UmenenaWatu wanaochangia hii mada naona wengi hawaelewi chochote juu ya mgogoro wa Cuf.Ukweli ni kwamba Lipumba amepandikizwa na serkali kukivuruga chama cha CUF ambacho ni chama cha upinzani chenye nguvu.Jaji Mtungi na Lipumba ndio waliopewa kazi hiyo.Kwa hiyo mapambano ni Cuf halisi na Serkali ya CCM.Kwenye mapambano kuna kushinda na kushindwa.
wapatane na nani wewe wacha uccm hamuwezi kuuwa upinzani hapaHii kesi bhana inafurahisha
Pesa walizo chukua kina seif bila Lipumba kujua ni mali ya chama si wizi
Alizo chukua Lipumba ndio wizi.
Mi naona kuna mawili aidha wote hapo ni wezi tu au wote si wezi
Ebu CUF acheni uhuni, kaeni chini mpatane.
Swala hapa ni , je serikali ya CCM kupitia hazina na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa wamefata maadili kuruhusu pesa hizo za umma kutolewa kwa njia hii ya kutia mashaka hususani kipindi hichi cha mgogoro ndani ya CUF?Kafu wanaelekea kufa.NCCR walianza hivi hivi.Mbona sefu alichota milioni 200 bila ya Lipumba kujua Mtatiro hasemi
serikali kupitia msajiri inafanya makusudi ili kuua chama,Hii kesi bhana inafurahisha
Pesa walizo chukua kina seif bila Lipumba kujua ni mali ya chama si wizi
Alizo chukua Lipumba ndio wizi.
Mi naona kuna mawili aidha wote hapo ni wezi tu au wote si wezi
Ebu CUF acheni uhuni, kaeni chini mpatane.
wanaomuunga mkono SEIFVIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomwunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kinatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360, dhidi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, viongozi hao wanatarajia kukutana kesho katika kikao ambacho kitahudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Wadhamini wanaomwunga mkono Maalim Seif.
Kikao hicho pia kitahudhuriwa na wanasheria na wakurugenzi ambao kwa pamoja watajadili suala hilo na kutoka na uamuzi wa kwenda mahakamani.
“Unajua huo ni kama utakatishaji wa fedha za umma hivyo basi hatuwezi kukaa kimya ni vema hatua stahiki zikachukuliwa,’’ kilisema chanzo hicho.
Pia kilisema kuwa CUF upande wa Lipumba watafunguliwa kesi kila mmoja kwa uzito wake jinsi alivyoshiriki tukio hilo ambalo wameliita ni wizi wa utakatishaji fedha za umma.
Naye Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano na Umma, Mbarara Maharagande, alisema Sh milioni 80 ambazo upande wa Profesa Lipumba unadai zimetolewa, zipo na ni mali ya chama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa chama hicho asiyetambuliwa na Msajili, Julius Mtatiro, alieleza jinsi fedha hizo zilivyotoroshwa kutoka Hazina hadi katika akaunti ya Wilaya ya Temeke na kuishia akaunti binafsi ya mtu aliyetambulika kama Mhina Masoud Omary, kupitia Tawi la NMB.
Haki gani wakati waliopewa Fedha ndio wanaostahili kwa mujibu wa Katiba!Wacha waende pengine haki yao itapatikana huko...!
Hiki chama bora kifutwe tu, hakina la maana wala tija kwa watanzania kwa sasa, kama ni uwakilishi vyama vingine vitarecover nafasi yake..VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomwunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kinatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360, dhidi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.