Ruzuku kwa vyama inatolewa ya kazi gani kama mikutano imezuiwa?

MUSUMIFYCOM

Member
Nov 28, 2012
55
28
*WASOMI HAMUONI HILI*

*USALAMA WA TAIFA HAMUONI HILI*
Mh rais unatoa ruzuku kwa vyama vya siasa kila mwezi moja ya kazi kubwa ya ruzuku hizi ni kuhakikisha chama kinajijenga,kinafanya mikutano na kulipia gharama zote za harakati na siasa, hivi kama unapiga marufuku siasa mpaka 2020. Je hizi pesa zinatolewa kwa kazi gani?

*Hebu tutafakari wote*
By *musumi (RAIA WA TANZANIA)*
 
Labda Hiyo mikutano UKAWA wangekua wanatoa semina za ujasiriamali Sawa. Mikutano ya siasa inanisaidia nini mimi Mwananchi niliye hoehae huku kijijini.?
 
Kwa hiyo unakubali pesa ya ruzuku iende kwenye vyama ikaliwe tu bila sababu. Wakati unajua ni kodi ya wananchi itumike kama ilivyo kusudiwa.
 
Wanasiasa wanaishiwa hoja sasa, Magufuli hajazuia thatswhy Lowasa alikutanika na bavicha pale karimjee jirani kabisa na Ikulu. Labda kama wanamaanisha Mangungu
 
President Magufuli did n't ban all forms of politics. Soma huo uzi utakusaidia
Nawe siku hizi umekuwa kopo tu unashabikia kila kitu. Kipindi anaongea hukumsikia? au uliziba masikio. Wacha tuvurugane tu labda ndo tutakaa chini kuelewana. BAVICHA wasibadili msimamo wao. Hivi mnadhani polisi wao hawana roho wana vyuma? au roho zao haziwezi kutoka? Amani ivurugike kwanza ndo akili ya kukaachini kusuluhishana itarudi.
 
Labda Hiyo mikutano UKAWA wangekua wanatoa semina za ujasiriamali Sawa. Mikutano ya siasa inanisaidia nini mimi Mwananchi niliye hoehae huku kijijini.?

longu livu;
Kweli kabisa, labda hiyo mikutano ya UKAWA wangelitoa semina za ujasiriamali huko vijijini. Huyu mleta hoja kauliza, kama mikutano ndo hivyo imepigwa ban, wewe kapuku utasikiaje hayo ya ujasiriamali wakati hata kusanyiko la ndani ni makurufu?? Wewe unatamani ufunzwe ujasiriamali wakati hao wa kukufunza hawana ruksa kukutana na wewe?? Hayo mawazo yako, mwombe basi aliyepiga ban kwamba afungue awaambie hayo ma UKAWA yaje kijijini kufundisha ujasiriamali. Ila, elewa kuwa, ili watu hao UKAWA, watimize lengo na mikakati yao, na kuitumia kistahiki hiyo ruzuku, ka-siasa lazima kafungue semina na kufunga semina zote za ujasiriamali.
 
mkuu upo too defencive. pamoja na kuwa mimi ni mfurahishaji mkuu wa kupigwa marufuku kwa hawa makanjanja akina dj, ukweli ni kwamba serikali iliban political activities nje ya bunge. hiyo sio kauli ya rais tu hata prime minister na wengine wameiongea sehemu mbali mbali.
 
*WASOMI HAMUONI HILI*

*USALAMA WA TAIFA HAMUONI HILI*
Mh rais unatoa ruzuku kwa vyama vya siasa kila mwezi moja ya kazi kubwa ya ruzuku hizi ni kuhakikisha chama kinajijenga,kinafanya mikutano na kulipia gharama zote za harakati na siasa, hivi kama unapiga marufuku siasa mpaka 2020. Je hizi pesa zinatolewa kwa kazi gani?

*Hebu tutafakari wote*
By *musumi (RAIA WA TANZANIA)*
Mleta uzi unatakiwa kuelewa kusudio la matumizi ya ruzuku inayolipwa na serikali kwa vyama vya Siasa. Na iwapo ruzuku hizo zingetumiwa kama ilivyokusudiwa chini ya sheria #5/1992 vyama vya siasa vingekuwa vimekua na kuwa imara.

Kutumia pesa za ruzuku kwa gharama za mikutano ya hadhara tu ni kuendeleza wizi wa hizo ruzuku ndani ya vyama vya Siasa.

Kwamba ni viongozi wakuu wa vyama tu, kutoka makao makuu ya vyama hivyo ndio watumie ruzuku hizo kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara. Baadaye mabwana fedha na utawala wa vyama hivyo waandike ripoti zao kuwa billion kadhaa zilitumika kuendesha mikutano xy ya hadhara (hakuna cha kuonesha hapo iwapo mikutano ya hadhara ilifanyika kweli, na kama ilifanyika hizo ndio gharama zake halisi kweli au la). Hapo hakuna accountability.

Viongozi wakuu wa vyama wanaonufaika na ruzuku hizo hawataki ruzuku itumike kujenga uwezo wa vyama kiutendaji katika ngazi zote.

Chama kama Chadema, na hata huko awali kama ilivyokuwa kwa NCCR-Mageuzi au TLP, vilitakiwa kuwa na ofisi zenye watendaji wataalam wa kuajiriwa wakiwa na vifaa vya kazi maofisini kwao ngazi za matawi/vijiji/mitaa, kata, wilaya an mikoa. Kwa maana hiyo, hizo ruzuku zilitakiwa kulipia mishahara na posho za wafanyakazi wa vyama, pango za ofisi za vyama, vifaa kama kompyuta na wawsiliano ndani na nje ya vyama na pengine kulipia gharama za vikao vya vyama katika ngazi zote.

Utashangaa kuna maeneo mengi vijijini katika nchi hii kukuta chama cha Chadema hakina hata pesa za kutengeneza muhuri wa Mtendaji/Mwenyekiti wa chama ngazi ya tawi wakati chama kinapokea ruzuku (mabayo haijawekwa hadharani).

Ruzuku za vyama ni kwa ajili ya kulipia gharama za political administration ambazo hazimaanishi mikutano ya hadhara tu.
 
Labda Hiyo mikutano UKAWA wangekua wanatoa semina za ujasiriamali Sawa. Mikutano ya siasa inanisaidia nini mimi Mwananchi niliye hoehae huku kijijini.?
Hulazimishwi kwenda mkutano wowote. Hakuna sheria inayokulazimisha kuwa mwanachama wa chama chochote.
 
longu livu;
Kweli kabisa, labda hiyo mikutano ya UKAWA wangelitoa semina za ujasiriamali huko vijijini. Huyu mleta hoja kauliza, kama mikutano ndo hivyo imepigwa ban, wewe kapuku utasikiaje hayo ya ujasiriamali wakati hata kusanyiko la ndani ni makurufu?? Wewe unatamani ufunzwe ujasiriamali wakati hao wa kukufunza hawana ruksa kukutana na wewe?? Hayo mawazo yako, mwombe basi aliyepiga ban kwamba afungue awaambie hayo ma UKAWA yaje kijijini kufundisha ujasiriamali. Ila, elewa kuwa, ili watu hao UKAWA, watimize lengo na mikakati yao, na kuitumia kistahiki hiyo ruzuku, ka-siasa lazima kafungue semina na kufunga semina zote za ujasiriamali.
Ruzuku si kwa ajili ya semina za ujasiriamali. hata hivyo ujasiriamali haufundishwi kupitia mikutano ya hadhara. Ni kwa ajii ya gharama za kuendesha vyama vya siasa. Hakuna aliyepiga marufuku shughuli za kisiasa bali vyama vimeshauriwa kufanya siasa za usimamizi wa migao ya huduma kwa umma (entitlements) katika ngazi za uwakilishi na utawala (serikali za vijiji, kamati za mitaa, halmashauri na bungeni).
 
Sophist;
Nisamehe kwa sababu sio wote tulioumbwa na kipawa cha kuelewa mambo upesi. Nieleweshe kidogo. Hizo siasa za usimamizi huo, Je, zitafanywa kwa barua au mikutano??
Mkutano usipokuwa wa ualimu tena darasani na wanafunzi wake, ukiisha itwa hata na m/kiti wa kitongoji, unakuwa ni wa siasa au?? Hakuna kitakacho elezwa kufuta amri/maelekezo ya rais kuwa uchaguzi kwisha sasa siasa ni mpaka 2020. Labda ka nilisikia vibaya.
Mkutano wowote utakaofanyika popote, lazima uanze na ka-siasa kidogooo halafu kiongozi wetu huyo aongezee umuhimu wa chanjo ya polio. Japo twajua kuwa, diwani aliuitisha kuongelea umuhimu wa chanjo husika. Sawa sawa???
 
Aha, Kahangwa ameandika vizuri leo, bofya hapa: Magufuli didn’t ban all forms of politics....

Lakini pia nieleze kidogo tu kuwa dhana inayokusudiwa hapa ni siasa amabazo wawakilishi/viongozi wa vyama Bungeni, halmashauri, kamati za mitaa au serikali za vijiji wanashiriki siasa za kujenga hoja juu ya namna ambavyo migao ya rasilimali za umma (entitlements) inavyotakiwa kufanyika ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika kwa kuzingatia vipaumbele na standing orders zilizopo. Kwa mfano, si unajua JPM ame-commit serikali yake kupeleka Tzs 50 millini kila kijiji? Lakini pesa haitapelewa kugawiwa raia mmoja mmoja vijijini, la hasha, bali vijiji vinatakiwa kuwa na mipango na mikakati ya maendeleo. Lakini mipango na mikakati hiyo lazima ijadiliwe na wawakilishi/viongozi wa serikali za vijiji ili kupata efficient allocation ya resources na pia kudhibiti rushwa na matumizi mabaya ya fadha za umma. Hii ndiyo vision ya JPM kuwa badala ya wanasiasa, tena kutoka makao makuu ya vyama, Dar es Salaam, kuendelea kuendesha mikutano ya hadhara ya kisiasa kama ilivyokuwa wakati wa Kampeini za uchaguzi, sasa wawakilishi waliochaguliwa wapewe fursa na changamoto kutenda yale ambayo wanawajibika ku-deliver. Nimezungumza kwa kifupi tu.
 
Kwa hiyo unakubali pesa ya ruzuku iende kwenye vyama ikaliwe tu bila sababu. Wakati unajua ni kodi ya wananchi itumike kama ilivyo kusudiwa.
Ruzuku si kwa ajili ya mikutano ya kisiasa pekee. Rejea kazi za vyama vya siasa nchini, usikariri mikutano.
 
Nawe siku hizi umekuwa kopo tu unashabikia kila kitu. Kipindi anaongea hukumsikia? au uliziba masikio. Wacha tuvurugane tu labda ndo tutakaa chini kuelewana. BAVICHA wasibadili msimamo wao. Hivi mnadhani polisi wao hawana roho wana vyuma? au roho zao haziwezi kutoka? Amani ivurugike kwanza ndo akili ya kukaachini kusuluhishana itarudi.
Acha kutokwa povu. Uvurugane na nanani?
 
Back
Top Bottom