Rwanda yaandika barua UN kupinga kupelekwa Jeshi la SADC DRC. Yasema sio jeshi la kulinda amani bali kuivamia Rwanda na kuwafuta Watutsi wa Congo

Berlin conference in modernity.
 
Kwanini waasi wa FLDR wasikae mezani na Kagame, ili waingizwe ndani ya Jeshi la Rwanda?. Halafu Tishekedi akaendelea kuwasafisha M23?, Kwa kupata msaada kutoka Tz?.
Kuna kipindi wakati Kikwete alipokuwa rais alitoa hili wazo. Kagame alimcharukia kidogo aanzishe vita na Tanzania.
 
Mambo ya ndani ya Congo Rwanda inamhusu nini wewe libavicha?
 
Sasa kwanini unataka waasi wa m23 waingizwe jeshi la congo kwanini kagame asiwachukue awaingize kwenye jeshi lake?
 
Ikiwa Congo Dr itamegwa na Kivu ikajitenga basi ushawishi kijeshi na kiuchumi wa Tanzania hapa East Africa utapungua kama sio kuisha kabisa. Natamani kumwona Samia ana declare FULL SCALE war na mamluki wa RDF waliopo Congo DR.
 
Swala kwamba kuna wa Congo wenye asili ya kitusi sio hoja,zamani walikuwa wanaitwa wanyamurenge, DRC haiwatambui kama ni raia, sasa DRC inataka iwafukuze waende Rwanda, lakini ardhi Yao ibaki kuwa ya Congo! Fikiria useme wamasai wote warudi Kenya, uende Arusha, uwafukuze wote waende Kenya, Ila ardhi Yao ibaki TZ! Kama, huwataki,Rudisha Arusha kwa, Kenya ikiwa, na wamasai wake.
Rwanda inawatumia kuiba madini, na kuna wadau wakubwa, Makampuni makubwa ya madini, yanayopeleka siraha ili hii Vita isiishe. Kila simu na computer inayotengenezwa duniani, madini yantoka Congo,
Dawa hapa, ni kukata mirija inayowapa siraha M23, winda na ua wafadhili wao, kimya kimya,
 
Tishekedi aruhusu Jeshi la Rwanda limsaidie kuwasafisha Waasi wa FLDR halafu akae mezani na M23 ili waingizwe kwenye Jeshi la DRC lakini kukimbilia kuomba Msaada wa SADC bila ku deal na MZIZI WA FITINA ni kupoteza muda tu.
Yaani fisi unampa nafasi ya kulinda butcher?
Eti Kagame apewe jukumu la kuwaondoa M23, how?
Hivi wewe hujui M23 ni jeshi la Rwanda?
 
M23 wamekaa hotelini Kinshasa miezi minne kuitikia with wa serikali ya Congo kufanya majadiliano hakuna kiongozi aliyefika hata kuwasalimia ikabidi wajiondokee na madeni ya hotelini wakalipa wenyewe.
Hii ilikuwa ni baada ya mivutano ya muda mrefu huki wakigoma kulegeza masharti yasiyotekelezeka.
 
Nakushauri fanya utafiti wa kina kuhusu FDLR wanaopigana huko Eastern DRC ujiridhishe wanapigania nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…