Ruvuma: CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Songea mjini

Udikteta wa chama ulimpoteza Chachawangwe
Hata wewe ukiambiwa uthibitishe hicho ulicho andika utashindwa kama ambavyo wanao dai lissu alipigwa risasi na serikali wanavyo shindwa kuthibitisha, hivyo achana na mambo ya hisia walio tangulia mbele ya haki waache walale panapo wastahili rudi kwenye mjadala , udikteta wa chama ambacho hakijawahi kushika dola una madhara gani kwa taifa??
 
Bila nidhamu bora msuse tu kwa kweli maana mtapigwa tuuh! Hakuna namna...
Uneaelewa unachoongolea au ndio walewale waimba pambio?? Maana nakuona kama unakichwa kizito kweli kuelewa upo kama zinduna usha elewa hiyo nidha inavyo shindikana kuwepo kwa mazingira kama ya uchaguzi wa madiwani ulio pita sasa unazungumzia kipi? Mimi naona ili watanzania wasiuliwe na wasijeruiwe na wasitekwe wala kukatwa mapanga bora upinzani ujiweke kando kwenye uchaguzi huu na ikiwezekana msajili wa vyama avifute kabisaaa vyama vya upinzan hadi hapo nchi itakapo kuwa na dhamira ya kweli kuhitaji vyama vingi.
 
Zikiwa zimepita siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mheshimiwa Freeman Mbowe kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani utaofanyika Januari 13, mwakani kwa majimbo matatu na kata sita chama hicho mkoa wa Ruvuma kimetangaza kuunga mkono tamko hilo na kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Ruvuma Bw. Erenius Ngwatura amesema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Mwenyekiti wao wa taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubainisha kuwa uchaguzi wa udiwani uliopita kwa kata 43 uligubikwa na dosari kadhaa.

Kaimu Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea mjini Bw.Masumbuko Mbogoro ansema sababu nyingine ya wao kujitoa kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini ni kutokana na maombi yao kwa tume ya uchaguzi ya kutaka uchaguzi usogezwe mbele kutosikilizwa.

CHANZO: ITV
Waongo hao tatizo lao kubwa hawana fedha kabisa.
 
Kususia kushiriki uchaguzi siyo ufumbuzi.Tutafute namna ya kushinikiza kuwa na tume huru ya uchaguzi.
Hivi vyama vina wabunge na wana uwezo wa kupeleka muswada juu ya yale wanayoyaamini na kuyasimamia.Badala ya kuja na porojo za kukimbia,kususia n.k.
Ifike wakati wabunge wawe watu wanaoaminika na wapiga kura wao.Wajue agenda iliyowapeleka kwenye jengo lile muhimu kwa mustakabali wa Tanzania yetu.
m
Mh. Mbowe na vijana wako, ni bora musimamie yale yanayoashiria kutuvusha.
 
Chadema wana nyuso mbili. Wanazitumiaga zote kwa wakati muafaka.

Yaani mkuu hadi nimesahau UKAWA walikuwamo kina nani.Siwasikii wengine sauti zao. Wako kimya mno. Muunganiko huu usije kuwa nao ni tatizo.
Hizi sura mbili za CHADEMA umezitaja hapa umenishtua upya.
Zinaweza kuwa SURA tu na sio SAUTI ya UKAWA. Kwenye kupigana na adui CCM lazima huu UKAWA utambue kama makamanda wao wana silaha zao wenyewe binafsi au wanategemea kukopa silaha kwa adui?

Kuna wakati msajili mwenye hatamu zake aliwahi kusema haitambuliki UKAWA kwa urasmi unaotakiwa . Nadhani wana UKAWA hawajawahi kufuatilia hili jambo pia.
 
Hata 2020 wasusie tu ili uchaguzi uende shwari.
Watasusa tu maaana bora roho za watanzania zibaki salama, maana huyu chinja chinja hana huruma, na ninadhan ndio mkakati wa chama cha mapinduzi nadhan msajili afute vyama vyote tubaki na chama kimoja pekee ili damu za watu zisiendelee kuwasakama polisi ambao ni wapokea amri tuu,
 
Zikiwa zimepita siku chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Mheshimiwa Freeman Mbowe kutangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani utaofanyika Januari 13, mwakani kwa majimbo matatu na kata sita chama hicho mkoa wa Ruvuma kimetangaza kuunga mkono tamko hilo na kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini.

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Ruvuma Bw. Erenius Ngwatura amesema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Mwenyekiti wao wa taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubainisha kuwa uchaguzi wa udiwani uliopita kwa kata 43 uligubikwa na dosari kadhaa.

Kaimu Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea mjini Bw.Masumbuko Mbogoro ansema sababu nyingine ya wao kujitoa kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini ni kutokana na maombi yao kwa tume ya uchaguzi ya kutaka uchaguzi usogezwe mbele kutosikilizwa.

CHANZO: ITV
Jamani wazee wa ufipa kubarini kataeni Mbowe upeo wake wa kuongoza chama umefika mwisho.Hivi nani asiyejua uchaguzi wa Arusha kwa Lema ulivyokuwa na figisu,uchaguzi wa Igunga baada ya Rostam kujiuzulu nk.Sasa leo akisema CHADEMA ijitoe kila uchaguzi maana yake nini?hiyo misuso ndiyo iliyomfanya Odinga akaangukia pua Kenya na sasa anatafuta njia za porini kujiapisha.Siasa ni mapambano.Remember Dr.Slaa,hii mashine wana-CHADEMA lazima muimisi this time.
 
Kususia kushiriki uchaguzi siyo ufumbuzi.Tutafute namna ya kushinikiza kuwa na tume huru ya uchaguzi.
Hivi vyama vina wabunge na wana uwezo wa kupeleka muswada juu ya yale wanayoyaamini na kuyasimamia.Badala ya kuja na porojo za kukimbia,kususia n.k.
Ifike wakati wabunge wawe watu wanaoaminika na wapiga kura wao.Wajue agenda iliyowapeleka kwenye jengo lile muhimu kwa mustakabali wa Tanzania yetu.
m
Mh. Mbowe na vijana wako, ni bora musimamie yale yanayoashiria kutuvusha.
Ni ufumbuzi wa haraka wakati jitihada za kutafuta suluhu zikiendelea kutafutwa maana kinyume na hapo roho za watanzania wenye mtazamo tofauti na chama tawala zitawalilia polisi maana wao ni watekelezaji tu, ili watu wasiuliwe tena kama arumeru na watu wasijeruiwe tena kama arumeru, na wasitekwe tena kama arumeru hakika bora kuto shiriki kwanza maana maafa ya wasio hatia yanaweza kutokea ,ni bora kukosa jimbo kuliko kuua roho za watu wasio hatia.
 
waache tu hakuna aliyewashika mikono kuwalazimisha ila uchaguzi utafanyika na mbunge atapatikana hakuna wanayemkomoa hadi 2020 waache pia urais wapiga kura tupo tutaenda kumpigia baba jesca
 
Hakuna cha chinjca chinja wala nini. Ni uwoga tu umewakumba hao Chadema. Kata moja dhidi ya kata arobaini na mbili sio mchezo ati.
Haina shida hasa ukizingatia nafsi yako ina ujua ukweli usio na shaka wa hali iliyo tokea kwwnye uchaguzi huo wa kata 42 , ni furaha tu ya kinafiki katika hilo , ushind wa mtutu wa bunduki na dam za watu hakika ni ushindi wa kishindo kwa wasio na akili , kuna watu wamezikwa arumeru na nadhan unalijua hilo, na kuna wengine tangu walipo tekwa hadi sasa hawaonekani nadhan tutakuja wakuta ufukwen , kuna wengine hawana miguu na viganja huko kisa madaraka ambayo wenye nayo watakufa na kuyaacha halafu wanaenda kujibia uuaji walio ufanya huku kama kweli kiama kipo.
 
waache tu hakuna aliyewashika mikono kuwalazimisha ila uchaguzi utafanyika na mbunge atapatikana hakuna wanayemkomoa hadi 2020 waache pia urais wapiga kura tupo tutaenda kumpigia baba jesca
Kuliko watanzania wasio hatia wauawe na kujeruhiwa bora kuachana na huu uchaguzi ili watanznia wabaki salama utu na uhai ni zaid ya madaraka bora kykosa madaraka kuliko watu wafe kisa madaraka.
 
Sasa na chama si kifutwe tu??
Itabidi iwe hivyo maana kwa mauaji na majeruhi yaliyo tokea arumeru hakika lengo kuu ni hilo
Vyama vya upinzan vikate tamaa na vifutwe na hayo huwa ni mawazo ya wajinga pekee ambao hata shule hawakwenda , tukiwa tizama CV zenu itakuwa umeishia firm two umejitahid sana ulifika form 4 with div 0 ndio maana hata elimu ya uraia tu kichwan haipo.
 
Kama hakuna mabadiliko yoyote hadi 2020 juu ya madai yanayowafanya msuse Leo maanake hata 2020 hamtashiriki otherwise utakuwa upumbavu.
 
...ushind wa mtutu wa bunduki na dam za watu hakika ni ushindi wa kishindo kwa wasio na akili , kuna watu wamezikwa arumeru na nadhan unalijua hilo, na kuna wengine tangu walipo tekwa hadi sasa hawaonekani nadhan tutakuja wakuta ufukwen , kuna wengine hawana miguu na viganja...
Hivi ni visingizio vya kocha wa timu ya Kilimanjaro Stars.
 
Back
Top Bottom