aloooo.....humu jamii kuna vituko...eti nini?well sijajua elimu yako...
kwli ni land-locked if u really are learned huwezi argue hivo economically imekula kwetu...na ndo maana umeona bwana PK anatafuta mbadala kabla hakijanuka zaidi...politics is killing us
Hata wale watanzania waliokuwa wanapeleka biashara zao nchini Rwanda nao wameathiriwa na fukuto hilo. Wamepewa masharti magumu ya kupeleka bidhaa nchini humo pia wamepandishiwa ushuru maradufu..
Hata wale watanzania waliokuwa wanapeleka biashara zao nchini Rwanda nao wameathiriwa na fukuto hilo. Wamepewa masharti magumu ya kupeleka bidhaa nchini humo pia wamepandishiwa ushuru maradufu..
kwli ni land-locked if u really are learned huwezi argue hivo economically imekula kwetu...na ndo maana umeona bwana PK anatafuta mbadala kabla hakijanuka zaidi...politics is killing us
.....Mimi nafikiri ili kuweza kutatua migogoro hii serikali ya tz inapaswa kwanza kuangalia athari mapema kabla ya kuruhusu kujitoa kwa nchi hizi tegemezi kwa matumizi ya bandari yetu.
ni jambo la kushangaza serikali inapoweza kupigia kelele suala la ziwa malawi wakati hakuna tunachoingiza pale zaidi ya wananchi tu kujitafutia riziki zao kwenye hilo ziwa malawi.
... serikali ijaribu kuonyesha sasa nguvu kama ilizoonyesha kwenye mgogoro wa ziwa malawi ambalo kiuhakika sio letu. na inachotakiwa isikilize kero za watumiaji wakuu wa bandari hii kwa faida ya nchi na si kukaa kimya kwa maslahi ya vijitu vichache tena viroho vyenye uchu wa kutafuna uchumi wetu.
TAFAKARI CHUKUENI HATUA..
.....Mimi nafikiri ili kuweza kutatua migogoro hii serikali ya tz inapaswa kwanza kuangalia athari mapema kabla ya kuruhusu kujitoa kwa nchi hizi tegemezi kwa matumizi ya bandari yetu.
ni jambo la kushangaza serikali inapoweza kupigia kelele suala la ziwa malawi wakati hakuna tunachoingiza pale zaidi ya wananchi tu kujitafutia riziki zao kwenye hilo ziwa malawi.
... serikali ijaribu kuonyesha sasa nguvu kama ilizoonyesha kwenye mgogoro wa ziwa malawi ambalo kiuhakika sio letu. na inachotakiwa isikilize kero za watumiaji wakuu wa bandari hii kwa faida ya nchi na si kukaa kimya kwa maslahi ya vijitu vichache tena viroho vyenye uchu wa kutafuna uchumi wetu.
TAFAKARI CHUKUENI HATUA..
Hakuna haja ya kulalamika,cha msingi bandari ipanuliwe,vinunuliwe vifaa vya kisasa kufacilitate utendaji wa kazi,urasimu na kodi kodi ziangaliwe upya.kwa kufanya hivyo wenyewe watakuja
Na Raymond Kaminyoge,
Dar es Salaam. Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.
Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.
Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.
Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam, alisema Hanspope.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.
Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.
Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.
Kamati ya Bajeti
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Andrew Chenge alisema katika kikao kijacho cha Bunge, kamati hiyo itaibana Serikali kuhusu mikakati inayofanywa kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.
Mizani ni mingi pia kuna usumbufu katika kupima mizigo yao na kwamba hali hiyo inawaletea usumbufu wafanyabiashara wengi, alisema.
Alisema vitendo vya askari wa usalama barabarani kudai rushwa pia ni miongoni mwa vikwazo pamoja na urasimu mkubwa katika utoaji wa mizigo bandarini ikilinganishwa na bandari nyingine.
Ni lazima tujifunze kwa majirani zetu Msumbiji, upanuzi wa haraka wa Bandari ya Beira umekuwa kikwazo kwetu, kampuni nyingi zimeanza kuitumia bandari hiyo, alisema.
Chenge alikitaka chama hicho kuiandikia kamati hiyo mapendekezo yake ikiwa ni hatua ya kunusuru uchumi wa nchi ili waweze kuijadili bungeni.
Umoja wa nchi tatu
Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda na mwenyeji wao Yoweri Museveni walikutana mjini Kampala, Uganda na kuamua kuitumia Bandari ya Mombasa kwa shughuli zao.
Waliahidi kuimarisha ufanisi katika huduma za Bandari ya Mombasa ili kuhakikisha bidhaa zinafika mapema Uganda na Rwanda.
Pia walikubaliana kujenga reli mpya ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mombasa kwenda Kenya na Uganda.
Viongozi hao walikubaliana pia kushirikiana katika sekta ya nishati hasa ikizingatiwa kuwa Uganda imegundua mafuta.
Nchi hizo tatu ambazo zimeruhusu kwa raia wao kusafiri kwa vitambulisho pale wanapotembelea nchi tatu miongoni mwao, zitakutana tena Kenya mwezi huu.
Khaa!! point kuu ya kujitoa ni hii nanukuu " Alisema sababu ya Rwanda na Uganda kujitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam ni vikwazo katika barabara ikiwamo mizani mingi ya kupimia mizigo.Hakuna haja ya kulalamika,cha msingi bandari ipanuliwe,vinunuliwe vifaa vya kisasa kufacilitate utendaji wa kazi,urasimu na kodi kodi ziangaliwe upya.kwa kufanya hivyo wenyewe watakuja
wewe kweli ni krapu
hebu niambie unalinganishaje matumizi ya bandari ya watu wa rwanda na wilaya ya ilala au temeke??
if we lose DRC, then tutaumia zaidi, ila si rwanda (kama unavyodhani
Uganda sio watumiaji wakubwa wa Dar, they have been using Mombasa for ages
fanya homework yako wewe imbechili kwanza... hatuangalii bendera tunaangalia numbers
nalaabuk wahed
Hao wasafirishaji kwa nini hawaleti mchanganuo wa kitakwimu....
1. Inachukua siku ngapi kuondosha kontena bandarini (Dsm/Mombasa)
2. Gharama za uondoshaji huo zikoje?
3. Unatumia siku ngapi kusafirisha kontena kwenda Uganda ama Rwanda?
4. Kero za traffic police kwa Tanzania na Kenya zikoje?
Kubwa zaidi hao kina Hanspope watwambie tukiondoa mizani wanatuhakikishiaje kuwa hawatabeba mizigo zaidi ya uzito unaoruhusiwa???
Bila kufanya haya tutakuwa tunapiga siasa tu!!
Kikubwa serikali yetu iongeze ufanisi tu bandarini, barabara ziimarishwe, tufufue reli ya kati jambo ambalo kina Hanspope hawato-support....mwisho wa siku wafanya biashara wa Rwanda na Uganda wataangalia njia ipi inawapa faida!!!!