuta wala gas (Dubai wanayo kiasi lakini siyo kiasi kikubwa). Sisi tumekosa nini mpaka tuone kuwa usafiri wa anga utatupatia faida kubwa ukilinganisha na fursa nyingi ambazo Taifa linazo? Mwerevu siku zote, ukitaka kumshinda mpinzani wako ni lazima utazame uwezo ulio nao ambao mshindani wako hana. You compete using your strengths and not your weaknesses.

Rais Magufuli, unaweza kudharau ushauri wa kila mtu lakini kuwekeza heavily kwenye usafiri wa anga, siyo uamuzi sahihi. Kama hutaelewa leo, kuna siku utaelewa na nafsi yako itaumia maisha yako yote kwa kuwafukarisha Watanzania kupitia maamuzi mabaya ya uwekezaji.

Umeme
Umeme ni nishati muhimu lakini ni ukweli kuwa TANESCO haijawahi kutengeneza faida hata mwaka mmoja. TANESCO inastahili kuendeshwa kwa ubia na sekta binafsi ili kuiondoa kwenye uendeshaji wa kisiasa ambao haujawahi kutupatia tija yoyote. Lakini kwa nini twende kwenye umeme wa maji wakati ambao mataifa mengi Duniani yanaondoka huko? Kwa nini jitihada za umeme wa gas zilizokuwa zikiendelea zimetupwa tu na halafu tunakwenda kwenye mradi mpya? Nalo hili kwa wakati huu haukuwa uamuzi sahihi.

Reli
Tunahitaji sana usafiri wa reli lakini siyo kila usafiri wa reli una faida kwa Taifa na kwa wananchi. Mradi wa reli ulitakiwa kuwekewa mazingira ya kuiwezesha sekta binafsi kuwekeza huko kwa kushirikiana na serikali. Serikali haijawahi kufanikiwa kuendesha mradi wowote wa biashara kwa mafanikio. Uamuzi wa kujenga reli mpaka Dodoma, nao ni kosa kubwa. Usafiri wa reli faida yake hutokana na usafirishaji wa mizigo, Dodoma kuna mizigo gani ya kuchukua na kupeleka? Ubuyu? Tulitakiwa kuwekeza kwenye miradi yenye faida kubwa ili baadaye tuwe na uwezo wa kuwekeza kwenye miradi yenye faida ndogo. Mtu mwerevu maskini hakopi gari ya kutembelea kwenda shambani bali atakopa tractor azalishe mazao na baadaye ndiyo afikirie gari la kutembelea, kuliko kukazania kusema kuwa ni muhimu sana kuwa na gari kwa sababu litakufikisha shambani na baadaye litasaidia kubeba mazao (ambayo hayapo).
 
I was Fortunate kupanda Rwandair, wana service nzuri sana, kuanzia hostesses hadi Airport yao.

Kwa mawazo yangu Rwanda wangetafuta partnership na Airline flani hivi kubwa kama Turkish, British Airways etc. If Possible angetumia Dar Es Salaam au Zanzibar as Hub yake kwa Sababu ya Geography.
 
acheniuongo bana
yaani kama wao wanapata hasara haimaanishi na sisi tutapata hasara.
sisi tukiland kila mkoa tu, tayari tunakuwa na destinations nyingi kuliko rwanda 🙄😵🙄😵
 
Na treni ya SGR ikianza kufanya kazi huyu jamaa atakuja na kiingereza gani kingine?
 
 
Nyinyi muna wivu tu, si lazima shirika la serikali lipate faida cha msingi ni Huduma nzuri za kizalendo.
Uzalendo wa kuzamisha pesa za walipa kodi into a non profit organization ni uzalendo wa kipumbavu.
 
Unahitaji kuifahamu biashara ya aviation ilivyo
Impact ya hiyo biashara inaonekana indirectly ndio maana licha ya mashirika mengi kuwa yanapata hasara lakini nchi zinaendelea kuzi-support
Endeleeni ku-justify maamuzi ya kijinga huku mkifahamu fika kwamba hospitali hazina madaktari wa kutosha wala dawa, mashule hayana walimu wa kutosha wala vitendea kazi, maji safi na salama bado ni changamoto kuu vijijini na matatizo mengine lukuki....

Mbaya zaidi, hapo hata nikikuambia taja hizo indirect benefits ambazo ni zaidi ya hayo niliyotaja hapo juu sidhani kama utaeleza!
 
mod msiunganishe uzi huu umekuja kwa ajili ya audience ya watumia kiswahili japo mbele imeenda kwenye 'kisungu'

turudi kwenye mada.


serikali imetoa tamko gani mpaka sasa? je halifanani na lile la serikali yetu lisemalo 'huwezi nunua ndege leo kesho uanze kutengeneza faida'

ili litimie andiko lisemalo ndege wafananao huruka pamoja?
 
Wewe ushaambiwa tunaboresha safari za anga ili kuongeza watalii mbugani mwetu..sasa hayo mashirika yanayoendeshwa kwa hasara?...yanavivutio vya utalii kama tz?
 
Tumetupiwa chambo.
Huu sijui uzi wa ngapi kuhusu story moja tu.

Shilingi ina pande mbili. Hili laweza kuwa kweli au uongo. Uongo kwa maana ya kutengenezwa ili Tanzania na Uganda tusiwe na Airlines na RwandAir ipanuke zaidi kuhudumia nchi zetu. Akili za Kagame, anazijua mwenyewe.

Hawezi kushindana na KQ au Ethiopian. Karata yake yaweza kuwa hiyo. Kama Tanzania na Uganda zikiwa na mashirika yake imara, RwandAir haina chembe ya nafasi.
 
Huyu Himbara alieleta huo uchambuzi sio wa kumuamini kirahirahisi. I personally know the guy.

Tukuamini wewe muandika threads huku mavumbini JF?

Yeye kawa presidential economist wa rais wa rwanda tangu 2003-2004 na 2006-2010..Mchumi mkuu wa bwana Slim!

Kaiset rwanda unayoiona leo...anajua more than anybody kuhusu uchumi wa rwanda even more than mr slim himself!

Hawakuelewana 2010 akaondoka...sio tatizo...anachokisema tunaweza kiamini zaidi ya utakachosema wewe au even slim!

Acheni kum discredit mtu akiwa critique...toeni hoja!

He is a leading rwandan economist ever...acheni mbwembwe,jibuni hoja bana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…