Ruvuma: CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Songea mjini

Unamsusia NGEDERE shamba la mahindi? Nini unategemea? Kususa hakujawai kumuacha mtu salama.

Upinzani ulipoteza dira toka uchaguzi wa mwaka 2015.

kuanza moja sio mbaya, tujipange tutengeneze SERA zenye mvuto.

UKWELI SIONI DALILI ZA UPINZANI KUSHINDA CHAGUZI ZA HAPA KARIBUNI.

KWA HOJA AU SERA IPI?

MWAKA 2019 na 2020 sio mbali vizuri upizani ukajipanga.

Sera za ccm zinaeleweka wakitumia mapanga dhidi ya upinzani? Nikuambie ccm haina sera wala mvuto, ndio maana inatumia mbinu za kikatili kujipatia madaraka. Uchaguzi wa juzi ndio mmegundua hamkubaliki kwa kiwango gani na ule unyama ni dalili za kutokukubalika kwenu. Hivyo huo uchaguzi mnaolazimisha kumwaga damu watu tumewapuuza shirikini wenyewe, pikeni matokeo kisha mkitoka hapo kesheni mkishangalia. Ila hata wananchi wamepata ujumbe kwamba mnatawala bila ridhaa yao.
 
Hivi ni visingizio vya kocha wa timu ya Kilimanjaro Stars.

Watu washawapotezea maana kama kanuni za mchezo zimewashinda mnataka watu washiriki nini? Vyama viko rafiki kibao, mnaweza shindana hata kikabila na kikanda huenda huko kukawa ba ushindani.
 
Mimi Mwenyezi Mungu kanipa Mtihani kidogo, bado sijabarikiwa watoto!!!

Ondoa Ofu.. endelea kumuaminia wala usiifikirie sana as haitakiwi na mwenza wako mpe amani usiyaongelee nae kabisa.. mumtumainie na yatakuja kupita.

Nakundondoshea baraka ubarikiwe kupata namba ya wanangu na kuizidi katika jina la Yesu Kristo.

Usisahau kunipa feedback mwakani mwezi huu.
 
Ondoa Ofu.. endelea kumuaminia wala usiifikirie sana as haitakiwi na mwenza wako mpe amani usiyaongelee nae kabisa.. mumtumainie na yatakuja kupita.

Nakundondoshea baraka ubarikiwe kupata namba ya wanangu na kuizidi katika jina la Yesu Kristo.

Usisahau kunipa feedback mwakani mwezi huu.
Inshallah.
 
Hawa huwa tumewazoea kususa!hii trick sidhani kama nyalandu atafurahia na sidhani kama waliposusa wakafanikiwa poleni sana makarai mna safari ndefu katika nchi hii
 
Mbona unatoka povu? Wewe ni msemaji wa NEC-Fisiem? Au wewe ndio Kailima???
Ndugu msipende kulaumu na kutupa shutuma kwa vitu msivyovijua... Hivi tujiulize ni lini CDM ilishawahi kuwasilisha malalamiko yake Tume ya Uchaguzi kulingana na sheria inavyooelekeza? Malalamiko yote ya CDM wanayatoa kwenye vyombo vya habari, So mlitegemea Tume ifanye kazi kupitia vyombo vya habari wakati kuna sheria inayoelekeza utendaji wa Tume ikiwemo hili la kushughulikia malalamiko yanayotokana na uchaguzi. Halafu kama walionewa kwenye uchaguzi mbona hawapeleki Mahakamani? mi nachoona hawa jamaa wameona kuliko kuendelea kupata aibu kwenye chaguzi kwa kushindwa ni bora ionekane hawakushiriki uchaguzi kabisa.
 
Kuna mpuuzi mmoja anajiita Ramadhan.....ni mpuuzi sana amewekwa pale kwa maslahi mapana sana ya walio madarakani....kazi yake kuwasulubu wapinzani........wakatae kabisa kwenda uchaguzi mwingine tena....wawaachie fisiem wapite tuuu la sivyo watakuwa wanawasindikiza maana policcm ndio wanawasaidia sasaaa
huyo unaemulaumu ni mtendaji na sio mwanasiasa, yy anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni na sheria zilizopo, tuwaombe wabinge wetu wa upinzani wapeleke hoja bungeni ya kurekebisha hizi kanuni kama hazifai
 

Zikiwa zimepita siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mheshimiwa Freeman Mbowe kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani utaofanyika Januari 13, mwakani kwa majimbo matatu na kata sita chama hicho mkoa wa Ruvuma kimetangaza kuunga mkono tamko hilo na kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Ruvuma Bw. Erenius Ngwatura amesema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Mwenyekiti wao wa taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubainisha kuwa uchaguzi wa udiwani uliopita kwa kata 43 uligubikwa na dosari kadhaa.

Kaimu Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea mjini Bw.Masumbuko Mbogoro ansema sababu nyingine ya wao kujitoa kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini ni kutokana na maombi yao kwa tume ya uchaguzi ya kutaka uchaguzi usogezwe mbele kutosikilizwa.

CHANZO: ITV
haya haya kumekucha
 
Back
Top Bottom