Rwanda yapiga marufuku adhana na miziki makanisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rwanda yapiga marufuku adhana na miziki makanisani

Discussion in 'International Forum' started by Songambele, Sep 28, 2009.

 1. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Rwanda imepiga marufuku sauti kama zilivyoitwa makelele yanayotoka katika nyumba za ibada kwa madai ya kuleta bugudha kwa wasiohusika na ibada hizo. Marufuku hiyo inahusu adhana kutoka katika misikiti yote na midundo ya miziki kutoka katika makanisa mbali mbali na mahubiri kupitia vipaza sauti. Nukuu kutoka BBC asubuhi leo.

  Waumini wameshaanza kuchukua hatua ya kupambana na amri hiyo kali ya serikali, kwa waislamu wameahidi kutumia radio kwa ajili ya adhana na kuhakikisha kila muumini anakuwa na Radio ili kupata taarifa za ibada na mahubiri.

  Serikali ya Rwanda inatofautiana sana na serikali nyingine za Afrika Mashariki katika kusimamia maagizo yake, ikipiga marufuku manake ni marufuku kweli hakuna compromise wala kuandamana ni utekelezaji tu na atakae kaidi hatua kali za kisheria zinachukuliwa. Kwa mfano mifuko ya nylon(rambo) na jamii yake maruku Rwanda maana yake hutaona mfuko huo kigali ukikutwa nao lupango tu.

  Kama ilivyo ada baadhi ya waumini hawajakubaliana na marufuku hiyo lakini hakuna namna nyingine ya wananchi kupinga kama ambavyo ingetokea Tz au Kenya watu wangepinga, wanaharakati wangetoka lakini wanaharakati hakuna Rwanda na waliokuwepo ni kuunga mkono mamlaka.
   
 2. Kaka Mkubwa

  Kaka Mkubwa Senior Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duuh!!!!!!!!!!
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  aaah mbona hii ni kuwanyima watu uhuru wa kidini ?
   
 4. J

  JituParaTupu Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sheria hii ingefaa sana hapa TZ kupunguza makelele mitaani.
   
 5. M

  Mamiso New Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 21, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Jenerali Kagame ndie aina ya kiongozi anayehitajika hapa kwetu.......sheria ziko wazi kuhusu uchafuzi wa mazingira ikiwa inahusisha na kelele za mihadhara na usumbufu kwa raia...lakini kuna serikali na hakuna chochote kinachukuliwa dhidi ya uvunjifu huu wa sheria,msikiti wa mtambani ni moja ya nyumba za ibada ambazo zinaongoza kwa kelele na mihadhara inayoeneza chuki kati ya raia....serikali imekaa kimyaaa na inasubiri siku itokee fujo ndipo iunde tume ya kuchunguza kiini cha tatizo....hii ndio tanzania......bila kuwa na viongozi mfano wa kagame sioni kasi ya maendeleo kama tunavyolazimishwa tuamini na wahusika
   
 6. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wamelogwa!!!!!!!!!! Wameanza kurudi walikotoka kwa staili nyingine
   
 7. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  hao wanyarwanda wanaumwa ugonjwa wa akili, wataalamu wa afya ya akili wanauita post combat symptons, ni wehu na wehu mtupu.
   
 8. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Vp na kwa hao ambao huo uhuru umekua kero kwao? Ifike wakati tuwe na mustakabali mzuri sio kulaamu tuu...we hayo makanisa na misikiti inavyochipuka kwenye makazi ya watu unadhani bila hizi sheria mabo yatakwenda? Usione Tz kwamba wapo kimya kuna watu wanakerekwa ila tu wamekosa pa kusemea.
   
 9. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Du ndugu yangu hapa nadhani unahitaji kuelimishwa tu, huo uchafuzi wa mazingira kwa sauti/kelele ni lazima viwango fulani vifikiwe ndio uchafuzi huo utimie, na kwa sauti za makanisa na misikiti nyingi hazifiki huko. Kwa karne hii kiongozi wa kuigwa si yule mbabe bali anayetawala kwa misingi ya kidemokrasia, hapa inamaanisha uhuru wa kuabudu pia. Kwa kigezo hicho tu Tanzania haipaswi kuiga kutoka kwa Kagame ila Kagame anapaswa kuja kujifunza hapa ni kwa jinsi gani raia wenye dini mbalimbali wamepewa fursa ya kuabudu na uhuru wao unalindwa katika katiba ya nchi(tazama ibara ya 19 katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2006.) Huo usumbufu kwa raia una maanisha raia gani tena ambao si waumini? unajua kwa sasa watu wasio waislamu wala wakristo ni chini ya asilimia 2 tu? tena wengi wa hao wanafuata imani nyingine na za kiyahudi, kibudha n.k ambazo zinasitiza umuhimu wa uhuru watu kuabudu.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280

  mie huwa nakereheka sana natamani yesu arudi hapa mtaani kwangu ikifika saa 11 asubuhi utasikia mapambio na usingizi wote kuisha
  mie nadhani labda huwa kuna uhuru wa dini ndo maana watu wanaamua kupiga makelele kama si sheria kwa nini hakuna nayefungua mdomo na kuwaambia??
   
 11. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Amri sawa. Lakini naomba aliye Rwanda anielemishe. Je, kengele za makanisani (hasa Kanisa Katoliki) pia zimepigwa marufuku? Je, miziki kwenye mabaa? Kelele nyingi za matangazo kama zilivyo Kariakoo (Dar es Salaam) kutwa nzima (zile za wauza vyandarua, muziki, chama cha Abiria, wauza madera). Sasa hivi niandikavyo kuna tamasha kubwa tu la Nokia pale soko Suu la Kariakoo (Dar) . Je, wamepiga marufuku aina hizo za kelele? Kama ndivyo, wanastahili pongezi.
   
 12. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Usijali Yesu yu karibu kuja ndo dalili zenyewe.. cha muhimu ni kua na uhakika kama tutakua wote kunako pepo...Jiandae mamie tusije kukuacha!
   
 13. M

  Muuza Maandazi Member

  #13
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kiufupi Kagame amechemka. Tanzania tumeendelea kubakia hivi tulivo bila ya kuchapana kidini ni kwa sababu tuna religious tolerance kubwa sana. Nakumbuka mwaka 98 wakati waisilamu wanapambana na serikali pale mwembechai kwa sababu za mihadhara, hakuna kanisa hata moja kati ya matatu yaliyopo pale m'chai lililotupiwa hata jiwe. siku zote mambo ya Imani si ya kuyachezea. tujiulize hao jamaa wa misikitini wanapotoa azana zao wanakusudia nini? ama mziki wa kanisani kazi yake ni nini? pia huyo kiongozi alosema atasambaza redio kwa waisilamu wote ili wapate azana ni kuchemka. kwani hio si sustainable hata kidogo. na pia mafundisho sidhani kama yanasema hivyo. na zaidi huo ni uoga wa kumuogopa kagame. kweli kabisa ipo siku atawaambia hakuna kuabudu madhabahuni na wao watawaambia watu wakae na kuabudu majumbani kwao. je kuna ishu za miziki katika mabaa nao vipi? hao wanaosema wanapata kero za kelele hizo mbona hwazisemi. Kagame aambiwe aache chokochoko nyingine. ukabila wanakaribia kuumaliza. sasa anagusa dini. ajue tu kuwa watu wanaamini ukiuwawa kwa sababu ya dini utauona ufalme wa milele. na kila mtu anautaka huo ufalme wa milele. na pia watu huwa wanakufa mara moja tu. na pia hakuna anayekufa sana na anayekufa kidogo.
   
 14. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #14
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi dini nchini Rwanda ilianza baada ya Kagame kuchukua uraisi au? Ndio maana ninawasiwasi sana na maraisi ambao shule zao hazieleweki zaidi ya uaskari tu. Amri unaileta katika dini? Amri karne hii? Tunaongelea kukuza demokrasia wewe unaleta amri mpaka kwenye vitu nyeti ambavyo vinahitaji dialogue na participatory approach ya hali ya juu namna hiyo? Acheni kusifia vitu ambavyo mwisho wake ni maafa tu. Kwa mtaji huo hatafika pahala popote. Dini ina nafasi yake katika uongozi,tusifanye mchezo na kufikiri binadam anajua kila kitu na kwa utashi wa binadam eti kila kitu kitaenda sawa. Wrong approach. Mara nyingi jamaa hua anashauriwa na mkewe,ila ktk ili either amekurupuka bila kumshirikisha au wote wamechemka naturally. Let's wait and see!!
   
 15. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiyo siyo kunyima uhuru hiyo ni kupunguza matatizo ya kiafya kelele zina madhara,mi ningeomba hizo amri zije tz kuna kanisa moja hapa mikocheni hatulali haswa siku ya mkesha wa ijimaa kuamkia jumamosi hatulali,
  Hivi ni lazima kufunga speaker nje? kwanii ni lazima uwaite waumini? kwani hawajui wajibu wao wa kumuomba mungu wao? na suala la amri kutekelezwa hapa kwetu zinashindikana kwakuwa wote wameingia madarakani kwa njia zisizo halali na hajui kwa nini yupo madarakani (nchi ina didimia na viongozi wapo) vidagaa machinga wamewashindwa! ndo watawaweza hawa wa dini,mifuko ya rambo(ptastic bag) na mapapa wengine?
  Viongozi muwe na uso wa aibu kidogo mji umekua mchafu kila mahala ni soko, daladala kila pahali ni stand wanapakia tu,kila junction ni vijiwe vya vijana, maskini nchi yangu!
   
 16. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera kagame kusumbua watu wengine na mikelele ndo kukuza demokrasia? hivi nini maana ya demokrasia
   
 17. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kule nishawahi kwenda hakuna kengele wala cha nini kule amri ni amri ukiambiwa usitupe taka ovyo ni usitupe kweli ukikutwa ni ndani hakuna cha ushaidi hajatosheleza kama kina ZOMBERI ni ndani tu upo hapo, Hongera kagame
   
 18. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja ya Kagame mia kwa mia, ila nachoomba JK naye a copy kidogo tu hata kwa maduka ya kuuza CD na kanda maana yanaboa na miziki yao.

  Big up Kagame, kwani kuwapa watu uhuru mkubwa kiasi hicho kama ilivyo hapa kwetu TZ kisha watu hawajui namna ya kuutumia uhuru huo ni balaa.

  Angalia mazingira yetu yanavyochafuliwa na mifuko ya Rambo, kisa uhuru, uhuru una mipaka yake, na ni lazima pia yawepo mazingira ya huo uhuru kutekelezeka.
   
 19. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama mimi nakerwa haswa tena haswa
   
 20. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu sijakupata vizuri hapo kwenye nyekundu...unasema waisilamu walipambana na serikali then hapo Ishu ya kanisa kutupiwa mawe unakujaje kwani Serikali ndo kanisa?
   
Loading...