Rwanda yamjibu Rais Kikwete

Rwanda yamjibu Rais Kikwete

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Dar. Serikali ya Rwanda imetoa tamko linaloonyesha kutoielewa kauli ya Rais Jakaya Kikwete, iliyoamuru wahamiaji haramu kuondoka nchini, hali inayoonekana kukwepesha hoja.

Rwanda kupitia waziri wake wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo, ilikaririwa ikieleza kwamba hawatajibu mapigo agizo la Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka Wanyarwanda wote waliolowea Magharibi mwa Tanzania kuondoka haraka.

Mushikiwabo alisema wako tayari kuwapokea na kuwalinda wote waliofukuzwa Tanzania kwa kisingizio kuwa ni wahamiaji haramu, akieleza kwamba anasikitishwa kwa kuwa Tanzania haikufanya jitihada yoyote kuwasiliana na Rwanda kuhusu suala hilo kabla ya kuchukua uamuzi huo.

"Ni uamuzi ambao umeshachukuliwa, hatukushirikishwa kwa namna yoyote na jukumu letu kama serikali na taifa ni kuwahakikishia ulinzi wote wanaokuja, na hili ndilo suala tunalolishughulikia kwa sasa," alisema.

Kwa mujibu wa gazeti la New Times, Mushikiwabo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba agizo hilo la Rais Kikwete pamoja na ushauri wa kuitaka Serikali ya Rwanda kuzungumza na wanamgambo hasimu wa FDLR waliopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), hayatayumbisha uhusiano imara baina ya Watanzania na Wanyarwanda.

"Sisi si majirani tu, tuna mfungamano imara baina ya watu wetu pia, tuna mfungamano wa damu, wa kibiashara, na mengine mengi ya kutufanya tuendelee kuwa pamoja," alisema na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania nchini Rwanda.

Watanzania wanaweza kuishi hapa kwa umri wowote wanaotaka. Tunawachukulia kuwa ni watu wetu muhimu kwenye fungamano la Jumuiya ya Afrika Mashariki," alisisitiza.

Rais Kikwete wakati akihitimisha ziara yake mkoani Kagera alitoa agizo la kuwataka wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu ama kuondoka au kuhalalisha ukazi wao, huku akitoa wiki mbili kwa zoezi hilo kutekelezwa, kabla ya kuanza kwa operesheni ya kuwasaka watu hao.

Kauli hiyo ilitokana na kushamiri vitendo vya kihalifu katika eneo la Kanda ya Ziwa, Rais hakutaja jina la nchi ya wahamiaji hao. Kwa ukanda huo Tanzania inapakana na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.

Pia, Rais Kikwete katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi alizungumzia kusikitishwa na kauli za shutuma, kejeli na udhalilishaji zilizotolewa na Rais Paul Kagame wa Rwanda dhidi yake.

Mvutano baina ya Rwanda na Tanzania ulianza kuwekwa hadharani Mei mwaka huu, baada ya Rais Kikwete kuishauri Rwanda kukaa na kuzungumza na FDLR wenye makao yao DRC, hatua ambayo haikuifurahisha Serikali ya Rwanda.

Wakati Rwanda ikieleza hayo jana Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alizungumza na gazeti hili, na kutaka majibu ya kauli hiyo ya Rwanda yatolewe na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mkumbwa Ally alisema kauli iliyotolewa na Rais Kikwete ilikuwa ni ushauri, kwamba Rwanda wanaweza kuukubali ama la.

"Kilichomkasirisha Rais Kikwete ni lugha za matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa Rwanda, ila kwa hicho walichokisema sidhani kama kitakuwa na tatizo kwetu," alisema Mkumbwa.

Alifafanua kwamba, alipokuwa mkoani Kagera Rais Kikwete hakutoa agizo la Wanyarwanda kufukuzwa, bali alitoa agizo la kuanza kwa operesheni ya kuwakamata wahamiaji haramu, wale wanaomiliki silaha kinyume na taratibu.

"Rais alizungumzia masuala ya jinai ‘Criminal Element', siyo kuwafukuza Wanyarwanda," alisisitiza.

Hatutazungumza na FDLR

Waziri wa Mambo ya Nje, Louise Mushikiwabo, aliendelea kusema sera ya Rwanda kuhusiana na makundi ya aina hiyo, iko wazi na haitabadilika, kauli ambayo amekuwa akiirudia kila mara na kuwataka wote wanaofikiria kuhusu Rwanda kuzungumza na FDLR kwa namna yoyote kusahau wazo hilo.

"Kama umehusika kwa namna yoyote na maangamizi, wewe utakuwa adui wa kila mtu. Ni wazi kwamba Wanyarwanda wote watakuwa kwenye majonzi iwapo kwa namna yoyote kutakuwa na mawasiliano ya FDLR," alifafanua.

Kundi la FDLR ambalo ni kifupisho cha Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, linaundwa na watu walioshiriki kwenye mauaji ya kimbari yaliyowalenga watu wa kabila la Watutsi mwaka 1994, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000 kwa miezi mitatu.

Kundi hilo ambalo limeweka makazi yake mashariki mwa DRC, linadaiwa kufanya mashambulizi kadhaa yakiwamo ya milipuko ya mabomu nchini Rwanda, ambapo mwezi uliopita shambulio la aina hiyo mjini Kigali lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi watu kadhaa.

Uhusiano wa kihistoria

Familia za Rwanda zikiwamo zilizoishi Tanzania tangu miaka ya 1950, zimeelezwa kuwa zimekuwa zikiwasili nchini humo kupitia mpaka wa Rusumo baada ya agizo la Rais Kikwete kuwataka wawe wameondoka ndani ya wiki mbili, kabla ya kuanza kwa operesheni rasmi ya kuwaondoa.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini Rwanda, mamia ya Wanyarwanda waliokuwa wakiishi mkoani Kagera ambako ndiko Tanzania inapopakana na Rwanda wamekuwa wakirejea kwa wingi, ambapo hadi juzi, zaidi ya watu 300 walikuwa wameshaorodheshwa kwenye ofisi za Uhamiaji.


Pia, soma: Kagame tells Kikwete "I will hit you......"
 
Sioni tatizo kwa wanyaruanda kurudi kwao. waende wakaijenge nchi yao nasi watuachie TZ yetu. Ni ajabu wanasikitika kurudi kwao wanataka kukaa ugenini hadi lini? wengi wao wako kwenye mapori ya Burigi na biharamulo wasije siku moja wakasema eneo hilo ni lao na kuanzisha vurugu kama wanazofanya wenzao wanyamlenge kule kongo. Tusitengeneze wanyamulenge wengine TZ. waondoke na mifugo yao na kila kitu walichokuja nacho.
 
.....aaaarrgghhh ile habari tena,

single ya Kagame, ishachuja, at least for now. Sasa tuna taharuki ya viongozi na wanaharakati wa dini kuwa target ya kuuliwa na polisi mchana kweupe. Serikali na vyombo vya dola kuwa against wananchi wake. This is only made in Tanzania.

Kagame asubiri kwanza, tusafishe nyumba yetu, mpaka iwe stable. Ikishakuwa safi tutaanza tena bifu kama kutakuwepo na sababu, ila kwa sasa tunachoweza kusema ni kwamba tunawapenda sana wanyarwanda, wahutu kwa watutsi, na sisi msimamo wetu ni ule ule kwamba, hakuna mwenye hati miliki ya rwanda, si mhutu wala mtusti wala nan, Rwanda ni ya wanyarwanda wote bilakujali rangi, kabila, dini etc etc.

Kwa hivyo kama kuna tofauti zozote ziwe za kisiasa, kiitikadi au nyingineyo 'meza ya mazungumzo' ndio njia muafaka ya kufikia consensus. Na katika hili, wala tusikuze mada, kama majirani zetu hawataki kuchukua na kufanyia kazi ushauri wetu, basi hamna shida na wala hakuna kinyongo, tukubaliene katika kutokubaliana....and life goes on! No hard feelings, hakuna cha "Ï will wait and hit him at the right time and place", hiyo hakuna, rest be assured; yote hayo hakuna kwa roho kwatu kabisa

Otherwise, asante kwa kukubali kukaa na watanzania wenye kuishi huko kihalali. Maana sisi shida yetu ni hawa ambao hawako kihalali, japo pia tumewapa muda wa kuhalalisha ukaazi wao. Kama hawataki kufuata taratibu, then they have to go back where they are coming from. It can be uganda, DRC, Rwanda, India, amerika etc

stay blessed
 
Watu kama dr. Slaa wanawapa hawa jamaa kiburi kuona kwamba kumbe kuna watanzania wanaovumilia ushenzi wao!!!
 
Kikwete yupo sahihi nchi yetu ina wahamiaji haramu wengi sana wengine ni majambazi, wezi na matapeli na kikwete hakumaanisha wanyarwanda haramu tu bali wahamiaji haramu wote toka nchi mbalimbali na kama walijua sisi ni wamoja mbona walimtukana raisi wetu? Bila sababu, vyombo vya ulinzi fanyeni kazi wote waondeke
 
Asanteni sana wanyarwanda kwa kutuvumilia sisi watanzania tunaofanya shughuli zetu KIGALI .
 
Hii habari inarudiwa mara ngapi? kwa sasa habari ya mujini ni Sheikh Ponda!!!
 
Hawa watutsi siyo watu wa kuwalea hata kidogo ni wakulejesha RWANDA tu sababu ni watu wenye ROHO MBAYA kuliko makabila yote yanayopatikana Afrika Mashariki na kati, warudi tu kwao pazuri.Kwa yeyote ambaye hajawahi kuishi na hawa watu anaweza kusema ni watu wazuri mno wanapokuwa wanaimba KWAO PAZUURI lakini ni wabaya kuliko hata shetani.Sisi watu wa BURIGI Tunamshukuru sana Rais Kikwete kwa kazi nzuri aliyoianzisha juu ya hawa watu.Pia tunamshukuru sana mchungaji CHRISTOPHER MTIKILA Kwa kuyaweka hazarani madudu waliyokuwa wanatufanyia hawa WATUTSI.Hawafai hata kidogo.
 
Asanten sana wanarwanda, malumbano hayajengi, kama vipi tundumishe umoja.
 
Huyu waziri angefafanua pia kauli za Kagame dhidi ya Kikwete, kwani ndizo zimechchea yote haya!
 
Huyu waziri angefafanua pia kauli za Kagame dhidi ya Kikwete, kwani ndizo zimechochea yote haya!
 
Hajaifafanua ile kauli ya jemedari wake kwa rais wa Tanzania 'sympathizer' ndugu J.M. Kikwete kuwa I'LL HIT HIM AT THE RIGHT PLACE.

Huyu waziri, hebu angeifafanua na ujumbe/maudhui yaliyobebwa kwenye hiyo statement ya General Kagame ndipo aeleweke vema.
 
===>> Kuna jamaa mmoja wa KINONDONI KAOA MNYARWANDA....asipomrudisha kwao NAMSEMA KWA POLICE.... amrudishe haraka alafu aoe mmakonde wa hapa Dar.... chezea Serikali ....
 
Watimke tu tushawachoka, wanatuharibia nchi yetu.....

Mkuu, wala tusitafute mchawi, wanaoiharibu nchi hii ni Watanzania 100% tena wasomi. Tusiwasingizie wahamiaji, tena haramu!!
 
Kikwete yupo sahihi nchi yetu ina wahamiaji haramu wengi sana wengine ni majambazi, wezi na matapeli na kikwete hakumaanisha wanyarwanda haramu tu bali wahamiaji haramu wote toka nchi mbalimbali na kama walijua sisi ni wamoja mbona walimtukana raisi wetu? Bila sababu, vyombo vya ulinzi fanyeni kazi wote waondeke

amejua lini?
 
Serikali ya Rwanda siyo lazima ielewe tamko la rais Kikwete. Ili mradi wanyarwanda wahamiaji haramu wameelewa, basi inatosha.
 
Yaani waziri ndio anamjibu rais wetu...i thought his counterpart should have done that...kweli bado kagame anamdharau rais wetu ati sio saiz yake ndio mana kamuagiza waziri...nami namshauri kikwete issue yoyote ya rwanda ridhwani ndio awe anatoa tamko...implication yake rwanda bado watoto sana
 
Back
Top Bottom