Rwanda Demokrasia imekuwa kuliko Tanzania!

Sio demokrasia tu rwanda wamepiga hatua kubwa sana hata kiuchumi pamoja na kwamba waliku kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi kirefu. Tatizo la tanzania viongozi wetu wengi ni wasanii.
 
hujui demokrasia uchaguzi wa rwanda uliuona wewe? Wapinzani waliambiwa wameungana makundi ya wapiganaji yaliyoko kongo, wapinzani waligaili uchaguzi. Kagame alifanya uchaguzi kama kawaida na alikuwa peke yake,mmoja aliyekuwa anakubalika kama slaa aliwekwa rumande mpaka sasa hivi yuko ndani je hiyo ndo demokrasia?
 
msingi wa demokrasia upo kwenye kujiuzulu?
au sijakuelewa?

sasa upo kwenye nini?au upokwenye kuunda tume na kung'ang'ania madarakani hata kwa makosa yaliyo wazi nakuhitaji uwajibikaji??
 
Ukiona watanzania wana mbinyo wa kiuchumi kisha wanalalama hali ngumu eti kwa sababu viongozi hawafai. Hapo kuna dosari kubwa katika bongo zetu, ukisikia kiongozi basi lazima ujue pana wanao ongozwa. Midhali kiongozi kawekwa na hao wananchi ni vyema tukubali kuwa tofauti ya wananchi na wenye nchi samahani, nakusdia viongozi na waongozwa ni idadi yao tu. aghlabu viongozi huwa ni wachache na waongozwa huwa ni wengi.

ukiondoa hilo la idadi. kinachobaki wote waliyochagua na kuchaguliwa ni sawa tu. Nia zao, tamaa, uadilifu na hata kufikiri kwao kama maji ya mtungini na kwenye gudulia yote huwa yanatoka kisimani hilo gudulia na mtungi ni vyombo vya kuhifadhia kwa mujibu wa matumizi ya maji.
 
Back
Top Bottom