Ruzuku yawapeleka CUF mahakamani

Ruzuku yawapeleka CUF mahakamani

mr mkiki

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
5,727
Reaction score
11,950
VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomwunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kinatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360, dhidi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, viongozi hao wanatarajia kukutana kesho katika kikao ambacho kitahudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Wadhamini wanaomwunga mkono Maalim Seif.

Kikao hicho pia kitahudhuriwa na wanasheria na wakurugenzi ambao kwa pamoja watajadili suala hilo na kutoka na uamuzi wa kwenda mahakamani.

“Unajua huo ni kama utakatishaji wa fedha za umma hivyo basi hatuwezi kukaa kimya ni vema hatua stahiki zikachukuliwa,’’ kilisema chanzo hicho.

Pia kilisema kuwa CUF upande wa Lipumba watafunguliwa kesi kila mmoja kwa uzito wake jinsi alivyoshiriki tukio hilo ambalo wameliita ni wizi wa utakatishaji fedha za umma.

Naye Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano na Umma, Mbarara Maharagande, alisema Sh milioni 80 ambazo upande wa Profesa Lipumba unadai zimetolewa, zipo na ni mali ya chama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa chama hicho asiyetambuliwa na Msajili, Julius Mtatiro, alieleza jinsi fedha hizo zilivyotoroshwa kutoka Hazina hadi katika akaunti ya Wilaya ya Temeke na kuishia akaunti binafsi ya mtu aliyetambulika kama Mhina Masoud Omary, kupitia Tawi la NMB.
 
Wacha waende pengine haki yao itapatikana huko...!
 
hii serikari haitaki vyama vingi, ila cha ajabu, ccm haikufia mikononi mwa kikwete, imekuja kufia mikononi mwa magufuli!!
Haaaaa. Mlisema itamfia JK, CCm ikaendelea kupeta, leo itamfia Magu, mtaendelea kusubiri kama fisi anavysubirikono wa binadamu udondoke auokote
 
wakina nani hao, make inaonekana ni wengi,
halafu, hapo hakuna cha kusubiri maana kila kitu kimo katika maisha yanayoendelea,

na safari ni hatua, sasa hayo ni mambo yanayotokea tu, utayasubiri kwa kuacha kuendelea na mengine wakati maisha yanaendelea?

USA, NIGERIA SOUTH A, KENYA & other countries is the sample
with it
 
Hii kesi bhana inafurahisha
Pesa walizo chukua kina seif bila Lipumba kujua ni mali ya chama si wizi
Alizo chukua Lipumba ndio wizi.
Mi naona kuna mawili aidha wote hapo ni wezi tu au wote si wezi

Ebu CUF acheni uhuni, kaeni chini mpatane.
 
Hii kesi wa kushtakiwa ni tume waliowapa akina lipumba pesa siyo kuwashtaki akina lipumba hapo, kama wataishtaki tume ni sawa na kesi ya nyani umpelekee ngedere.
 
Mkuu wanaenda kumshitaki nan? Wakat lipumba anatambuliwa na msajili kwanini wanaendeleza mabishano wakati wanajenga nyumba moja? Hapo kwa cuf kuna watu nyuma yao je dhamira ya hao watu ni nn
kaka wanaend mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360?
 
Hii kesi bhana inafurahisha
Pesa walizo chukua kina seif bila Lipumba kujua ni mali ya chama si wizi
Alizo chukua Lipumba ndio wizi.
Mi naona kuna mawili aidha wote hapo ni wezi tu au wote si wezi

Ebu CUF acheni uhuni, kaeni chini mpatane.
Kwani Lipumba ni kiongozi wa CUF? Alishajiuzulu na kukaa nje ya chama mwaka mzima.
 
VIONGOZI wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaomwunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad, kinatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi ya uchotwaji wa fedha za ruzuku Sh milioni 360, dhidi ya mwenyekiti anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, viongozi hao wanatarajia kukutana kesho katika kikao ambacho kitahudhuriwa na wajumbe wa Baraza la Wadhamini wanaomwunga mkono Maalim Seif.

Kikao hicho pia kitahudhuriwa na wanasheria na wakurugenzi ambao kwa pamoja watajadili suala hilo na kutoka na uamuzi wa kwenda mahakamani.

“Unajua huo ni kama utakatishaji wa fedha za umma hivyo basi hatuwezi kukaa kimya ni vema hatua stahiki zikachukuliwa,’’ kilisema chanzo hicho.

Pia kilisema kuwa CUF upande wa Lipumba watafunguliwa kesi kila mmoja kwa uzito wake jinsi alivyoshiriki tukio hilo ambalo wameliita ni wizi wa utakatishaji fedha za umma.

Naye Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Uhusiano na Umma, Mbarara Maharagande, alisema Sh milioni 80 ambazo upande wa Profesa Lipumba unadai zimetolewa, zipo na ni mali ya chama.

Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi wa chama hicho asiyetambuliwa na Msajili, Julius Mtatiro, alieleza jinsi fedha hizo zilivyotoroshwa kutoka Hazina hadi katika akaunti ya Wilaya ya Temeke na kuishia akaunti binafsi ya mtu aliyetambulika kama Mhina Masoud Omary, kupitia Tawi la NMB.
Huu mpango wa kutorosha pesa ulipangwa na serikali na jaji Mtungi kaamurishwa kutoa hizo pesa kuwapa Cuf ya Lipumba.Kwa hiyo kwenda mahakamani kwa jaji alieteuliwa na raisi ni lazima atapindisha maamuzi kumfurahisha boss wake.
 
Cuf si ndio hao wako busy kuvunja Muungano, sasa kinawauma nini pesa za ruzuku za watanzania.
 
Hii kesi wa kushtakiwa ni tume waliowapa akina lipumba pesa siyo kuwashtaki akina lipumba hapo, kama wataishtaki tume ni sawa na kesi ya nyani umpelekee ngedere.
Watu wanaochangia hii mada naona wengi hawaelewi chochote juu ya mgogoro wa Cuf.Ukweli ni kwamba Lipumba amepandikizwa na serkali kukivuruga chama cha CUF ambacho ni chama cha upinzani chenye nguvu.Jaji Mtungi na Lipumba ndio waliopewa kazi hiyo.Kwa hiyo mapambano ni Cuf halisi na Serkali ya CCM.Kwenye mapambano kuna kushinda na kushindwa.
 
Wata kuja, kushtuka wamebaki na mbao hata chama cha juzi kitawapita
 
Kafu wanaelekea kufa.NCCR walianza hivi hivi.Mbona sefu alichota milioni 200 bila ya Lipumba kujua Mtatiro hasemi
 
KAFU MANDEVU kila siku wanapigwa wao tu maana wamekuwa mdebwedo. Inavyoonekana BUGURUNI ina nguvu zaidi ya VUGA.
 
Back
Top Bottom