Rwanda yapiga marufuku adhana na miziki makanisani

mie huwa nakereheka sana natamani yesu arudi hapa mtaani kwangu ikifika saa 11 asubuhi utasikia mapambio na usingizi wote kuisha
mie nadhani labda huwa kuna uhuru wa dini ndo maana watu wanaamua kupiga makelele kama si sheria kwa nini hakuna nayefungua mdomo na kuwaambia??
Naona ndugu yangu uko "biaz" na adhana pekee, hauangalii mahubiri na mikesha ya kilokole hasa TAG. Wewe kumuunga mkono kagame ni sawa, kwa sababu ndio upeo wako wa mambo ya kijamii unapoishia. Remember once you are living within the intermingled community you have to sucrifice some of your intersts, (ikiwemo usingizi wako wa asubuhi). Our country, Tz both Muslims and Christians are equally balanced to freedom of worship. None of either religion's interest can be outweighed from onother. if you don't believe it try a bit UONE.
Haruna
 
Kiufupi Kagame amechemka. Tanzania tumeendelea kubakia hivi tulivo bila ya kuchapana kidini ni kwa sababu tuna religious tolerance kubwa sana. Nakumbuka mwaka 98 wakati waisilamu wanapambana na serikali pale mwembechai kwa sababu za mihadhara, hakuna kanisa hata moja kati ya matatu yaliyopo pale m'chai lililotupiwa hata jiwe. siku zote mambo ya Imani si ya kuyachezea. tujiulize hao jamaa wa misikitini wanapotoa azana zao wanakusudia nini? ama mziki wa kanisani kazi yake ni nini? pia huyo kiongozi alosema atasambaza redio kwa waisilamu wote ili wapate azana ni kuchemka. kwani hio si sustainable hata kidogo. na pia mafundisho sidhani kama yanasema hivyo. na zaidi huo ni uoga wa kumuogopa kagame. kweli kabisa ipo siku atawaambia hakuna kuabudu madhabahuni na wao watawaambia watu wakae na kuabudu majumbani kwao. je kuna ishu za miziki katika mabaa nao vipi? hao wanaosema wanapata kero za kelele hizo mbona hwazisemi. Kagame aambiwe aache chokochoko nyingine. ukabila wanakaribia kuumaliza. sasa anagusa dini. ajue tu kuwa watu wanaamini ukiuwawa kwa sababu ya dini utauona ufalme wa milele. na kila mtu anautaka huo ufalme wa milele. na pia watu huwa wanakufa mara moja tu. na pia hakuna anayekufa sana na anayekufa kidogo.
Fikiri kabla hujaandika, acha udini wewe! kutokana na kuwa na viongozi kama wewe ndo maana amri hazitekelezwi!
 
Jenerali Kagame ndie aina ya kiongozi anayehitajika hapa kwetu.......sheria ziko wazi kuhusu uchafuzi wa mazingira ikiwa inahusisha na kelele za mihadhara na usumbufu kwa raia...lakini kuna serikali na hakuna chochote kinachukuliwa dhidi ya uvunjifu huu wa sheria,msikiti wa mtambani ni moja ya nyumba za ibada ambazo zinaongoza kwa kelele na mihadhara inayoeneza chuki kati ya raia....serikali imekaa kimyaaa na inasubiri siku itokee fujo ndipo iunde tume ya kuchunguza kiini cha tatizo....hii ndio tanzania......bila kuwa na viongozi mfano wa kagame sioni kasi ya maendeleo kama tunavyolazimishwa tuamini na wahusika

Ngwilizi aliwahi kung'oa vipaza sauti misikitini, alivyokuwa RC mwaka 1996
 
Naona ndugu yangu uko "biaz" na adhana pekee, hauangalii mahubiri na mikesha ya kilokole hasa TAG. Wewe kumuunga mkono kagame ni sawa, kwa sababu ndio upeo wako wa mambo ya kijamii unapoishia. Remember once you are living within the intermingled community you have to sucrifice some of your intersts, (ikiwemo usingizi wako wa asubuhi). Our country, Tz both Muslims and Christians are equally balanced to freedom of worship. None of either religion's interest can be outweighed from onother. if you don't believe it try a bit UONE.
Haruna

Kuweni na kiasi
kuna wengine tuna usingizi wa kulenga na manati so ukiudisturb kidogo ndo uamke ukaanze kucheza mziki ama uendelee na wewe kuimba mapambio :)
 
msishangae jamani kwa mfano hapa kwetu kungekuwa na amri za dizaini hiyo watu tungenyooka kwani kuna makanisa katikati ya watu tena baada ya hatua 5 kuna kanisa ndani ya maeeneo ya watu tena dirishani wakianza kukesha kwa mapambio hulalli. shei ziko wazi hapa kwetu ila watu ni wagumu tu na upendo umezidi
 
Tanzania tunaigiza sana na kupenda kuonekana nice guys, lakini wakati mwingine tunalazimika kuchua maamuzi magumu bila kujali nani ataguswa. Ibada zinanoga zaidi kwa vipaza sauti jamani na sauti kubwa? manake hata sauti zikiwa kubwa kiasi gani bado waumini ni wale wale na sauti zikitoka hakuna anayesikiliza. Wauza cassette kariakoo kila mtu katoa speaker kubwa nje na kila mtu anapiga mziki wake sasa mteja anasikiliza upi?

Wakati unabadilika na dini zinatakiwa pia kwenda na wakati uhsusani katika kutumia teknolijia ya kuwasiliana na waumini kung'ang'ania misimamo na uzoefu bado hakutasaidia sababu wakati dini zinaanza hakukuwa na hizo speaker wala ala hizi za miziki.
 
msishangae jamani kwa mfano hapa kwetu kungekuwa na amri za dizaini hiyo watu tungenyooka kwani kuna makanisa katikati ya watu tena baada ya hatua 5 kuna kanisa ndani ya maeeneo ya watu tena dirishani wakianza kukesha kwa mapambio hulalli. shei ziko wazi hapa kwetu ila watu ni wagumu tu na upendo umezidi

:) upendo umezidi tena
 
Sheria hii ingefaa sana hapa tanzania kupunguza makelele mitaani. nyingine zinazidi hadi hospitalini
 
Serikali ya Rwanda inatofautiana sana na serikali nyingine za Afrika Mashariki katika kusimamia maagizo yake, ikipiga marufuku manake ni marufuku kweli hakuna compromise wala kuandamana ni utekelezaji tu na atakae kaidi hatua kali za kisheria zinachukuliwa. Kwa mfano mifuko ya nylon(rambo) na jamii yake maruku Rwanda maana yake hutaona mfuko huo kigali ukikutwa nao lupango tu.

this is what i call readership...! u stick to the laws and decrees whatever it is..!

i wish kagame angekuwa rais wetu..! ile amri ya kupiga marufuku mifuko ya nylon (vi-kondom) bongo iliishia wapi..? polisi wanafanya nn..? hawa ndo watekelezaji wa amri za serikali...! kwa sasa mifuko hii ipo kila mahara..! wakati bunge lilipitisha sheria ya kuipiga marufuku.!
icon8.gif
kiwanda kinachotengeza kinafahamika.....! why....! kwa kifupi hatuna serikali inchi hii...!

ngoja niishie hapa nisije nikatukana kwa hasira..!
 
Sheria hii ingefaa sana hapa tanzania kupunguza makelele mitaani. nyingine zinazidi hadi hospitalini

Hivi na nyinyi mna nyumba gani ambazo makelele ya nje yanaishia ndani? acheni kulaumu waumini jengeni nyumba bora ili muepuke kelele za mitaani, na pia mtusaidie na sisi na makelele yenu huko vyumbani yanatupa wakati mguu tunapopita karibu na madirisha yenu na watoto wetu....utasikia baba mbona mama nanii analia?
 
Me ninafikiri wenye mawazo potofu kama hawa banyamulenge basi nao hawamie huko Rwanda ili wakauwane vizuri...
 
..Raisi Bagaza wa Burundi aliwahi kutoa amri kama hii ya Kagame.

..Fidel Castro naye alipiga marufuku shughuli za kidini[kanisa katoliki] na kuamuru Krismas kuwa siku ya kazi.
 
Rwanda inabidi ivamiwe kijeshi haraka iwezekanavyo. Mujahidina na macrusaders nendeni mkabidlishe utawala haraka sana. Hii ni breaking news.
 
Hizi sheria hata TZ zipo ila hazifuatiliwi tuu,ni sheria za miji mingi ili kuzuia usumbufu kwa wakazi wake,hebu imagine umelala then walokole na mikesha yao na ngoma za mapambio mpaka asubuhi? hapo ustaarabu uko wapi?na watu msilete hoja ya uislam VS Ukristu maana hakuna hapo...swala ni makelele tuu na ndio maana kuna hata sheria za ujenzi na miji ambazo kanisa au nyumba za ibada lazima ziwe umbali fulani toka makazi ya watu na sababu kubwa ni huu usumbufu,angalia bongo bar za wazi na spika ziko nje muziki full blast mpaka mtaa wa pili ukilalamika wanakushangaa na wananchi wanaona sawa tuu na ni kwa sababu hawajui haki zao,halafu hii tabia ya kufikiri kila amri ni lazima atoe Raisi ni ya bongo,hizi sheria ni za miji na wala Kagame hahusiki na zilikuwepo tangu zamani...yaani hii tabia ya kusubiri hata makelele ya mitaani kwetu aje JK ndio umaskini wa mawazo!
 
Mkuu sijakupata vizuri hapo kwenye nyekundu...unasema waisilamu walipambana na serikali then hapo Ishu ya kanisa kutupiwa mawe unakujaje kwani Serikali ndo kanisa?
ishu si kuihusianisha serikali na kanisa...my point ni kuonyesha religious tolerance hata katka jambo ambalo chanzo chake ni tofauti ya dini mbili...
 
Sasa nani atafuatia EA kupiga marufuku kuamshana asubuhi?

Kwa walio nje ya Tz,scandinavia,us,kwa bibi (UK) hakuna kitu kama kuadhini lakini kengele kama kawa.

Hivi Masaki na Osterbay na maeneo ya Ocean Road kuna misikiti?

Ningefurahi sana pale kwetu Manzese kwa Mtogole wangengóa vipaza sauti,manake ukilala mida ya saa kumi na Hangover,11 asubuhi masela washakuamsha na adhana.

Mawazo tu jamani.
 
..wengine ambao tunaishi karibu na misikiti na makanisa adhana na kengele ndiyo alarm clocks zetu za kutuamsha asubuhi.

..inawezekana Kagame kajipatia tenda ya kuagiza alarm clocks Rwanda, sasa hapo anajaribu kuondoa upinzani ktk soko/biashara.
 
Hii sheria inafaa sana Tanzania.Wakati mwingine unavuta usingizi mtamu unasikia kelele za maspika ya msikitini zinakatiza usingizi wako.Kwani mtume alikuwa anatumia maspika kuamusha watu kwenda kuswali.
 
mnajua maana ya religion tolerance, tusimsupport tu kagame tu, maeneo kama SA mbona kanisa na miskiti wanaendeleza mambo yao kama kawaida....sheria hiyo haifai TZ kwani sisi ni watu wa kupendana na umoja popote pale unapo mkuta m tZ hasa nje ya nchi na wenzake utaligundua hilo
 
Back
Top Bottom