RWANDA: FDLR Plan To Topple Kagame In 120 Days From Congo

Its time Rwanda has to stop killing their own people by nosense reason.
 
akili ndogo haiwezi tawala akili kubwa.wewe ulishamuuliza mkuu wa wa nchi ana tatizo gani na kagame?.Kuna kitu tena sio hii issue ndogo ya upatanishi.kuna kitu cha siku nyingi sana.wenye vichwa vya banzi hawezi kuona.
 
Mojawapo ya vitu ambavyo Kagame amefanya kuisaidia Rwanda kuepukana na huu mvutano wa kikabila ni kupiga marufuku identity ya makabila, na hata kwenye serikali ya RPF kuna viongozi Wahutu. Vyama vya siasa vinaruhusiwa ili mradi visiwe na mrengo wa kikabila na visiwe na identity ya kikabila. Alianzisha mahakama za Gacaca ambako wale walioshiriki katika genocide wanatubu na kusamehewa. Hata Wahutu waliokimbilia Congo walikaribishwa warudi lakini kwa maoni yangu wale ambao hawataki kurudi ni wale ambao mpaka sasa hawakubaliani na status quo. Na miongoni mwao ni FDLR. Sasa hapo utajiuliza hawa FDLR wanataka nini? They want to come back as a Hutu movement and if that is the case what is there to talk about with Kagame?
 
I hope jokaKuu na wote wanaomtetea Kikwete katika saga hili wataisoma makala hii.

Bado tunawasihi kama wana EA Wenzenu - Kaeni meza Moja ili muondoe tofauti zenu !! Kwani Rwanda ni ya Wanyarwanda Wote na Si ya PK na Wapambe wake !!
 

Mkuu Highlander Hapo umenena,Nikweli kabisa bila Maridhiano Migogoro haitoisha kamwe !!
 
Mkuu Jasusi nakubaliana na wewe Gen Kagame amefanya mambo mengi ya kuisaidia nchi yake,lakini pia Gen Kagame huyo huyo ana husika kwa kiasi kikubwa kukandamiza demokrasia Rwanda.Nina rafiki yangu aliyekuwa akifanyakazi mahakama ya kimataifa ICTR Mjini Arusha alinihakikishia hizo mahakama zza Gacaca hazina sifa ya kuitwa mahakama hata kidogo zaidi ya uhuni mwingine wa Kagame.

Kwanza mshitakiwa akipelekwa Gacaca lazima akubali kafanya kosa hata kama hakuna ushahidi wenye mashiko.

Pili Gacaca zinaongozwa na watu wasiokuwa na ujuzi wa sheria.

Mwisho Gacaca ni mahakama zinazo walenga na kuwadhalilisha wahutu hata pale ushahidi unapokosekana.Mtuhumiwa hawezi kutu ikiwa hajatenda kosa hilo ndiyo kosa kubwa la hizi mahakama za Kagame.

Mkuu wangu Jasusi umewahi kujiuliza safu ya uongozi wa juu wa jeshi la Rwanda lina wahutu wangapi ?.


 
Last edited by a moderator:
Highlander mkuu maelezo yako yanashibisha,hiyo vita haitaisha majeshi yake mara kadhaa yamejaribu kukifuata kikundi cha FDLR huko kilikojichimbia yaani DRC ili kukifuta lakini wapi,sawa na M7anavyokimbizana na KONYI huko uganda.Cha msingi PK asahau kuwa atatawala Rwanda milele suluhu ni kupatana tu na kukubali kuwa wamoja.
 

Mkuu Vonix, unajua kichaa ni kitu tricky sana. Hitler alikuwa kichaa. Idd Amin alikuwa Kichaa. Kichaa ujue si lazima aokote makopo. Kuna vichaa wanapigiwa hadi salute. Kuna vichaa wanavaa hadi suti ukadhani ni mtu normal. Kichaa kwa maana ninayotaka kuitumia hapa ni mtu detached kutoka hali halisi--detached from reality.

Reality katika situation ya Rwanda ni kwamba Wahutu na Watusi ni watu wanaotakiwa kukaa katika nchi moja. Kinachotakiwa kufanywa ni kukaa wapange hiyo namna ya kukaa pamoja. And that has to be done by talking--NOT fighting.

Unahitaji kichaa kutokuona reality hii. Na dawa ya vichaa ni kuwatandika watoke madarakani. Kuna mtu ni lazima atoke madarakani pale Rwanda. The earlier, the better!
 

Maelezo yako ni mazuri vya kutosha Mkuu. Lakini yameacha kipengele muhimu sana bila kukijadili. Soma hapo kwenye RED utanielewa sasa.

Kikwete alipendekeza mazungumzo kwa lengo la ku-deal na hiyo sehemu yako yenye RED. Kama FDLR hawakubaliani na status quo, kuna sababu. Swali zuri umeuliza: Hawa FDLR wanataka nini? Jibu la swali hili linapatikana kwenye meza ya mazungumzo--preferably atakuwepo referee ambaye ni neutral na hizi pande mbili zitafika mahala zinakubaliana what is best for their country. Mazungumzo ndiyo njia sahihi ya kuenda. Siyo vita!

Kwa hiyo Kikwete anaweza kuwa kuna jambo kafanya ndivyo sivyo hapa nyumbani, lakini katika hili la Rwanda hakuna hata chembe moja ya kosa hapo. They should come together, sit down and talk! Somewhere, somehow!
 
I hope jokaKuu na wote wanaomtetea Kikwete katika saga hili wataisoma makala hii.
Jasusi,

..Rwanda wanasaidia M23, na DRC wanasaidia FDLR.

..DRC wanafanya mazungumzo ya amani na M23, sasa kwanini Rwanda hawazungumzi na FDLR?

..binafsi sielewi nyinyi mnaomshabikia Kagame hoja yenu ni nini haswa. we have already tried WAR and 3 million Congolese have died. Since u dont belive in peace talks, the come up with a different idea on how to bring this conflict to an end.

NB:

..FDLR ilianzishwa in 2000 kwa msaada wa DRC.

..sasa jiulize Rwanda na Uganda wamekuwa wakifadhili uasi dhidi ya DRC since when.

..unawakumbuka kina Bizima Karaha, Wamba Dia Wamba, Jean Bemba?? Unakumbuka nani alikuwa anawa-sponsor?

cc😡 Dr.W.Slaa, Ben Saanane, Nguruvi3
 
Nakuunga mkono, kuwe na jukwaa la Rwanda tu, imeonekana wadau wako interested sana na Rwanda. [/QUOTE]
 
Kitendo cha Dr. Slaa kumkumbatia Kagame kinaleta maswali mengi sana!

Slaa ameingia deal gani na Kagame? Kwa manufaa ya nani?

Nadhani Hajamtetea wala kusema Kagame yuko right.....ni kwamba mtoa ushauri ameambiwa ajiangalie maana huo ushauri unamfaa yeye pia ajipe!
 
mkuu hebu mimi mnikumbushe John Bosco ntaganda,na General Nkunda hawa walikuwa M23 au?????? ila nahisi walikuwa wanasaidiwa na Rwanda.
 
akili ndogo haiwezi tawala akili kubwa.wewe ulishamuuliza mkuu wa wa nchi ana tatizo gani na kagame?.Kuna kitu tena sio hii issue ndogo ya upatanishi.kuna kitu cha siku nyingi sana.wenye vichwa vya banzi hawezi kuona.

wewe mwenye akili tujulishe sisi wenye vichwa vya panz tatzo n nin.?
 
I hope jokaKuu na wote wanaomtetea Kikwete katika saga hili wataisoma makala hii.

Hiyo ni propaganda tu.......hata Gen. Kayumba alipokimbia mtego wao wa kumkamata, waliishia kusema aliwapa watu mabomu walipue Kigali...!
 
Hii website ya watu wasio kurupuka na kuweka uzi husio na data.Ndio maana unaambia kuwa lazima ujue chanzo cha mgogoro.Kagame mara ya mwisho kuja Tanzania ni lini?unajua wewe?.sasa deep down.Jf for great thinkers.
 
Hapana. Kwa maoni yangu amani haiwezi kupatikana Rwanda kwa kuzungumza na FDLR. Ni kama vile umwambie Myahudi enzi za holocaust azungumze na Wanazi. Kikwete is still wrong on this.

Wayahudi hawakuivamia Germany kijeshi kama hawa wa'Tutsi' na RPF yao. Usifananishe holocaust ya ma'NAZI' na ya Rwanda ambapo pande zote mbili zilikuwa vitani na wote kupoteza watu sawasawa! Nyingine ni propaganda ambazo Kagame na wenzie wamekuwa wakizifanya kuhalalisha utawala wao wa kudumu/maisha Rwanda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…