Rwanda kufanya uchaguzi wa rais Agosti, 2017

Rwanda kufanya uchaguzi wa rais Agosti, 2017

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Serikali ya Rwanda imetangaza tarehe za uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika mwakani. Kulingana na tangazo la lililotolewa baada ya kikao cha baraza la mawaziri uchaguzi huo utafanyika tarehe 4 Agost, 2017.

Shughuli za kampeni zitaanza mwezi Julai lakini hakuna tarehe rasmi iliyotangazwa kwa wagombea kuwasilisha hati za kugombea urais, licha ya kwamba tangazo hilo linasema wagombea watatangazwa kabla ya kuanza kwa kampeni.

Kwa mujibu wa katiba mpya ya rais Paul Kagame anaruhusiwa kuwania muhula wa tatu.
Image caption Ramani ya Rwanda

Mtu pekee katika kambi ya upinzani aliyetangaza nia yake ya kugombea urais ni kasisi wa zamani wa kikatoliki Joseph Nahimana.

Hata hivyo juhudi zake za kutaka kurejea nchini Rwanda wiki mbili zilizopita ili kuandikisha chama chake na kugombea urais ziligonga mwamba.

Kasisi Joseph Nahimana na wenzake watatu walikataliwa kuingia nchini Rwanda walipokuwa mjini Nairobi Kenya kuelekea Rwanda kutoka nchini Ufaransa anakoishi kama mkimbizi.

Serikali ya Rwanda haikutaka kuzungumzi lolote kuhusu tukio hilo, lakini mashirika ya Rwanda yanayotetea maslahi ya manusura wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 walikuwa wameanza kulalamika kuwa tovuti ya Padre Nahimana akamatwe kwa madai kwamba tovuti yake inaendeza na kuchoche fikra za mauaji ya kimbari.

Chanzo: BBC
 
wanapoteza ela kufanya uchaguz ambae mshnd anajulikana..wangesubiri tu hadi 2034 ndo wafanye uchaguzi
 
Watu wanampenda wenyewe PK wao, hao wengine vibaraka wanaotumwa ku destabilise nchi hawatakiwi kuchekewa.
 
Watu wanampenda wenyewe PK wao, hao wengine vibaraka wanaotumwa ku destabilise nchi hawatakiwi kuchekewa.
hapo ndo kuna shida, stability ya rwanda kama ipo kwa kagame tu, then rwanda ni unstable!................uimara wa taifa hautakiwi kujengwa kwa mtu mmoja. kagame atapita rwanda itaendelea kuwepo.
 
hapo ndo kuna shida, stability ya rwanda kama ipo kwa kagame tu, then rwanda ni unstable!................uimara wa taifa hautakiwi kujengwa kwa mtu mmoja. kagame atapita rwanda itaendelea kuwepo.

Kuna mijitu tumejaribu kuifundisha lakini wapi vichwa vimejaa maji matupu.
 
Huku ni kupoteza hela za wananchi bure tu, kama referendum ya kuvunja katiba ili kagame aendelee kutawala kwa mihula mingine "ilipitishwa" kwa zaidi ya 90%, uchaguzi huu ni wa nini?
 
Back
Top Bottom