Rwanda yapiga marufuku Galaxy Note 7

Rwanda yapiga marufuku Galaxy Note 7

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
Serikali ya Rwanda imepiga marufuku uagizaji na usambazaji wa simu za kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7.
Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya kampuni hiyo ya Korea Kusini kutangaza kwamba ingesitisha uundaji na uuzaji wa simu hizo kutokana na kuongezeka kwa visa vya simu hizo kushika moto au kulipuka.

Mamlaka inayosimamia bidhaa na matumizi nchini Rwanda imesema hatua ya kupiga marufuku simu hizo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

"Kwa sababu za kiusalama, wateja ambao huenda walinunua simu hizi binafsi nje ya nchi wanatakiwa kuzizima na kuzirejesha eneo walizozinunua," imesema taarifa ya kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Meja Jenerali Patrick Nyirishema.

Chanzo: BBC
 
Kuna nchi nyingine kuandaa mazingira ya usalama kwenye matumizi ya bidhaa kwa raia wake haziwezi basi hata kuiga kwa jirani zao washindwe.
 
Back
Top Bottom